Dk. Slaa: CCM kamwe hawatatuweza CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mpango wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwamo mawaziri kuanza ziara mikoani, hauwezi kukisaidia chama hicho kujiimarisha kisiasa wala kuathiri kasi ya Chadema ya kujipanua nchi nzima.
Chama hicho kimesema CCM hawatafanikiwa kwa kuwa zimejitokeza tuhuma nzito ambazo hazijajibiwa na serikali ya CCM kwa Watanzania na hivyo kuwafanya wananchi kukosa imani na serikali ya chama hicho.

Kauli hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kueleza kuwa Sekretarieti mpya ya Chama hicho inatarajia kuongozana na mawaziri kufanya ziara ya kichama mikoani kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo.
Nnauye alisema juzi kuwa katika ziara hiyo ambayo itaanza leo katika mikoa ya Mtwara, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, atakuwa akiambatana na baadhi ya mawaziri kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM tangu mwaka 2010.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, alisema ziara hiyo haiwezi kukisaidia CCM kwa sababu hata mwaka 2007 mawaziri walifanya ziara mikoani kuelezea utekelezaji wa bajeti ya kipindi hicho na bado hawakufanikiwa.

"CCM leo ndiyo wameamka, sisi Chadema kama ni kufanya ziara kila siku tupo mikoani, tunakumbuka mwaka 2007 mawaziri walifanya ziara kama hiyo wakatumia fedha za walipa kodi Shilingi bilioni 2.5 na bado hawakufanikiwa, hawawezi kujibu hoja," alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye wakati akizungumza na NIPASHE jana alikuwa njiani akielekea mkoani Kagera kwa ziara ya kichama, alisema CCM hawawezi kuwa na majibu ya kuwatosheleza Watanzania kutokana na kashfa na tuhuma kadhaa ambazo zimejitokeza kipindi hiki ambazo serikali yake imeshindwa kujibu na hivyo kuzua maswali mengi kutoka kwa wananchi.

Alitolea mfano mwaka 2007 wakati Chadema kilipowataja kwa majina baadhi ya viongozi wa serikali na CCM kwa tuhuma za ufisadi, lakini hadi sasa hawajachukuliwa hatua za kisheria licha ya kuwapo kwa ushahidi wa kutosha ambao ungesaidia kuwatia hatiani.
Dk. Slaa alisema kashfa nyingine za hivi karibuni ambazo bado serikali ya CCM haijazijibu ni utoroshwaji wa meno ya tembo yenye thamani ya Sh. bilioni 2.24 ambayo yalikamatwa na maofisa wa bandari ya Hong Kong.
Aliongeza kuwa kashfa nyingine ambazo Watanzania wanataka majibu ni usafirishaji wa wanyama hai akiwamo twiga kwenda nje ya nchi.

Dk. Slaa alisema CCM lazima itambue kuwa kikatiba kazi ya wapinzani ni kusema na serikaki kazi yake kubwa iwe ni kujibu hoja kwa vitendo kwa kutekeleza mambo yanayokuwa yanalalamikiwa.
"Wapinzani kazi yao ni kusema au kuisema serikali iliyopo madarakani, na serikali kwa upande wake inatakiwa kutekeleza mambo yanayolalamikiwa na nchi inaendelea kusonga mbele, lakini inashangaza unapoona serikali nayo inafanya propaganda za kisiasa, hii ni hatari," alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kama serikali itaendelea kuzungumzia propaganda za kisiasa kwa kujibu kwa maneno wapinzani badala ya kutenda kwa vitendo, nchi itaendelea kurudi nyuma kimaendeleo na wananchi wataendelea kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.
"Watanzania wanataka kujua lini CCM na serikali yake watachukua hatua za dhati kukabiliana na ufisadi, CCM wasifikiri ajenda ya ufisadi itaishia hewani…hapana itakuwa ya kudumu hadi tutakapoona hatua zimechukuliwa dhidi ya wahusika," alisema

Source:Nipashe Jumatano
 
Huyu SLAA mbona kazi yake ni kufuatilia tu CCM? CCM wao wamesema KINANA anafuatana na mawaziri kukagua shughuli za maendeleo, yeye anakuja na hoja kuwa CCM haitawaweza, kwani CCM wanakwenda kwenye kampeni au kukagua miradi ya maendeleo? SLAA aache kumuogopa KINANA na kuanza kuomba msaada wa wananchi kwa propaganda zake.
 
