Dk Slaa atajwa kugombea urais mwakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa atajwa kugombea urais mwakani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 15, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,285
  Likes Received: 5,639
  Trophy Points: 280
  Dk Slaa atajwa kugombea urais mwakani[​IMG]Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, huenda akwa mgombea urais wa chama hicho uchaguzi mkuu mwakani.[​IMG]Na Mussa Juma, Arusha

  VUGUVUGU la kupata mgombea wa urais mwakani ndani ya Chedema linadaiwa kuanza huku Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa akipendekezwa kuchukua nafasi hiyo.

  Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili zimeeleza kuwa Dk Slaa ametajwa kuwania nafasi hiyo akipambana na kiongozi mmoja wa juu serikalini ambaye ni mwanachama wa Chadema.

  Mchakato wa kutafuta mgombea huyo, umeanza kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuamua kugombea ubunge katika Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro hivyo kukosa sifa kikatiba kugombea urais.
  Â
  Habari zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa Chadema ambaye hakutaka kutajwa gazetini, zinaeleza kuwa suala hilo limekuwa likijadiliwa katika vikao vya juu vya chama bila mwafaka.
  Â
  “Ni kweli kuna viongozi wanamtaka Dk Slaa agombee pia kuna kigogo mmoja ameonyesha nia ya kuja Chadema na kugombea na kuna wanasiasa wengine maarufu hawajatoa uamuzi, lakini mapema mwakani nadhani tutakuwa katika hali nzuri ya kujua nani atagombea,”alisema kiongozi huyo.
  Â
  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, Chadema imekuwa na wakati mgumu kumtangaza Dk Slaa kuwa atagombea urais mwakani hasa kutokana na hofu ya kupoteza Jimbo la Karatu.

  Pia hofu nyingine inatokana na baadhi ya wana CCM kuanza kuonyesha nia ya kuondoka katika chama hicho kujiunga na Chadema, kutokana na mgogoro unaoendelea kukitafuna chama chao.

  Inaelezwa kuwa kutokana na mgawanyiko mkubwa uliopo ndani ya chama hicho, huenda makada maarufu wakaamua kujitoa na kujiunga na upinzani, hali ambayo inaweza kuwafanya wakapata mgombea urais.

  Akihutubia wananchi wa Karatu wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Phillemone Ndesamburo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua mtu ambaye ataletwa badala ya Dk Slaa kwa sababu chama kimeamua kumpa majukumu mengine.

  Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo, akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Titus Lazaro ambaye amekuwa akitajwa
  kutaka kumrithi Dk Slaa.

  Alisema hadi sasa anaamini hakuna mtu wa kumrithi Dk Slaa Karatu hivyo ni
  bora akaachwa aendelee kuwa mbunge wa jimbo hilo.

  Lazaro ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema kuanza kutafuta mrithi wa Dk Slaa sasa kunaweza kulipoteza jimbo hilo ambalo limekuwa likinyemelewa na CCM.

  “Mimi sijafikiria kugombea ubunge kama Dk Slaa akigombea urais kwani najua ugumu wa jimbo hili na mikakati mingi ya CCM kulitaka jimbo la Karatu”alisema Lazaro.

  Hata hivyo,kwa upande wake Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa bado hajaamua kugombea urais mwakani.

  “Mimi huwa sipendi kuzungumza bila ya kufanya utafiti..ni kweli watu wanasema nigombee ila bado sijaamua na jambo hili linahitaji utafiti kwanza,”alisema Dk Slaa.

  Dk Slaa ambaye katika siku za hivi karibuni, amekuwa mmoja wa viongozi wanaoheshimika na wenye msimamo mkali ndani ya chama hicho na bungeni, alisema muda wa kutangaza kugombea urais haujafika na suala la urais ni zito sio la kusema bila kuwa na mikakati.

  Umaarufu wa Chadema katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa ukiongezeka hasa kutokana na kuanzisha Operesheni Sangara nchi nzima ambayo imekifanya chama hicho kupata wafuasi wengi.

  Chadema ilianza kuweka mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 ikimsimamisha kuwania kiti hicho, Freeman Mbowe ambaye pia alisimama mwaka 2005, huku ikiweka rekodi ya chama cha upinzani kutumia helikopta katika mikutano yake ya kampeni. Mkakati wa kumsimamisha Dk Slaa ni kutaka kuongeza idadi ya wabunge baada ya kumtumia Mbowe mara mbili.
   
 2. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Kama ni msomaji mzuri wa nyakati (at least kwa kuangalia upepo uliopo)naamini hawezi tosa mguu wake huko labda kama ana lengo tu la kutengeneza CV!!! I guess we still need this babu kule mjengoni, kwavile ndiko hasa kwa sasa ni viable business site for him and Tanzanians kwa ujumla wao!!
   
Loading...