Dk Slaa: Sitagombea urais 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa: Sitagombea urais 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Balantanda, Nov 18, 2009.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Na Patricia Kimelemeta

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, amevunja ukimya na kueleza kuwa hafikirii kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Dk Slaa ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Karatu, alisema "Ikulu si mahali pazuri kukimbilia na urais si mchezo wa kitoto."

  Alisema wakati alipojiundoa katika upadre na kujitumbukiza katika ulimwengu wa kawaida, aliahidi kuwatumikia wananchi wa Karatu na si kutafuta njia ya kuingia Ikulu, ambako alisema kuna matatizo mengi yanayoweza kumfanya mtu kukosa usingizi.

  "Unajua Ikulu si lele mama, kunahitaji mtu mvumilivu hasa wananchi wake wanapohangaika na ugumu wa maisha ya kila siku, jambo ambalo linaweza kumfanya ashindwe kupata usingizi, kwa sababu ya mawazo," alisema Dk Slaa.

  Alisema kama mtu anataka kugombea nafasi hiyo anapaswa kukumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtu anayekimbilia Ikulu anapaswa kuogopwa kama ukoma.

  Alisema mtu wa aina hiyo mara nyingi anakusukumwa na maslahi binafsi kuliko maendeleo ya watu.

  Dk Slaa alisema maendeleo yanapatikana bila ya hata kuingia ikulu na kwamba la msingi ni viongozi kujipanga katika kupigania maendeleo ya wananchi.

  Alisema mkakati wake ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Karatu wananufaika na uongozi wake kwa kuwatafutia maendeleo na kuwaondolea kero kama ya maji na kadhalika.

  Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na uvumi kwa Dk Slaa ana mpango wa kuwania kiti cha urais kupitia tiketi ya Chadema.

  Kwa mujibu wa habari hizo, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, hana mpango wa kuwania tena nafasi hiyo na badala yake anakwenda kuwania ubunge katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro.

  Source:
  Gazeti la Mwananchi
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,607
  Trophy Points: 280
  Nilimsikia akizungumza kwenye redio, points zake za kutogombea ni very valid. Dr. Slaa ni true visionary leader and has a mission to accomplish.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Well maadam hakuweza kuyaona tunayoyaona sisi, namtakia kila la kheri... lakini 2015 hawezi kugombea kwani kila mwanasiasa nchi anasubiri wakati huo na nina hakika kwa asilimia kubwa sana vyama vingi vya Upinzani vitakuwa havina nguvu tena kwa wananchi..Mwaka huu 2010 ndio utakaopanga mustakabali wa miaka inayofuata..Mkombozi hachagui uongozi ila hali iliyopo ndiyo humsukuma kupigania haki hiyo kwa wananchi wake ambao hawana kiongozi.

  Sasa kama Dr.Slaa anapaona IKULU sii mahala pa kukimbilia, then wananchi walio chini ya Utawala uliopo wafanye nini... Pateni kura za ubunge haiwezi kubadiilisha kitu, wilaya na kata zilizokuwa na wabunge wa vyama pinzani zimekuwa na wakati mgumu kimaendeleo kuliko sehemu nyinginezo na wananchi na hasa maskini wanaliona hilo wazi kabisa na tabia ya maskini hawezi kuvumilia njaa kwa muda mrefu hata kama kuna haramu anachula haramu kuondoa njaa...Hawezi kuilaumu CCM isipokuwa chama kilichochukua jimbo..Yale maneno ya Pinda kule Kigoma!

  Kwa Muislaam ni halali kula nguruwe (CCM) ikiwa hakuna chakula kingine. ukipima uzito wa maneno haya ndicho kitakachotokea Tanzania..CCM ushindi wa Tsunami unakuja tena 2010.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wamechukua! wameweka! waah!
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Nov 19, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,908
  Trophy Points: 280
  Hata angesema anagombea, anamtisha nani CCM!

  Ameshakiharibu Chadema, amekubali kuwa mtumwa kwa nira ya kuheshimu waasisi na mwenyekiti, amehujumu nafsi yake mwenyewe!'kwenye miti hakuna wajenzi'

  Slaa anapendwa na wengi walio nje ya Chadema, walio ndani ya Chadema-mikoani wanajua na wanasema haya.

  Yeye ndiye aliyeongoza kubaka demokrasia na kukataa kutangaza matokea ya uchaguzi.ndiye huyu mnataka awe rais! give me a break!

  mmetukatisha tamaa
   
 6. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani hapa mkuu hata Makamba asingesema vizuri hivi. Umepiga kampeni nzuri sana kwa chama. Hongera sana Waberoya kwa job well done. Kidumu chama cha mapinduzi.
   
 7. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na ule muungano na CUF unavyokuja kwa kasi, nani atasimama against CCM?
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  This is what I think. Hawa wapinzani wengi wanajua kwamba chances za kupata uraisi ni mdogo. Kwa hiyo mtu anaona kama anaweza kupata ubunge ni bora aende huko apate maslahi ya ubunge. Tumeona mtu kama John Cheyo kajiamulia kugombea ubunge. Freeman Mbowe nae aliye gombea 2005 ana taka kurudi kwenye ubunge. Kwa hiyo mimi nadhani wengi wao siyo kwamba wanaona wao kuwa wabunge badala ya kugombea uraisi kuna manufaa zaidi kwa wananchi bali wao wana jijua kabisa kuwa chance zao za kupata urasi ni mdogo. Why run for the presidency and lose while you can be an MP right?
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=dIVfbylUU-M[/ame]​
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wameiba, wameiba wameiba. Kama kawaida yao. Na siku za mwizi ni 40.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,607
  Trophy Points: 280
  .

  Mkandara, mimi nimemsikia Dr. Slaa kwa masikio yangu, na nimemwelewa, ametumia maneno yale yale ya Nyerere kuhusu ikulu, para material, (neno kwa neno) amesema
  "Ikulu sio mahali pa kukimbilia, ukimuona mtu anataka kupakimbilia ikulu, ni wa kuogopwa kama ukoma".

  Maana yake, uamuzi wa kugombea, hautakiwi uwe wake, kama vyama vya upinzani vitakaa pamoja, na kujitathmini kuwa mgombea wa mmoja, na wote kwa kauli moja wakaamua mgombea atakaye tufaa ni Dr. Slaa, basi Dr ataingia ulingoni, hivyo kuifuta dhana ya kuwa anakimbilia, hapo atakuwa ameombwa.
   
 12. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa maandishi mekundu hapo juu nafurahi kujua kwamba hata wapinzani wanajua majukumu mengi na mazito aliyonayo rais wetu hata kumkosesha usingizi. Bravo slaa
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwani tatizo ni Ikulu? Hivi tunamfikiria Rais wa Tanzania kama Mfalme? Kwanini hatutaki kukubali ukweli wetu wa Kikatiba kuwa sisi ni Jamhuri?
   
 14. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Dk Slaa kugombea uraisi!!! Ni habari njema na yenye kuandikwa na kujadiliwa sanaa..

  Amekanusha hana mpango wa kugombea uraisi!!! Ni habari kubwa pia.
  Kama taifa mawazo ya mtu mmoja mmoja, kikundi, vikundi, na taasisi mbali mbali huonyesha aina ya jamii ilivyo.

  Dk Slaa amekuwa shujaa wa vita ya ufisadi kwa kuiasisi..Imetekwaa tayari vita hiyo na kikundi kidogo chenye kiu ya umaarufu kwa faida binafsi.. Wamelazimisha umma kuwakubali kama wapiganaji kwa kutumia nyenzo mbali mbali ikiwemo media...

  Tatizo la Taifa hili kwa sasa sio nani kuwa Raisi!!! Kilema hicho ndo bado kinatuumiza tukiamini Dr Slaa akisimama kugombea ni bora zaidi..Ataleta chachu ya ushindani kwa sifa aliyo nayo kulinganisha na wagombea wengine..Ndo kiu ya wengi labda...

  Kwangu tunahitaji kujenga mfumo wa kitaasisi wa kupambana na serikali iliyopo na sio personality tuu..Upinzani imara ni bora ukajengwa sasa kwa vyama vilivyopo kutambua nafasi ya mabadilko iliyopo na mwitikio wa jamiii...

  Tumeendekeza siasa za personality ambazo waliopo madarakani zinawafaidisha zaidiii...Mfano Raisi ni safi, mawaziri na wasaidizi wengine mzigooo..Fikra potofuuuuuuu..Tujenge uwezo wa kupambana na mfumo na sio watu. Watu wanapita..Alianza na mawaziri 60, leo kapunguza hadi 40s na ana mpango wa kuongeza vijana zaidi akifanikiwaa awamu ijayoo...Hatufaidi chochotee kama jamii kutatua changamoto za maendeleooo
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani kwa kuwa taasisi ya urais ni ngumu na inakosesha usingizi kwa nini tusibinafsishe kitengo hicho kwa kutangaza tenda ulaya? lli tupate rais rahisi, na atuongoze kwa mkataba maalum? Ebu tufikri kuibinafsisha magogoni pls.

  Shida yangu inakuwa kwamba kwa kuwa hatuna bado wanasheria maahiri katika mikataba na hapa tutabolonga kwa watu kudai 10% yao kwanza kabla ya mkataba.

  Au basi tumshauri yule rais wa Zanzibar anayemaliza muda wake agombee urais wa jamhuri na awaachie kafu kule pemba waendelee kutamba.
  Ni mawazo yangu.
  Nimechoka na nchi hii kwa kweli!
   
