Dk Slaa ataka posho za wabunge zipigwe panga ziongezwe waalimu

wajameni
haya ni mambo ya kisiasa...hakuna kitu kama hicho yaani mtu utafute kura kwa mbinde halafu uende bungeni upate hela kiduchu...bado hata hili mnadanganywa???am sure at any given time 90% ya wanaotaka ubunge ni njaa tu......hakuna cha wapinzani wala watawala........hii yote ni kwa sababu ya mazingira tuliyomo....nina kauzoefu na maisha ya kila siku ya kawaida ya mbunge..lazima awe na ka uwezo flani ili aeleweke kwenye jamii inayomzunguka au iliyompigia debe na kumchagua...automatically unabadilika hata kama unania nzuri kabla.........kaaazi kwelikweli
 
hubutu!
haya ni mambo ya kisiasa...hakuna kitu kama hicho yaani mtu utafute kura kwa mbinde halafu uende bungeni upate hela kiduchu...bado hata hili mnadanganywa???am sure at any given time 90% ya wanaotaka ubunge ni njaa tu......hakuna cha wapinzani wala watawala........hii yote ni kwa sababu ya mazingira tuliyomo....nina kauzoefu na maisha ya kila siku ya kawaida ya mbunge..lazima awe na ka uwezo flani ili aeleweke kwenye jamii inayomzunguka au iliyompigia debe na kumchagua...automatically unabadilika hata kama unania nzuri kabla.........kaaazi kwelikweli
 
Ili mjadala huu uwe mzuri inabidi Dr. Slaa atueleze kama kuna mishahara au posho zingine wanazopata wabunge mbali na zile alizozitaja yeye(tsh 135,000/day).
 
Hivi kuna cheap idea zaidi ya "maisha bora kwa kila mtanzania" au "nguvu mpya, kasi mpya na sijui ari mpya". Magufuli si ndio alikuwa anasimamia hayo. Au hilo leo mnamsukumia muungwana tu?

Litawezekana kama watafuata ushauri aliowaambia wananchi - Wawachague wabunge wa upinzani wawe wengi waweze kupiga kura za kutosha ya kubadilisha posho zao. Unataka aende bungeni akamshawishi nani? hao mafisadi yaliyoshinda ubunge mwaka 2005 kwa kutugaia fulana za epa, na sukari za tangold na khanga za meremeta. hao wanaojua sasa deep green sio as deep as it used to be. 2010 pesa watatoa wapi? Atakayemtolea macho mwenzake atakuwa nani?

Dk Silaha piga nondo kama kawaida mpaka wakuelewe. Unachoongea wengi hawakipati wanaelea tu. Hamna wazo la zamani au jipya hapa. Kama issue inatusumbua hata iwe ya zamani kiasi gani kama bado machungu yake tunayasikia tupige kelele.

Kuonyesha jinsi ambavyo hoja yake ameisimamia na si propaganda za kisiasa za kutupiga changa la macho sisi wadanganyika basi afanye hivi.

Yeye mwenyewe aanze na posho lake japo halitoshi lakini atuonyeshe mfano hai awe anachukuwa posho linalojitosheleza kununua pentrol,kulipia nyumba ya kulala na chakula harafu HUDI linalobaki analigawia masikini.

CHEMBE na CHEMBE mkate huwa anze akipigana na wezake bungeni wakati huo huo anawaonyesha wananchi kwa kulikataa posho hilo ama kulichukuwa na kuliwapa wanalolihitaji.

Ni kweli kwa yeye pekee kuwapa waalimu itakuwa no sense lakini kunavituo vingi sana vya watotot yatima,watoto wa mitaani nafikiri ktk maeneo haya posho lake akiwapatia watu hawa litavisukuma sana vituo hivi.
 
Kama ni wazo la zamani inamaanisha ndo halifai? Mkama, wananchi gani wnapitisha posho ya Wabunge? Labda ni wananchi wa Jimbo lenu na kama ni wao basi nyote ni wajinga! Nijuavyo mimi ni Wabunge wenyewe ndiyo hupigania maslahi yao pale Bungeni wakidai waongezewe posho na mishahara na sisi wananchi wenye akili (labda wewe si mmoja wetu) hupingana na mawazo ya kuwaongezea posho wabunge kwa hiyo ni Wabunge wachache sana (kama Dr Slaa) hupingana na mawazo ya Wabunge wenzao katika suala la posho.

Inawezekana kuwa Dk ametoa cheap idea, lakini haina maana kuwa kwa kuwa ni cheap basi siyo point! Inaweza kuwa cheap idea but strong one. Jambo hilo haliwezi kutokea Bungeni kwa Wabunge ambao wewe unadai alipeleke huko akawatolee macho Wabunge wenzake ambao hawawezi kumuunga si mguu tu bali hata kidole! Ni bora atuletee wapiga kura ambao tunaweza kuwakomalia hao Wabung mwakani kupitia kura zetu.

Mkuu
Naona hukunipata vyema ama kiswahili changu sikukipanga ili kieleweke.Swali langu ni kama mawazo yako ya kwamba nini maana ya Mbunge kwenda ku apili kwa wananchi kuhusu fedha ambazo wao wenyewe ndio wanajipitishia na kujilipa??

Aende huko Bungeni apeleke mswaada akautetee huko ,sasa anapokuja kutuambia sisi wananchi ambao hata mswaada hatuwezi kuufikisha huko ana maana gani kama sio kutafuta ----------.

Sisi wananchi karibu wote tunajuwa wabunge wanajipa fedha nyingi na ndiyo maana tunapiga kelele tukapinga kipindi kile walipotaka kujiongeza fedha zaidi hii ina maana mwananchi yuko aware na tatizo hilo,sasa kazi ya wabunge ni kwenda kupigania mawazo ya wananchi huko bungeni na sio kusababisha BROADCAST STORM kama hii ya SLAA .
 
Dk Slaa alisema suala hilo amekuwa akilipigia kelele kila wakati, lakini kutokana na kuwepo na wabunge wengi wenye ubinafsi, suala hilo limekuwa likipingwa na hivyo kuwataka wananchi kubadilika na kuchagua wabunge wengi wa upinzani, ili kuongeza nguvu bungeni na kusaidia kulinda malislahi ya nchi.
Huu ni unafiki tu... Na utaendelea kuwa unafiki iwapo ataendelea kupita mitaani na Sangara wake akijinadi kwa posho la wabunge. Zaidi nitafurahi iwapo nitamsikia bungeni akilikoromea hili kama anavyofanya kwa issue zingine.
 
Safi sana,Lakini mambo mengi yamekuwa yakisemwa sana na hakuna action yeyote.
 
Back
Top Bottom