Dk Slaa ataka serikali kumkamata Kagoda

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
Na Salim Said


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbroad Slaa amesema vita ya ufisadi nchini, haitafanikiwa kama serikali haitamkamata Kagoda na kumchukulia hatua kali za kisheria.

Kagoda ni kampuni inayotuhumiwa kuhusika na wizi wa fedha uliotokea katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania.

Kauli hiyo ya Dk Slaa, inakuja miaka mitatu baada ya hatua yake ya kutangaza hadharani, orodha ya watu 11 aliodai kuwa ni mafisadi.

Akizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari kwa kutumia njia ya kujibu maswali ya moja kwa moja wiki iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alisema anajivunia mapambano yaliyoendeshwa na serikali yake katika vita dhidi ya ufisadi.

“Katika historia ya serikali za Tanzania naweza kusema kuwa hii ni serikali pekee iliyothubutu katika vita ya rushwa, nina marafiki zangu wengi wapo mahakamani,” alisema Rais Kikwete.

Lakini Dk Slaa anaiona kauli ya Rais Kikwete kuwa ni ngonjera tu ikiwa orodha ya watu 11 waliowataja kuwa ni mafisadi katika mkutano wake uliofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke,mwaka 2006 hawatakamatwa.

“Siwezi kutaja orodha nyengine wakati ile tuliyoitaja miaka mitatu iliyopita haijafanyiwa kazi, kwa maana hawajashughulikiwa wale tuliowataja,” alisema Dk Slaa.

Alisisitiza kuwa yeye binafsi hawezi kuridhika ikiwa Kagoda hajakamatwa na kuchukuliwa hatuwa za kisheria.
Dk Slaa alibeza vita dhidi ya ufisadi kwa upande wa serikali kwamba hakuna chochote kinachofanyika katika kuhakikisha kwamba ufisadi unakoma nchini.
 
mheshimiwa jk ameshasema mafisadi ni wajanja sana
hivyo ni shida kuwakamata.

sasa mpaka hapo dk. slaa bado anategemea kagoda
akamatwe kweli?
 
Ndio maana tunasema kuwa Kama Kagoda hawawezi kukamatwa basi hakuna haja ya ajenda ya ufisadi kusemwa na watu au CCM
 
Slaa kaona bunge limesimama anataka kuwin watu,hayo mambo yameshasemwa toka mwanzo hayawezekani narudia tena hayawezekani akitaka ndio hivyo hasipotaka ndio hivyo.Tutakuwa tunapoteza muda bure kuzungumzia kagoda wakati wenyewe wanakula maini kwa asali mbichi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom