Dk Slaa ataka posho za wabunge zipigwe panga ziongezwe waalimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa ataka posho za wabunge zipigwe panga ziongezwe waalimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 18, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  Date::3/18/2009
  Dk Slaa ataka posho za wabunge zipigwe panga ziongezwe waalimu

  Na Mussa Juma, Moshi
  Mwananchi

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk Wilbroad Slaa amesema posho wanazolipwa wabunge wakati wa vikao bungeni ni kubwa , hivyo kupendekeza kuwa kuna haja ya kupunguzwa, ili fedha hizo zisaidie kuongeza mishahara ya watumishi na hasa walimu.

  Akizungumza wakati wa mkutano wa Operesheni Sangara katika kata za Rundugai na BomangÂ’ombe, Dk Slaa alisema wabunge wanalipwa fedha nyingi kwa siku wanapokuwa kwenye vikao vya bunge ambazo alisema zinazidi mishahara ya walimu wengi hapa nchini.

  Takwimu zinaonyesha kuwa walimu wa shule za msingi hupata mshahara wa kuanzia jumla ya Sh166,199 na baada ya makato Sh141,000 wakati walimu wa sekondari ngazi ya diploma huanzia jumla ya Sh203,000 na baada ya makato Sh178,000, wakati walimu wa shahada hupata kuanzia Sh360,000 na baada ya makato Sh270,000.

  Posho za wabunge kila siku wanapokuwa katika vikao vya Bunge kila mmoja anapata Sh135,000 na kwa wiki tatu wanazokaa mjini Dodoma wakati wa vikao vya kawaida hupata jumla ya Sh2,835,000

  Dk Slaa alisema suala hilo amekuwa akilipigia kelele kila wakati, lakini kutokana na kuwepo na wabunge wengi wenye ubinafsi, suala hilo limekuwa likipingwa na hivyo kuwataka wananchi kubadilika na kuchagua wabunge wengi wa upinzani, ili kuongeza nguvu bungeni na kusaidia kulinda malislahi ya nchi.

  Alisema njia pekee ya kuondoa hali hii ni wananchi kuamka na kuchagua viongozi na wabunge wengi wa upinzani ambao watasaidia kutetea maslahi ya wananchi kwa kulinda fedha nyingi zinazopotea na kuwanufaisha watu wachache.

  Akizungumzia kuhusu fedha mbalimbali zinazotolewa na serikali kuu na mifuko mbalimbali ya maendeleo ya jamii, Dk Slaa aliwataka wananchi kujenga tabia ya kuhoji mapato na matumizi ya fedha hizo zinazoletwa katika halmashauri za wilaya na manispaa kwa lengo la kuanzishia miradi ya maendeleo.

  "Mimi kama mwenyekiti kamati ya hesabu za serikali za mitaa, nimebaini kuwa fedha nyingi za serikali haziwafikii walengwa lakini wananchi hamjui na wachache mnaojua hawahoji lolote," alisema Dk Slaa.
   
 2. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Safi sana Dr. Slaa, mimi naamini kabisa wewe ndio unafaa zaidi kuwa Rais wa nchi yetu ya Tanzania mwaka 2010.
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Dr. Slaa nakuunga mikono na miguu kwa hili. Isiishie hapo, hata Mashangingi hatuhitaji, nunueni magari ambayo yanaendana na umaskini wa TZ. Gari la USD 20,000 ni gari la maana kabisa. Hakuna haja ya kununua magari ya USD 100,000.

  Ebu angalia, unaenda kumtembelea mwananchi wa Kanjunjumele ambaye hana nyumba ya maana, hana baiskeli, njaa inamsumbua, hana dawa ya kutibu malaria, mtoto wake kashindwa kulipa ada ya mwaka 50,000 secondary ya kata, unaenda na shangingi la USD 100,000. Kweli sisi tuna akili?
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Dr kama unamaanisha unalolisema mimi nakuunga mkono na unatakiwa ugombee urais wa nchii hii 2010
   
 5. J

  JuniorK Member

  #5
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi hapo nakwenda sambamba na Dr, kwani sula hilo ni la aibu kwa taifa kama letu, hicho kipato cha waheshimiwa cha week tatu hakiendani kabisa na viwango vya mishara ya majority of Tanzanians. Na on top of that bado wana huduma nyingi ambazo ni free. Hii sio right kabisa kwa Watanzania tulio wengi.
   
 6. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa naheshimu sana mawazo yako ila kilichonifurahisha zaidi ni kuona na kujua kwamba kuna umuhimu wa CCM kurudisha pesa kwa namna nyingine kwenye serikali maana ninavyojua wengi wa watakaotoa posho ni wabunge wa CCM kwa idadi yao kubwa. Good Thinking.
   
  Last edited: Mar 19, 2009
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hapana
  hili wazo la zamani na alilianzisha Magufuli miaka kumi na kitu iliyopita.Na kwanini alikomalie kwa wananchi kwani wananchi ndio wanapitisha posho yao?ende huko bungeni akawatolee macho wabunge wenzie.

  Hizi ni cheap idea zakutaka kuaminika kwa watu fulani wakati ukijuwa jambo kama hilo haliwezi tokea.
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hatakama Magufuri ni mjombaako sio hivyo mkulu, is either unaunga mkono hoja au unapinga huyu magufuri mbona mnamtajataja hata mahali asipostahiri??? mnanini nae!
   
 9. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #9
  Mar 19, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna cheap idea zaidi ya "maisha bora kwa kila mtanzania" au "nguvu mpya, kasi mpya na sijui ari mpya". Magufuli si ndio alikuwa anasimamia hayo. Au hilo leo mnamsukumia muungwana tu?

  Litawezekana kama watafuata ushauri aliowaambia wananchi - Wawachague wabunge wa upinzani wawe wengi waweze kupiga kura za kutosha ya kubadilisha posho zao. Unataka aende bungeni akamshawishi nani? hao mafisadi yaliyoshinda ubunge mwaka 2005 kwa kutugaia fulana za epa, na sukari za tangold na khanga za meremeta. hao wanaojua sasa deep green sio as deep as it used to be. 2010 pesa watatoa wapi? Atakayemtolea macho mwenzake atakuwa nani?

  Dk Silaha piga nondo kama kawaida mpaka wakuelewe. Unachoongea wengi hawakipati wanaelea tu. Hamna wazo la zamani au jipya hapa. Kama issue inatusumbua hata iwe ya zamani kiasi gani kama bado machungu yake tunayasikia tupige kelele.
   
 10. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Njia pekee ya kuwezesha kujadiliwa kwa tamko hilo la Slaa na hatimaye kuweza kufanyiwa kazi ni kwa yeye mwenyewe au mbunge mwingine yeyote yule kuwasilisha muswada huo Bungeni na sio kwenye jukwaa la kampeni.

  I admire Dr. Slaa's apparent concern for the plight of our teachers, I wish more lawmakers would adopt a similar stance.
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Namuunga Mkono Slaa 100%!

  Haya ni ya Tz mbunge hupata say 4,000,000 Tshs kwa mwezi!

  Kenya Mbunge hulipwa mara 4 ya Mbge wa Tz yaani 12,000,000- 14,000,000 Tshs au 860,000 Kshs kwa mwezi!

  Hawa jamaa yaani kukaa tu na kupiga domo kuliwa hii pesa? Angalia mwalimu au daktari hulipwa kiasi gani!

  Tz wako wazalendo wachache kama akina Slaa.. sema majarority wamajaa uroho!

  Mtanzania nakuunga mkono ndugu: we make a reality check ya jinsi wanainchi wetu wa kawaida wanaishi!

  Ubinasfi wa wanadamu: hao hao waliopewa dhamana na nafasi ya kuwatetetea maskini- ni hao hao wanaamua kuchukua ile keki ya taifa!
   
  Last edited: Mar 19, 2009
 12. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Dr. Slaa ni kati ya wazalendo wachache walio baki bongo hii wenye uchungu na nchi na ndugu zao watanzania! Kweli haingii akilini wabunge kwa muda wa wiki tatu kupata posho zaidi ya mshahara wa daktari anaye okoa maisha ya wanadamu wenziwe, pengine hata ya kwao kwa zaidi ya myezi sita!!

  Ubinafsi umewazidi wanacho waza ni kubuni mbinu za kuzidi kujilimbikia mali kwa kufungua mifuko ya majimbo, ambayo kimsingi hiyo pesa itakuwa ikiishia matumboni mwao!

  Watanzania hatuna budi kuamuka na kufanya mabadiliko kwa kuoondoa mfumo CCM ulio tufikisha hapa tulipo!, Jukumu letu walau wenye uwezo wa kuchungulia hapa JF ni kuwafikia jumbe hizi ndugu zetu kila kona ya nchi, na kuwasihi pilau na tisheti wachukue, lakini hasira yao iishie kwenye sanduku la kura! Ni SANDUKU HILO PEKEE NDILO LITAKALO TUKOMBOA, KWANI MAMBO YA BUNDUKI HATUYAWEZI!!!
   
 13. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wanakijiji naungana na Dr. Slaa lakini niende mbali zaidi. Demokrasia ni kitu aghali kwa hiyo napendekeza tuwe na serikali ya kijeshi wanakuwepo mawaziri wachache na wakuu wa mikoa basi ndio waamue staili ya Libya. Serikali za mitaa ziundwe pale wenye uwezo wa kuwalipa wapo vinginevyo Mkuu wa mkoa atawale. Hatuna haja ya kuchaguana kila baada ya miaka mitano halafu tuwe na Wabunge karibu 400 ambao wanamtindio wa Ubongo. huwezi ukajilipa posho ya Tshs. 135,000 kwa siku alafu ukaseme kima cha chini ni Tshs. 80,000 kwa mwezi kwa mtu mwenye familia ya watu wanne hii ni zaidi ya mauaji ya kimbari. Tujaribu Dictatorship au hata Ufalme. Kama manabisha kalakabaho. Kukabiliana na hali ngumu tufute semina zote na pesa wapewe wajane!te'...tee teee!
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Kama ni wazo la zamani inamaanisha ndo halifai? Mkama, wananchi gani wnapitisha posho ya Wabunge? Labda ni wananchi wa Jimbo lenu na kama ni wao basi nyote ni wajinga! Nijuavyo mimi ni Wabunge wenyewe ndiyo hupigania maslahi yao pale Bungeni wakidai waongezewe posho na mishahara na sisi wananchi wenye akili (labda wewe si mmoja wetu) hupingana na mawazo ya kuwaongezea posho wabunge kwa hiyo ni Wabunge wachache sana (kama Dr Slaa) hupingana na mawazo ya Wabunge wenzao katika suala la posho.

  Inawezekana kuwa Dk ametoa cheap idea, lakini haina maana kuwa kwa kuwa ni cheap basi siyo point! Inaweza kuwa cheap idea but strong one. Jambo hilo haliwezi kutokea Bungeni kwa Wabunge ambao wewe unadai alipeleke huko akawatolee macho Wabunge wenzake ambao hawawezi kumuunga si mguu tu bali hata kidole! Ni bora atuletee wapiga kura ambao tunaweza kuwakomalia hao Wabung mwakani kupitia kura zetu.
   
 15. P

  Preacher JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa namuunga mkono - ingalau ameweza kulisema - hivi Wabunge wanapangiwa na nani posho, maslahi etc.?? NADHANI UMEFIKA WAKATI WABUNGE WAPEWE JOB DESCRIPTION - maana yake wengine hawajui kabisa - WANADHANI UBUNGE NI KWENDA DODOMA NA KUHUDHURIA VIKAO, KUPOKEA POSHO, NA MAGARI MAKUBWA - hivi mtu unachaguliwa ubunge unakaa term nzima ya 5 years hufiki wala kutembelea eno lako la uchaguzi? Sasa uwakilishi unakuwaje?? wanawakilisha wananchi waliowachagua au wanawakilisha mawazo yao?? SOMETIME I FEEL ITS NOT WORTH HATA KUPIGA KURA - YOU CHOOSE SOMEONE TO REPRESENT YOU BUT THERE IS NO INTERACTION WITH THAT PERSON - NAONA DR. SLAA ASINGEANGALIA POSHO TU BALI HATA UTENDAJI WAO NA KUPUNGUZA MATUMIZI KUPITIA JASHO LA WTZ. MASKINI
   
 16. N

  NTIRU Member

  #16
  Mar 19, 2009
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Magufuli yupi? Yule aliyeshupalia kuuza nyumba za serikali akiwagawia hata ndugu na "washikaji" (wa kike) wake ambao si wafanyakazi wa umma? Aah!! tena siyo "kuuza" bali kugawiana, nyumba yenye thamani ya Shs. 150m/= inauzwa kwa bei ya kutupa ya Shs. 10m/= hadi 30m/=?! Wizi mtupu!!!!

  Dr. Slaa ni Shujaa na mkombozi wa nchi hii. Bila yeye kujitoa mhanga na kueleza orodha ya mafisadi pale Mwembeyanga, nani alijua kampuni ya wizi ya Richmond, EPA, Kagoda, Deep green, Meremeta n.k.? Mbona waliotishia kumpeleka mahakamani hawakwenda na baadhi yao wameburuzwa mahakamani wenyewe? Cheche za Dr. Slaa zimefanya mafisadi ndani ya chama chao cha mafisadi (ccm) waanze kukwaruzana. Si unaona yanayoendelea sasa!!! Tumwombe Mungu azidi kumlinda na kumpa afya njema Dr. Slaa. Matunda ya ujasiri wake yameanza kuonekana.
   
 17. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  [QUOTE=Mtanzania; Kweli sisi tuna akili?[/QUOTE]

  Du mzee hauna hakika kama ninyi mna akili? Napenda tu kukusaidia kama mnatumia magari ya kifahari kiasi hicho na akina mama kibao wana kufa kwa kukosa vifaa vya kujifungulia au wanachangia vitanda, watoto wenu wanashindwa kusoma elimu ya sekondari kwa upingufu wa madarasa, halafu zaidi ya silimia 60 ya bajeti yenu inategemea wahisani BASI ninyi HAMNA AKILI HATA KIDOGO.
  Sina shaka kabisa na dhamira ya DK Slaa ila pia sitaki kuamini kama DK hajui mahala muafaka kulisemea hili. Angepeleka hoja binafsi bungeni hata wabunge wengeikataa angekuwa na base ya madai yake.Kusemea hili kwenye majukwaa ya kisiasa ni kutafuta huruma za wananchi ambazo haziwezi kutatua tatizo hili
   
  Last edited by a moderator: Mar 19, 2009
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ninaamini kuwa kama mapendekezo ya tume ya JK ya kupitia modalities za mishahara kama ingekuwa imefanyiwa kazi kikamilifu, hili lisingezua mjadala kwani moja kati ya mapendekezo ilikwua ni kuhakikisha uwiano wa vipato vya watanzania. Ukiangalia mapato ya Mbunge, kwa kweli ni vigumu kuamini kuwa ni mbunge wa nchi kama Tanzania, ambayo watu wengine (wengi tiu) kipato chao hakifiki dola moja kwa siku
   
 19. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  MkamP,
  Kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe kuwa Dr. Slaa anatafuta cheap popularity, lakini ameongea jambo muhimu linalotakiwa kubadilishwa ASAP.

  Posho za vikao kwa wabunge hazitakiwi ziwepo kabisa maana wanalipwa mishahara ili pamoja na mambo mengine wawe wanashiriki vikao vya Bunge.

  Kama suala ni la mahitaji ya malazi wanapokuwa Bungeni, kwa nini pasiwe na hostel ya Bunge kwa ajili ya wabunge wasiokuwa na makazi Dodoma, wakati inajulikana wazi kuwa siku zote watahitajika kuwepo Dodoma?

  Hili linapaswa lisiishie tu kwenye posho za wabunge bali na zile za mawaziri na wakurugenzi wasiokaa ofisini kwa kutengeneza vitripu kila kukicha.
   
 20. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Dk Slaa kwa hilo tunakuunga mkono. Tunaomba lisiishie huko Wilaya ya Hai bali ifike Dodoma ili kunusuru maisha ya walalahoi.
   
Loading...