 16. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wapinzani wameshaona urais ni kazi ngumu kuliko walivyofikiria,sasa wameamua wenyewe kunyoosha mikono.Jamani kuwa kichwa cha Taifa ni kazi ngumu na si lelemama.
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani kura nyingi za ubunge zina maana kwa sababu iwapo wapinzani watakuwa wengi bungeni, itakuwa njia nzuri ya kuhakikisha serikali inawajibika kwani haitakuwa na nafasi tena kulifanya bunge kuwa muhuri tu wa kupitisha mambo yake.
  Sasa hivi serikali haina hofu sana kwa sababu inajuwa kuwa chama kinachoiongoza kina wabunge wengi, hivyo wanaweza kupitisha mambo yao bungeni kwa jinsi wapendavyo. Tukiwa na bunge lenye wapinzani wengi, serikali itakuwa makini sana kwa sababu inajua itakuwa rahisi kwa mipango yake hovyo hovyo kukwamishwa
   
 18. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,939
  Trophy Points: 280
  Mie namkubalia Slaa kuwa Uraisi acha Wananchi wakupe wao sio wewe uutafute maana huwezi kuitafuta kuikimbilia kazi unayojua ni ngumu bila kuwa na sababu zisizo wazi. JK alipanga mikakati wa kuupata Uraisi miaka 10 kabla kwa njia chafu na safi, leo hii yuko wapi na amefanya nini zaidi ya kuzikana ahadi zake na kushindwa kuwajibika katika kazi ambayo ameisotea kwa miaka 10 aipate? Waliomsaidia kuhakikisha anaingia Ikulu ndio wanaoikebehi kauli yake kuwa "Uraisi hauna ubia" kwa kumuonyesha kwa vitendo kuwa Uraisi wake wao wana Ubia atake asitake.
   
 19. M

  Magezi JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Labda kama mko nje ya nchi lakini mimi hili nililisemea kwamba kwa hali ya sasa ya vyama vya upinzani si rahisi kujihakikishia kwamba watashinda. Kwa hiyo mtu muhimu kama Dk. Slaa si vyema ajitupe huko kwa sababu wakishindwa hata mchango wake muhimu bungeni utakosekana na ndo mwisho wake kisiasa.

  Kuna watu muhimu kama Tundu Lissu na hata wengine wanaweza kujitokeza wakagombea, yeye abakie kwenye ubunge ili kuweka chachu bungeni.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu maana kubwa na yenye nguvu ya kukiita chama Mbadala ni uwezo wa chama hicho kuchukua madaraka. Hilo ndio linakuwa lengo kubwa otherwise vyama vyote vinatafuta kuwa na wabunge kulinda maslahi ya kile wanachokisimamia (mrengo).

  Tunaweza kuwa na wabunge 3/4 wa Upinzani, lakini kama watasahau malengo ya Upinzani hayatokani na matukio, basi hatusa sababu ya kuwa na bunge kubwa la Upinzani...kwa mfano, Ufisadi ni swala la Uvunjaji wa sheria ni tukio, lakini limewekwa kama vile ni agenda ya Upinzani..wabunge wanagombania hoja hiyo kila kona wakati huo huo wanaoendesha Ufisadi nchini ni wawakilishi wetu wa bunge na serikali, hivyo kugombea ubunge ni ktk kutafuta nafasi ya kujineemesha..

  Ni wabunge wangapi wanakubaliana na Dr.Slaa ktk maswala ya malipo makubwa kwa wabunge? Na wangapi wanakubaliana naye ktk Ufisadi wa EPA bila kuogopa vitisho vya Hosea kuhusiana na posho mbili mbili!. Kikatiba kinachotakiwa kubadilishwa ni posho lakini watakuwa radhi kuikosoa serikali ktk Ufisadi (tukio) lakini wazito kupitisha muswada unahusu Ufisadi huo (posho mbili)..
  Ubunge Tanzania ni uwakilishi bungeni tu, huna mamlaka ya kubadilisha jimbo lako pasipo baraka za chama tawala..mkuu wa mkoa na wilaya wote hawa ni wateule toka chama tawala...

  Amini maneno yangu, mkuu wangu zingatia sana watu na mazingira yetu..Akisimama Dr.Slaa kuna uwezekano mkubwa wa Mkandara kushinda ubunge Ukerewe, mfano tumekwisha ona kwa Mrema mwaka 1995 na JK mwenyewe mwaka 2005 kawabeba wabunge wengi sana..

  Maadam Mbowe alishindwa na JK 2005 leo anakwenda gombea Ubunge Hai, basi ni muhimu sana kwa Chadema kumweka mtu ambaye ataweza kushindana laa sivyo hakuna sababu ya kujiita chama mbadala ikiwa lengo la upinzani ni kutetea maslahi ya wananchi kwani kila chama cha upinzani ndio dhumuni na hatua yake ya kwanza..
   
Loading...