Dk.Slaa bado 'amtesa' Kikwete


Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
bul2.gif
Hali bado tete hadi ndani ya serikali
bul2.gif
CHADEMA washitukia mtego wa mgogoro

HALI ya nchi bado ni tete kutokana na baadhi ya wafuasi wa aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kutoridhishwa na matokeo yaliyompa ushindi Rais Jakaya Kikwete, huku nao wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakionyesha kutoufurahia sana kama mwaka 2005, Raia Mwema limebaini.

Pamoja na kundi kubwa la wabunge wa CHADEMA kumsusia Rais Kikwete, kwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge dakika chache baada ya kuanza kulihutubia Bunge jipya, bado baadhi ya wafuasi wa Dk. Slaa wameonekana kutoridhishwa sana na hatua hiyo, huku uongozi wa juu wa CCM ukionyesha kukerwa na hatua hiyo waliyoitafsiri kama utovu wa nidhamu.


Habari za uchunguzi katika baadhi ya maeneo ya nchi zinaonyesha kwamba wafuasi wa CHADEMA bado wanaamini Dk. Slaa ameshinda, imani ambayo imeelezwa kupenya hadi ndani ya baadhi ya ofisi za serikali waliko wafuasi hao.


Kutokana na hali hiyo, imeelezwa kwamba Kikwete kupitia chama chake na vyombo vyake vya usalama, walijitahidi kuzuia mpango wa wabunge wa CHADEMA kutaka kumsusia hotuba yake bila mafanikio ikiwa ni pamoja na kuwatuma viongozi wastaafu wa serikali ambao bado ni makada wake kusaidia kuwalainisha CHADEMA.


Chanzo cha habari ndani ya CCM kilieleza kwamba, saa chache kabla ya wabunge wa CHADEMA kususia hotuba hiyo ya Rais Kikwete, vigogo kadhaa wastaafu serikalini walitumika kuokoa jahazi kwa kukutana ana kwa ana na viongozi wa chama hicho cha Upinzani kilichopanda chati kwa kasi bila. Hata hiyo, vigogo hao hawakufanikiwa.


Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, mmoja wa vigogo hao ni aliyepata kuwa Waziri Mkuu wakati wa utawala wa Awamu ya Pili ya Ali Hassan Mwinyi pamoja na kigogo mwingine anayeheshimika nchini.


Wazee hao waliaminika kuwa na ushawishi mkubwa kwa baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMA walielezwa kutanguliwa na kiongozi mwingine wa zamani wa CCM ambaye, hata hivyo, imeelezwa kuwa alimvurugia zaidi Kikwete kutokana na kuwa mmoja wa watu wanaohusishwa na kashfa za ufisadi.


Uchunguzi wa gazeti hili kabla na baada ya tukio hilo la wabunge hao la kususa hotuba ya Kikwete, uliohusisha watu walioko karibu na Rais, umebaini kuwa uongozi wa CHADEMA, licha ya kuwaheshimu baadhi ya vigogo hao kwa mchango wao kitaifa, lakini hawakuwa tayari kurudi nyuma kufikisha ujumbe wao kwa njia waliyopanga kama chama na si mtu binafsi.


Gazeti hili limebaini kuwa hali ya mazungumzo kati ya vigogo hao na wengine waliotumwa kwa upande mmoja na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kwa upande mwingine, yalikwenda vizuri ingawa hayakuwa na matokeo yaliyotarajiwa serikalini.


Inaelezwa kuwa wito wa vigogo hao kushindwa kugeuza msimamo wa viongozi wa CHADEMA ni kutokana na msimamo wa chama hicho kutokuwa wa viongozi binafsi bali ni wa chama na hususan wabunge walifikia uamuzi huo kwa kupiga kura.


"Wazee walikwenda kuonana na uongozi wa CHADEMA ili kuokoa jahazi lakini walishindwa kutokana na ukweli kuwa, uamuzi ule haukuwa wa Mbowe au kiongozi mwingine, ulikuwa uamuzi wa pamoja wa viongozi wa chama chao.


"Kama Mbowe au mwingine yeyote angetii wito wa vigogo hao na kusitisha uamuzi wa wabunge, basi angekuwa kwenye hali mbaya zaidi kwa wenzake.


