Dk. Slaa: Si uhaini kumng'oa rais Kikwete kabla ya 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa: Si uhaini kumng'oa rais Kikwete kabla ya 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, May 21, 2011.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Daktari (PhD) wa ukweli amemjibu Mukama kuwa wananchi wanauezo kikatiba wa kumuondoa JK madarakani kabla ya 2015. “Ibara ya 146 ya Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982, inasema wananchi ndio wenye mamlaka yote ya kumweka mwenyekiti wa serikali ya mtaa au kijiji na ndiyo wenye mamlaka ya kumwondoa wakati wowote kwa kupiga kura ya maoni.

  “Wakitaka hata kabla ya kipindi rasmi cha uchaguzi kufika....kwa hiyo kama ni halali kwa ngazi ya kijiji basi ni halali pia kwa ngazi ya urais kama wananchi wenyewe walio wengi wakiamua kufupisha muda wa serikali yao,” alisema Dk. Slaa.

  Kauli hiyo ya Dk. Slaa, imekuja siku chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, kusema kuwa Rais Kikwete hawezi kung’olewa kabla ya mwaka 2015 na kusisitiza kuwa kufanya hivyo ni uhaini.

  CHANZO: GAZETI LA TANZANIA DAIMA
   
 2. J

  John W. Mlacha Verified User

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  ina maana mukama hajui sheria za nchi?
   
 3. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,461
  Likes Received: 1,334
  Trophy Points: 280
  Anajua ila anasimamia na kutekeleza ilani ya CCM
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Tafsiri aliyotumia Dr nyepesi sana haiendani na hadhi yake
  Hata hivyo kuna "kuweza kumtoa" na kuna sheria pia imetamka bayana kuwa ni uhaini
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,620
  Trophy Points: 280
  ilani ya ccm inapingana na sheria za nchi?
   
 6. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hiyo ndiyo Sheria aliyosoma dr slaa bora akagombee uenyekiti wa kijiji huko kwao Karatu kwa urais anadhihirisha kua hatoshi.ndiyo maana alishindwa kusimamia. canon law akafukuzwa upadri!
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na wewe pia unajiona great thinker, eeh?
   
 8. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Duh shame on him! Mwenyekiti wa Kijiji anaweza kushtakiwa yaani hana kinga, kwahiyo na rais ni hivyohivyo! Kuongea sn wakati fulani ni kutafuta kuonekana mjinga. Hivi kuna clip ya hii kitu?
   
 9. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  labda tuanze na maana ya uhaini

  Uhaini ni pale mtu anapotenda jambo dhidi ya nchi yake. Kwa mfano, mtu anaweza kuisaidia nchi nyingine ipigane vita dhidi ya nchi yake kwa kuwaambia habari za siri. Uhaini ni neno la kawaida, lakini nchi tofauti zina sheria tofauti na adhabu dhidi ya matendo ya kihaini.
  Neno la mtu anayefanya uhaini ni msaliti. Miongoni mwa wasaliti maarufu duniani ni pamoja na Yuda, Benedict Arnold, Pétain na Quisling.

  SASA USALITI HUKO WAPI? DR SLAA NI MWANASIASA ANAYETUMIA NGUVU YA WANANCHI KUMTOA RAISI WASIYEMTAKA HUKO WAPI USALITI(UHAINI) HAPO,? Kwa tafusili hii ya usaliti (uhaini) ni kiongozi gani msaliti hapa nchini kwa kuwalaghai wananchi?

  kale watu walifungwa kwa kubebeshwa kesi nzito kama hizi lakini sasa ni wakati wa WELEDI mwanasiasa anayetumia majukwaa kamwe awezi kuwa muhaini maana hakuna anachofanya kasiri, sio kila mapinduzi ya serikali ni uhaini kama wamefanywa kwa nguvu ya umma kamwe sio uhaini.

  huu ni ujanja wa ccm kudanganya umma wasinge muacha Dr slaa kutembea huru na kesi ya kihaini halafu Arusha wamfungulie kesi ya uchochezi, mimi ni hakika kama kungekuwa na uhaini angekuwa UKONGA aU segere zamani sana kama kuna mtu anatafuli tofauti ya uhaini amwage hapa.
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Te hehe he! Mengi tutayaona! Hivi CHADEMA wanalilia serikali za Mitaa?
   
 11. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Du mbona unaruka tu wakati mwenyewe Dokta ameshasema sheria ni ya Serikali za Mitaa? Ku ch amb a kwingi huko kutawaadhirisha watu!
   
 12. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwako wewe demokrasia ni nini? Na nini maana ya chaguzi? Hizi kelele zinapoteza lengo sasa na hatimaye hata ile maana ya sensitisation inaondoka.

  Hivi kwanini kelele hizi zisipigwe kwenye katiba? Au kwanini nafasi hii na hizo rasilimali chache wangewekeza kwenye majimbo? Maana hii ni njia rahisi kujulikana kuwa chama kinataka kufanya nn kuliko sasa hivi msisitizo umekuwa ni vurugu.
   
 13. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kama kweli Dr Slaa kasema hivi,basi atakuwa amechemka na kajishushia hadhi.Mfano wa Rais na Mwnyekiti wa Kijiji wapi na wapi?
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Rudi home uitumikie nchi yako wewe acha longolongo!
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Walewale wa hoja za kopo la kuchambia.
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tanzania si kigenge cha wahuni! Wananchi wa Tanzania msiwafanye waovyo! Ni miezi sita tu nyuma walipewa hiyari na kumchaguwa waliemuona anawafaa. Walipofanya hivyo walikuwa wakijuwa kwa hakika kuwa watakuwa nae kwa kipindi cha miaka mitano!

  Hivyo hiki kipindi cha miezi sita kimeshatowa jawabu kuwa walikosea? na kipi kilichofanywa na CHADEMA cha kuwafanya wahisi walikosea kutokichagua?
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Nchi yangu chini ya dokta anaejifananisha na mwenyekiti wa kijiji nashindwa kujua niitumikie vipi. Hebu niongoze!
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Ndio hali yenyewe mtu anapochemsha hana budi kuambiwa na iwapo hamtaki akosolewe basi nyie hamko tofauti na hao Magamba!
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  May 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Dr. Slaa ametumia mantiki na si ngumu kuelewa; kama Mwenyekiti wa Mtaa amechaguliwa na anaweza kuondolewa na wananchi wake waliomchagua kabla ya muda wake (wakifuata taratibu zilizopo) basi yawezekana kabisa kumuondoa Rais aliyeko madarakani kabla ya muda wake kwa kufuata taratibu zilizopo. Hili haliitaji uanasayansi kulielewa vinginevyo tusingekuwa na vipengele vya impeachment au sheria inayoruhusu mtu akivuliwa uanachama wake anapoteza haki ya kuwa Mbunge au Rais.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  May 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Anfaal, rais anaweza kuondolewa madarakani kabla ya kikomo cha muda wake. Hili haliitaji ugenius wowote kuliona. Kinga ya rais haimzuii kuondolewa na Bunge au kulazimishwa kujiuzulu kabla ya muda wake. Wananchi kwa mfano wakiamua kumshinikiza ajiuzulu Rais atajiuzulu na Makamu wake atachukua nafasi yake. Kama serikali nzima inaonekana imepoteza uhalali wake basi Bunge zima linaweza kujiuzulu na Uchaguzi Mkuu mpya ukaitishwa ndani ya siku 90. Hakuna alichokisema Slaa ambacho ni nje ya uwezekano wa kinadharia au kisheria.

  Rais amefanya ile ile syllogism ambayo niliitumia kwenye ile mada nyingine; kama inawezakana wananchi (ambao ndio asili ya madaraka) kumuondoa kiongozi wao waliyemchagua wao wenyewe kwenye mtaa ina maana inawezekana wananchi wa nchi nzima wanaweza kumuondoa Rais wao. Hivi ndivyo ilivyokuwa Tunisia, Misri, Ukraine au hata nchi nyingine ambapo wananchi walitumia madaraka yao ya kutawala kumuondoa mtu waliyemkasimisha madaraka hayo.
   
Loading...