Dk. Slaa awaweka pabaya vigogo wa Sao Hill | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa awaweka pabaya vigogo wa Sao Hill

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SG8, Jun 4, 2011.

 1. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  na Francis Godwin, Iringa  TUHUMA za ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali na mawaziri wa Rais Jakaya Kikwete kumiliki vitalu vya miti katika msitu wa taifa wa Sao Hill wilayani Mufindi mkoani Iringa zilizoibuliwa na viongozi wa kitaifa wa CHADEMA zimechukua sura mpya.
  Jana wanawachama wa chama cha wenye viwanda vya mbao Sao Hill (SAFIA) wamewataka viongozi wa chama hicho kujiuzulu kwa madai kutumiwa na mafisadi kwa ajili ya kutafuna raslimali ya taifa.
  Hatua hiyo imekuja huku zikiwa zimepita siku chache tangu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, kuibua ufisadi mkubwa unaofanywa na baadhi ya mawaziri, wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa serikali katika msitu huo wa Sao Hill wakati wa ziara ya mikutano na maandamano ya chama hicho mikoa ya kusini.
  Baadhi ya wanachama wa Safia wamemthibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa chanzo cha ufisadi katika msitu huo ni viongozi wa chama hicho ambao wamekuwa wakikiendesha chama bila kuwa na katiba kinyume na taratibu za nchi huku viongozi wa wizara wakionyesha kushindwa kufuatilia suala hilo.
  “Tunapenda kuushukuru sana uongozi wa CHADEMA ngazi ya taifa ambao katika ziara yake mikoa ya Nyanda za Juu Kusini waliweza kumulika ufisadi katika msitu wetu huu wa Sao Hill.
  Pamoja na kwamba viongozi wanaodaiwa kujimilikisha vitalu katika msitu huo wakikana madai hayo, wanachama hao waliwapinga wakidai kuwa kauli zao zilikuwa ni njama za Safia kutaka kujiosha kwa kuichafua serikali ya Kikwete.
  Wanachama hao wa Safia pia walidai kuwa pamoja na chama hicho kutokuwa na katiba bado kimeendelea kutekeleza majukumu ya kiserikali kwa kujipa hata yale makubwa zaidi, jambo ambalo ni kinyume na taratibu.
  Hata hivyo walisema katika kikao cha wavunaji miti katika shamba hilo la Sao Hill kilichofanyika Machi 27 mwaka jana wajumbe kwa kauli moja mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu, waliwaagiza viongozi wa Safia kuandaa rasimu ya katiba ya chama hicho ndani ya miezi sita bila mafanikio hadi sasa.
  Suala hilo lilipelekea kuzuka kwa mtafaruku mkubwa ndani ya kikao cha Mei 5 mwaka huu kilichofanyika mjini Mafinga chini ya meneja wa shamba la Sao Hill na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mufindi baada ya wajumbe kutaka uongozi wa Safia kuvunjwa kutokana na kuendesha isivyo chama hicho.
  Kadhalika kikituhumiwa kufanya ubadhilifu wa fedha asilimia mbili 2 kwa kila mvunaji bila fedha hizo kujulikana zilipo .
  Kwa upande wake mwenyekiti wa Safia, Wilam Nyalusi, alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alithibitisha kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wanachama wake huku akidai akitofautiana na wanachama wake kwa kudai kuwa katiba ya chama hicho ipo kwa zaidi ya miaka 10 sasa japo bado haijasajiliwa rasmi.
   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hii nchi inahitaji watu aina ya Dr Slaa,ili tusonge mbele! huwezi kutamani kusikiliza upupu kila kona ni hovyo. Hivi kwa nini viongozi wetu hawachukui hatua au ndo bongolala au uroho, can't wait 2015 general election! Can't wait new constitution nk.
   
 3. kidadari

  kidadari JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2015
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 2,338
  Likes Received: 1,198
  Trophy Points: 280
  kwa bei ya mbao ilivyo hapa town cjui wanapga hela kiasi gan! CCM must go!
   
Loading...