Dk. Slaa atangaza ratiba ya CHADEMA na kusema hagombei urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa atangaza ratiba ya CHADEMA na kusema hagombei urais

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, May 3, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Akitangaza ratiba hiyo Dk Slaa alifafanua kuwa fomu kwa wanachama wanatakaowania nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani zinaanza kutolewa Mei 3 kwenye ofisi za majimbo yaliyopo nchi nzima.

  “Kuanzia Mei 3 hadi 9 Agosti mwaka huu ni kipindi cha wanachama kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi za ubunge, hata hivyo majimbo yamepewa fursa ya kupanga ratiba kwa maeneo husika kwa idhini ya sekretarieti ya kamati kuu ndani ya mipaka ya tarehe iliyotolewa,”alisema.

  Alisema mara baada ya kurudishwa kwa fomu hizo wagombea wa nafasi zote watapigiwa kura za maoni kati ya June Mosi na Agosti Mosi mwaka huu.

  Alifafanua kuwa uteuzi wa awali wa wagombea udiwani utafanywa na kamati tendaji ya Kata kati ya Julai Mosi na wakati uteuzi wa wabunge na wawakilishi utafanywa na kamati tendaji ya Jimbo kati ya Agosti 2 na 9 mwaka huu.

  Tofauti na kipindi kilichopita kazi ya uteuzi wa awali wa wagombea ubunge kupitia viti maalumu itafanywa na Baraza la Wanawake la Chama hicho(Bawacha), Agosti 8 mwaka huu na ambapo halmashauri kuu ya chama hicho itathibitisha majina ya wagombea ubunge wote Agosti 10 mwaka huu.

  Dk. Slaa alisema Baraza Kuu la chama ndilo litakalopendekeza jina la mgombea urais, mgombea mwenza na mgombea urais Zanzibar. Alisema uteuzi wa mgombea urais pamoja na ilani ya chama hicho vitathibitishwa Agosti 12 mwaka huu wakati ratiba ya kuchukua fomu na kurejesha itatolewa na Kamati Kuu itakapokutana tena.

  Wakati huo huo Dk. Willbrod Slaa, amevunja ukimya wa muda mrefu na kusema hatagombea urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba.

  “Mimi sina mpango wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, naelewa wazi kwamba hizi ni mbinu chafu zinazofanywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuweza kuwavunja moyo wapiga kura wangu wa Jimbo la Karatu…nasema wananchi wangu ndio waamuzi,” alisema Dk. Slaa.
   
 2. Ninja

  Ninja JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  Kupoteza pesa kijinga noma. Bora uwe makini na jambo unaloliweza kuliko kucheza karata tatu.

  Kugombea Urais Tanzania 2010 ni sawa na kamari ya karata tatu. Lengo la karata tatu linajulikana, na Dr Slaa anafahamu hilo.
   
 3. B

  Bull JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Uchaguzi Mkuu wa kumchagua Mwenyekiti mpya chadema nilini?? Au Chadema inaongozwa kama Royal familiy?
   
 4. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mbona wanashtukiza hivi?kwanini wasingetoa taarifa mapema?
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  May 8, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Here again.Umeajiriwa na nani?
   
Loading...