Pengine angeulizwa hao waliokutaka ubadili uamuzi halali wa viongozi wa chama ni wanachama au viongozi wa CHADEMA?" alisema mtu aliyekaribu na viongozi hao wakongwe wa CCM nchini.


Kwa mujibu wa ufafanuzi uliowahi kutolewa na viongozi wa CHADEMA, uamuzi wa chama hicho kutaka wabunge wake wasusie hotuba ya Kikwete umetokana na chama hicho kutotambua matokeo yaliyompa ushindi Kikwete ambaye alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


Kwa sasa CHADEMA ndicho chama kikuu cha Upinzani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kuwa na wabunge wengi zaidi bungeni ikilinganishwa na vyama vingine vya upinzani kwa ujumla wake.


Miongoni mwa majimbo mapya ambayo CHADEMA kimeshinda kwa mara ya kwanza kutoka CCM ni pamoja na Musoma Mjini, mkoani Mara, Bukombe, Maswa Magharibi na Mashariki mkoani Shinyanga, Mbeya Mjini, Ubungo na Kawe jijini Dar es Salaam , Arusha Mjini, Hai na Rombo mkoani Kilimanjaro.


Alhamisi ya Novemba 18 wabunge wa CHADEMA waliandika historia kwa kuondoka bungeni mara Rais Kikwete alipoanza kuhutubia Bunge mjini Dodoma, hatua iliyotafsiriwa kumkera na kumuumiza Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


Wakati hatua hiyo ikiwa imewakera viongozi hao, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alizungumza na wanahabari akisema waliondoka bungeni ili kutilia mkazo msimamo wao wa kutotambua mchakato uliompa Kikwete urais, na kusisitiza mabadiliko ya Katiba na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.


Mbowe, ambaye ndiye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisisitiza kuwa urais wa Kikwete umetokana na mfumo mbovu wa uchaguzi unaoendekeza wizi wa kura, chini ya uratibu wa vyombo vya usalama wa taifa.


Kuhusu kuondoka kwao bungeni, Rais Kikwete akiwa katika hali ya kusononeka mwishoni mwishoni mwa hotuba yake alisema; "Hata wasionichagua hawana serikali nyingine ni hii hii. Watakwenda, watarudi, hawana mwingine wa kumwomba yao yatimie zaidi ya serikali ya CCM ambayo mie ndiye rais wake."


Naye Pinda, wakati anaahirisha Bunge, aliwakejeli wabunge hao akisema: "Hata waliotoka nje wako kwenye runinga wakiangalia, ile ilikuwa geresha tuu… lakini kuna baadhi ya vyama vimeanza kuonyesha mwelekeo usio sahihi. Tuukatae!"


Lakini katika mazungumzo yake na wanahabari siku ya tukio hilo, Mbowe alisema wanatetea mabadiliko ya Katiba na sheria ambayo inawanyima fursa watu wanaopinga matokeo ya kura za urais yanapotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), tofauti na matokeo ya ubunge yanayoweza kulalamikiwa na kupingwa mahakamani.


"Watu wanafikiri kuwa madai haya ni mapya,.... hapana yalianza siku nyingi, hawa wenzetu waligoma kuyafanyia kazi, sasa sisi tunaoonyesha kutokubali matokeo yaliyomuingiza Kikwete madarakani tunaonekana ni watu wa ajabu.


"Tunajua Kikwete amehuzunika kwa sisi kutoka pale ukumbini; tunafurahi kwa sababu ujumbe umemfikia na tuko tayari kuzungumza na wadau mbalimbali wa siasa juu ya ubadilishwaji wa Katiba na uundwaji wa tume huru ya uchaguzi," alisema Mbowe.


Katika mazungumzo hayo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, alisema wabunge wa CHADEMA hawajavunja kifungu chochote cha sheria au Katiba kwa uamuzi wao wa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.


Alisema ibara ya 100 ya Katiba kifungu cha kwanza na cha pili inaeleza haki za mbunge kutoshtakiwa kwa kupinga jambo asilokubali hasa anapofanya hivyo kwa njia zisizovunja sheria.