Tunataka utekelezaji wa vitendo, sio kuzunguka na kupiga siasa.
Serikali ya CCM imefilisika kimawazo na viongozi wa chama wamepanic.
Kwa ufupi CCM ni sawa na mbwa anayeenda haja na kula kinyesi chake.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hata Sekretariati ya akina Mukama ilipochaguliwa ilizunguka nchi nzima,lakini hakukuwa na matunda yoyote,hata hii tunategemea itakuwa hivyo hivyo.Wanachotakiwa kufanya sio kuzunguka mikoani,bali ni kufanya yafuatayo;
1.Kupeleka watuhumiwa wote wa EPA na Richmond mahakamani,mahakama ihamue kama kuna kesi za kujibu au la!
2.Kuhakikisha pesa zote zilizoibiwa na kufichwa nje zinarudishwa.
3.Kuacha TAKUKURU na jeshi la polisi kufanya kaze zake bila kuingiliwa
4.Kurusu utawala wa sheria kufanya kazi
5. Kutatua kero mbali mbali za wananchi

Yako mengi,ila haya naona ndo mambo makuu yakufanyiwa kazi,na ndo yatarudisha imani ya wananchi kwa CCM
 
Huyu mzee amechuja hata mtoto hawezi akamsikiliza sasa hivi.Hana jipya zaidi ufisadi ndo single yao ambayo raia wameichoka.Chama cha kidini(CDM) lazima kife mikononi mwake
 
Na kutumia mabilioni ya kodi yetu kusafirisha viongozi wa chama na mawaziri kwa madhumuni ya chama nao ni ufisadi mwingn
 
Hapo kasema Facts zipi mkuu? au ndo wale wale bendera fuata upepo, madam kasema SLAA basi ni facts.

Facts ni kwamba tunataka kuona utekelezaji wa sera zote kwa vitendo, tunataka kuona majibu ya kashfa zinazoikabili serikali ya ccm kwa vitendo(kashfa ya pembe za kinana, kashfa ya mabillion ya uswis ya Jk na wenzake, kashfa ya utoroshaji wa wanyama wa maige na wenzake)
Tunataka kuona maendeleo kwa mtanzania tena kwa vitendo na sio kuja kuadithiwa majukwaani kwa propaganda.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Huyu mzee amechuja hata mtoto hawezi akamsikiliza sasa hivi.Hana jipya zaidi ufisadi ndo single yao ambayo raia wameichoka.Chama cha kidini(CDM) lazima kife mikononi mwake

Wewe ni Taahira hatukushangai kwa huu utaahira ulioandika
 
Huyu mzee amechuja hata mtoto hawezi akamsikiliza sasa hivi.Hana jipya zaidi ufisadi ndo single yao ambayo raia wameichoka.Chama cha kidini(CDM) lazima kife mikononi mwake
Hoja ya ufisadi haiwezi kuwa mpya kwa sababu ccm haijashuhulikia kashfa zote za ufisadi za awali na sasa zinaibuka nyingine.
Kwa iyo wewe unataka kusema tuchekelee mabillion ya uswiss yaliyofichwa na JK na makada wengine wa ccm???
Vipi kuhusu wanyama hai waliotoroshwa tena kwa ndege ya jeshi la taifa lingine?
Vipi kuhusu biashara ya meno ya tembo inayofanywa na Kinana mama salma???
Ufisadi ni tatizo la kudumu tz.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kodi zetu zilifujwa mwaka 2007 kwa ushenzi na leo tena wanaamua kuzifuja,si bora zikanunue ambulance.. mwisho wenu waja.
 
Huyu SLAA mbona kazi yake ni kufuatilia tu CCM? CCM wao wamesema KINANA anafuatana na mawaziri kukagua shughuli za maendeleo, yeye anakuja na hoja kuwa CCM haitawaweza, kwani CCM wanakwenda kwenye kampeni au kukagua miradi ya maendeleo? SLAA aache kumuogopa KINANA na kuanza kuomba msaada wa wananchi kwa propaganda zake.

Kinana kwa Dr Slaa ni sawa na sisimizi,Usijidanganye kumfananisha Kinana na Slaa.
 
Back
Top Bottom