DK. Slaa Kanisa haliendishi huduma zake kwa staili hiyo!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DK. Slaa Kanisa haliendishi huduma zake kwa staili hiyo!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anold, Mar 21, 2012.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Nimesikia kupitia vyombo mbalimbali vikimnukuu Dk. Slaa jinsi alivyolielekeza kanisa lisikubali kupokea michango ya mafisadi na kudai kuwa fedha hizo ni najisi. Siamini kabisa kuwa Dk Slaa anaweza kusema maneno hayo ukizingatia kuwa yeye alikuwa Padri aliyekuwa anaongoza waumini wengi tu ambao kwa namna moja au nyingine sitaki kuamini kuwa wakati huo aliwahi kukataa sadaka za waovu ambao hata kwa jicho la nyama kwa mtu makini anaweza kuwabaini kwenye hizo nyumba za ibada.

  Mafundisho ya kanisa wakati wote nijuavyo mimi si kuwahukumu waovu bali kuwafundisha kutubu na kuacha uovu wao ili kama kuna namna ambayo walikuwa wanafanya isivyo halali, iwe ni kujipatia fedha, au ujanja wowote watubu ili wawe waumini wazuri. Leo hii Dk. Slaa anapojaribu kufunga mlango wa waovu kufika kanisani kwa namna yeyote kwangu mimi huko ni kupotoka na kuchanganya mambo. Kanisa haliongozwi kwa taratibu za kisiasa na wala haliwezi kuchukulia mambo kama dunia ifanyavyo au kwa matakwa ya kisiasa. Kanisa wakati wote husisitiza msamaha na utakaso, hakuna sehemu nyingine Fisadi,mwizi, jambazi, kibaka pamoja na waovu wengize wanaweza kuhurumiwa na kupata msamaha wa kweli hadi kuwa viumbe vipya nje ya mafundishi ya kiimani.

  Dk Slaa aelewe wazi kuwa hao mafisadi anaowajua kwa majina ni wachache sana, ila kuna idadi kubwa ya waovu wanaopeleka michango yao makanisani huku wakiwa wamejaa uovu, kanisa halina muda kabisa wa kufanya kazi ya kuhukumu mtu maana kazi hiyo ni ya Mungu.

  Nahisi Dk slaa anahofu na nguvu ya hao anaowaita mafisadi endapo watajaribu kugombea nafsi ambayo Dk slaa naye anaimezea mate.Dk Slaa ni mtu makini ambaye naamini anabusara za kutosha kuwasaidia wananchi wa Tanzania, kama anauhakika na ushahidi angewafikisha mahakamani hao mafisadi wote ili sheria za kibinadamu zichukuwe mkondo wake? Sioni mantiki ya kulalamika pembeni kwa kuyashawishi makanisa wakati yeye anauwezo wa kudhihirishia umma uovu uliopo. vinginevyo naona huu ni unafiki tu. Sijawahi kusikia hata siku moja kanisa likihakiki vyanzo vya mapato vya waumini wao na usafi wao, nijuavyomimi kila siku kanisa huhamasisha watu waache dhambi, je Slaa anauhakika hao anaodai ni mafisadi hawajatubu? kwahiyo Dk slaa ni mwanadamu msafi anayeweza kukemea usafi wa watu wengine? Nijuavyo mimi masuala ya Mungu yeye yalimshinda ndiyo maana akavua joho na kujiunga na siasa, ingekuwa ni busara akaachana na kanisa maana hata yeye anamengi ya kuhojiwa juu ya uchamungu wake nafikiri haya mambo ya kiroho
  angekaa tu pembeni.
   
 2. bepari1

  bepari1 Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Nonesense! Hajaongelea kuhusu mtu yeyote kuzuiwa kuingia kanisani alichowasihi viongozi wa dini ni kuwa makini ikibidi kuikataa michango(na hajataja swala la sadaka) inayotolewa na watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi sasa wewe unatuletea pumba gani hapa jf? Kama una chuki na dr.slaa au unamtaka sema tujue la sivyo tutakuchukulia kama m-beya na mnafiki usiyefaa kusikilizwa.
   
 3. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mbona hata yeye ni fisadi halafu anawalipa walinzi wa kanisa fedha za chama?
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Ukimzungumzia slaa kwa sasa mzungumzie kama katibu mkuu wa CHADEMA na sio padre! Alishacha upadre na sasa yupo kwenye siasa hivo m judge kwenye context hiyo.,.kwamba mwizi akiiba anaenda kutubu hiyo labda ni biblia yako uliyooandika mwizi na fisadi anatakiwa aige mfano wa zakayo mtoza ushuru aliyewarudishia aliowadhulumu mara nne ya alichowaibia ndipo akatubu, sasa wewe nenda kakwapue mabilioni uyahifadhi benki halafu ukatubu ukifikiri umesamehewa!!
   
 5. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  kwanza nadhani mleta mada ni eidha mwislam au mkristo asiyesoma biblia vizuri, huo utaratibu wa kukataa sadaka za waovu upo kwa baadhi ya makanisa wala sio sia, kuna huyu muhaya wa heineken beer aliwah kutoa milions zake kuchangia ujenz wa kanisa lutheran pale makongo zikakataliwa, sio kila ki2 ni siasa uliza kwanza.
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Inategemea ni kanisa la namna gani. Na baada ya kupokea wanamsaidiaje huyo fisadi. Kama kwa kujikomba la hasha.
   
 7. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mtoa mada amechanganya mambo, Hakuana mtu asiyejua kuwa kuwa El si msafi ndiyo maana alipata hukumu yake pale bungeni, Ikiwa serekali yako ingekuwa makini haitaji ushaidi toka kwa Dr. then ndiyo ichukuwe hatua huo ni udhaifu mkubwa serekali yote makini ingeshafanya uchunguzi na hizi tuuma ndiyo maana hata EL hawezi kumshitaki Dr. kwani anajua tuhuma zake zina ukweli.

  Kwa msingi huo El hana na Moral Authourity hata ya kusimama kwenye mathabahu sembuse kutoa mchango wake na ingekuwa enzi za yesu angecharazwa viboka kama wale waliyogeuza nyumba ya ibada pango la wanyanganyi.
   
 8. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Nilikuwa Malawi tangu kuanguka kwa Dr Kamuzu Banda hadi wakati wa Dr Muluzi. Wakati wa Dr Muluzi, alijitahidi sana kutoa michango kwa kanisa - kujenga nyumba na fensi. Baadhi ya waumini waliona watumie hiyo njia kufanikisha malengo yao hasa kwa mambo ambayo yalikuwa yamewashinda kukamilisha kwa wakati na kila mara Dr Muluzi akitembelea chuo, shule au jengo fulani la ibada aliahidi na kutoa mihela kadhaa. Maaskofu walianza kushtuka na kuanza kusema wasikubali michango kama hiyo maana in the long run italifanya kanisa kuona huruma na kuistahi serikali pale inaposhindwa kutekeleza wajibu wake. Binafsi sina shida na fedha zinazotolewa na mtu yeyote - after all - hazina alama kuwa hizi ni za wizi na zile si za wizi nk. Hatari inayoweza kujitokeza ni kuandaa mazingira ya ndoa takatifu kati ya taasisi za dini na serikali na kufanya hizo taasisi kulala usingizi wa fofo na wasione tena kama wana mchango wa kuisaidia serikali kuenenda katika njia ya haki. Nadhani tatizo liko hapa - kwamba kwa asili - mtu anayekufadhili unamstahi!
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nonsensical
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Juma, utanisamehe bure, lakini kwa mujibu wa jina lako nalazimika kukutambua kama Muislamu na hivyo, ninakuomba mambo ya wakirsto uwaachie wakirsto wenyewe wayajadiri. si busara kabisa kuyaangilia ama sivyo utabadirisha muelekeo wa uzi sasa hivi. na huo uwezo ninao ukitaka hata sasa.

  Sasa Najielekeza kwenye hoja ya msingi.
  Yesu Kristo ambaye ndie Mmiliki wa Kanisa alituachia maelekezo ya kuwaogopa matajiri na kukaa mbali nao. Kwa msingi huu Kanisa linawajibika kuwafukuzia mbali matajiri ambao nyendo zao haziendani na utamaduni aliolifundisha Yesu.

  Na katika hili namshukuru DR SLAA kwa kulirudisha kanisa kwenye mstari.
   
 11. Rabin

  Rabin Senior Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  MUNGU wangu, binadamu wa Africa ni wagumu sana kuelewa na tukielewa ni wepesi sana kusahau na tunasahau kwa huruma zetu wenyewe, hata ukiua watu wengi kwa makusudi, tutalia kwa wakati huo lakini ukipita muda fulani ukiwa rumande ukisubiri adhabu yako, kuna watakao kuja na hoja za kukuonea huruma na utetezi wa hoja nzito ili mradi uonekane ulichofanya si kosa, na ndiyo yanayotokea kwa EL, bila akina slaa kuumbua uozo wake, watanzania tulio wengi tulikuwa hatujui, lakini tumeanza kumsafisha, hata hao viongozi wa dini walikuwa wakali sana lakini kwa vile bado tuna hulka ileile ya kiafrika, nao wanamsafisha sasa.Kwani hakuna watu wengine wanoweza kuteka fikra za watanzania kwa nafasi za uongozi zaidi ya hawa tulio nao? nani EL? ana nini? TUBADILIKE!!
   
Loading...