Alibainisha kuwa utaratibu huo ni wa kawaida kwa nchi zenye kujali demokrasia ambapo upande wa wachache una haki ya kuonyesha kutoridhishwa kwao na utawala uliopo au jambo fulani.


Alisema hata Chama cha Wananchi (CUF) kiliwahi kufanya hivyo kwa kutowatambua marais wa Zanzibar ambapo walianza na Dk. Salmin Amour na baadaye kwa Amani Abeid Karume ambaye walimkataa kwa karibu miaka 10.

Alisema utaratibu huo ni mgeni kwa Tanzania Bara lakini ni njia muafaka kwa upande unaoonekana kuonewa au kutokubaliana na jambo fulani.

Tayari kumekuwa na juhudi za makusudi zinazofanywa kujaribu kuiingiza CHADEMA katika mgogoro, hali ambayo imeelezwa na uongozi wa juu wa chama hicho kwamba mpango huo hautofanikiwa kutokana na chama hicho kuwa na viongozi makini hususan katika ngazi yake ya juu.


"Sisi tunaendesha chama kwa misingi ya demokrasia na utawala bora, na hivyo hakuna ambaye anaweza kupenyeza mgogoro.


Tumechukua baadhi ya hatua kudhibiti baadhi ya mambo yanayoweza kutumika kutugawa, na uongozi wote wa juu uko makini kukabiliana na propaganda za kutugawa," anaeeleza kiongozi mmoja wa CHADEMA ambaye alianza kuhusishwa na matatizo ya ndani ya chama hicho.


Hata hivyo alikataa kutajwa jina ikiwa ni moja ya masharti ya kukabiliana na mbinu za kuwagawa.
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
523
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 523 280
Why no mention of Zittos stand? another propaganda paper!
 
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2008
Messages
13,598
Likes
523
Points
280
Z

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
Joined May 11, 2008
13,598 523 280
Unataka kila article lazima imtaje Zitto ndipo uridhike.
Sio lazima wamtaje, ila wanapaswa kulielezea tukio kama lilivyotokea. Kwa kufanya hivi kunakuwa hakuna tofauti kati ya raia mwema na Uhuru.
 
YeshuaHaMelech

YeshuaHaMelech

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
2,624
Likes
4
Points
0
YeshuaHaMelech

YeshuaHaMelech

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
2,624 4 0
"Sisi tunaendesha chama kwa misingi ya demokrasia na utawala bora, na hivyo hakuna ambaye anaweza kupenyeza mgogoro.

Tumechukua baadhi ya hatua kudhibiti baadhi ya mambo yanayoweza kutumika kutugawa, na uongozi wote wa juu uko makini kukabiliana na propaganda za kutugawa," anaeeleza kiongozi mmoja wa CHADEMA ambaye alianza kuhusishwa na matatizo ya ndani ya chama hicho.

Hata hivyo alikataa kutajwa jina ikiwa ni moja ya masharti ya kukabiliana na mbinu za kuwagawa.
Why no mention of Zittos stand? another propaganda paper!
Think big!
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Why no mention of Zittos stand? another propaganda paper!
Tumechukua baadhi ya hatua kudhibiti baadhi ya mambo yanayoweza kutumika kutugawa, na uongozi wote wa juu uko makini kukabiliana na propaganda za kutugawa," anaeeleza kiongozi mmoja wa CHADEMA ambaye alianza kuhusishwa na matatizo ya ndani ya chama hicho.

ZeMarcopolo
Ukisoma kwa uangalifu sentensi hiyo inamhusu Zitto. Think big.
 
K

Kachest

Senior Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
192
Likes
0
Points
0
K

Kachest

Senior Member
Joined Nov 6, 2010
192 0 0
Acha JK ateseke kwa mawazo sababu bila hivyo hafurahi.

Pia wana JF naomba mwenye kumbukumbu kwa mambo yafuatayo anieleze:

1. Nani anakumbuka scandal ya Makamba na kifo cha aliyekuwa mbunge wa kigoma kaskazini wakati Makamba ni mkuu wa mkoa Kigoma
2. Nani anakumbukumbu zake kwa nini alifukuzwa kazi
3. Nani aliyewahi kumsikia akizungumza hata sentensi moja ya kiingereza
 

Forum statistics

Threads 1,237,750
Members 475,675
Posts 29,299,413