Boramaisha
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 820
- 18
Wana-JF wapenda mabadiliko ya kweli yenye manufaa kwa nchi yetu hatuna budi kumpongeza kwa dhati kutoka ndani ya nyoyo zetu Dk. Wilbroad Peter Slaa kwa kazi nzuri na kubwa mno aliyoifanya kwa Chama chake CHADEMA, kwa Tanzania yetu na Watanzania wanyonge kwa ujumla.
Awali ya yote, Dr. Slaa amejinyanyua na amekinyanyua chama chake juu kabisa. Dr. Slaa amekuwa tishio na mwiba uliowachoma viongozi wa CCM katika kipindi chote cha Kampeni na upigaji kura. Dr. Slaa aliweza kubadili hali ndani ya CCM na chama hicho kutokuwa na uhakika wa ushindi na hata pale viongozi wa juu wa CCM nyuso zao zilionyesha taharuki walipokuwa wakitumbukiza kura zao kwenye masanduku ya kura. Dr. Slaa amefanikiwa kuondoa kujiamini kupita kiasi kwa viongozi hao wa CCM na wanachama wa chama hicho kwamba ushindi kwao hauwezi wakati wote kuwa wa cheeeee kama ilivyokuwa huko nyuma. Dr. Slaa alipoingia ulingoni kila kitu kilibadilika. Asante Dr. Slaa kwa kuwaamsha viongozi wa CCM na wanachama wao kutoka lindi la usingizi la kudhani kwamba wakishavaa magwanda ya kijani na njano kwenye mikutano ya kampeni basi wataendelea kupata na kuchaguliwa kuwa watawala wa nchi hii daima dumu.
Dr. Slaa amefanya tuelewe kwamba CCM sasa kimefikia ukingoni katika uhalali wa kuiongoza Tanzania yetu. Dr. Slaa ameweza kutuonyesha jinsi CCM kilivyooza na kuharibika kutokana na vitendo vya rushwa iliyokithiri tangu kwenye kura za maoni za chama hicho hadi kipindi chote cha kampeni. Je. CCM wanaweza kututajia ni mgombea gani wa chama hicho ambaye hakutoa chochote kuwashawishi wananchi wamchague? HAKUNA!
Dr. Slaa ametufungua macho, masikio na akili zetu kuelewa kwamba bila kutumia nguvu za ziada za rushwa na mabango kila kona, CCM si lolote kimepoteza mvuto na uhalali wake wa kuongoza wananchi. Wakati wote CCM imekuwa ikipanga mbinu mbalimbali za kujitafutia ushindi kwa nguvu, ushindi usio halali. Tumejionea wenyewe jinsi ambavyo kura za mijini na vijijini zilivyoweza kuwa na tofauti kubwa. Kwa nini? Kwa sababu CCM wametumia umaskini wa wananchi wa mijini na vijijini kama mtaji wao wa kupatia kura. Wamewahonga wananchi t-shirt, kofia, skafu, pombe, sukari, chumvi, kanga, pikipiki, baiskeli, vijisenti viduchu kiasi cha elfu moja ama mbili n.k. ili waweze kupata kura kutoka kwao. Ni aibu kubwa kwa Chama chochote cha siasa kufanya mambo hayo kwa makusudi ya kuwarubuni wananchi ili chama hicho kichaguliwe.
Wana-JF wapenda mabadiliko na wanaoitakia mema Tanzania yetu, hatuna budi kumshukuru sana Dk. Slaaa kwa kuweza kutufumbua macho na kuweza kuyaona maovu yote hayo kwa ukweli, uwazi na mwanga zaidi.
Tumuombe Dk. Slaa asife moyo kabisa kwa kukosa ushindi katika uchaguzi huu. Yeye ni shujaa na tena ni ‘Rais' wa Watanzania wanyonge aliokuwa akijaribu kuwatetea kwa dhati majukwaani akionyesha dhahiri kuwa na uchungu wa dhati kwa Watanzania hao waliopigika. Tumuombe Dk. Slaa asherehekee ushindi wake yeye binafsi na ushindi wa CHADEMA na hata wa vyama vingine vya Upinzani vilivyoweza kupata viti Bungeni na kwenye safu ya Udiwani ambao tunaamini kabisa umetokana na yeye Dk. Slaa na si vinginevyo.
Tumuombe na tumuunge mkono Dk. Slaa aanze sasa kukijenga na kukiimarisha CHADEMA tayari kwa mapambano mapya ya 2015. Twendeni vijijini tumsaidie. Hatuendi huko tukiwa tumebeba mafurushi ya kanga, t-shirt n.k. lakini tunakwenda huko na dhamira ya dhati ya kuwaelimisha wananchi wenzetu kwamba maisha bora kwao yataweza kuja tu pale watakapoelewa nini maana ya utawala bora na haki yao ya msingi ya kuweza kugundua na kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia kuyatafuta hayo maisha bora kwa kutumia raslimali ambazo ni mali ya kila Mtanzania kwa manufaa ya Watanzania wote na si wachache.
Zaidi ya hayo, ushindi wa CCM safari hii na amani na utulivu katika upigaji kura na kusubiri matokeo na kuyakubali vimetokana na kile alichokijenga Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Kinachoshangaza, CCM wamebaki kujisifia wao juu ya hali hiyo na kutaka kurushia lawama kwa vyama vya upinzani kila zinapotokea rabsha ndogo ndogo wakisahau kwamba wananchi wa Tanzania bila kujali vyama vyao ndio wadau wakubwa na wajengaji wa hali hiyo ya amani na utulivu iliyotamalaki kwa miaka mingi hadi kuonekana ni jambo la kawaida. Cha kushangaza zaidi ni kwamba CCM kwenye kampeni zao wameonekana dhahiri kunyanyapaa hata jina la Mwalimu Nyerere! Mgombea gani wa CCM aliyejaribu kuomba kura kwa kutumia jina la Mwalimu Nyerere zaidi ya Dk. Slaa wa CHADEMA?
Tumuombe Mungu ampe Dk. Slaa nguvu na uwezo wa kuendelea kupambana kwa manufaa ya Watanzania. Mungu ampe ujasiri wa kufuata nyayo za Baba wa Taifa.
Dk. Slaa ni Mwanamume! Ameweza kuwanyima usingizi viongozi wa CCM waliodhani kuwa kwao uongozi wa nchi yetu ni haki yao ya kuzaliwa!
HONGERA SANA DK. SLAA, NA MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA!