Dk. Slaa ashindwa kutokea kwenye usuluhishi wa kesi

kim jong ii

Member
Nov 3, 2010
42
1
Dk. Slaa ashindwa kutokea kwenye usuluhishi wa kesi Send to a friend
Tuesday, 16 November 2010 22:21

James Magai

ALIYEKUWA mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi mkuu, Dk Willibrod Slaa jana hakutokea kwenye kikao cha usuluhishi wa kesi inayomkabili ya kumdhalilisha mkazi mmoja wa jijini Dar es salaam kwa kupora mke na kuzini naye.

Aminile Mahimbo, ambaye anadai ni mume halali wa ndoa wa Josephine Mushumbushi anayedaiwa kuchukuliwa na Dk Slaa, amefungua kesi ya madai akitaka alipwe fidia ya Sh1 bilioni kwa tuhuma kwamba katibu huyo wa Chadema aliingilia ndoa yake na kuzini na mkewe huyo.
Kesi hiyo ilikuwa isikilizwe jana mbele ya msuluhishi Zainabu Mruke ambaye ni jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaa.
Hata hivyo Dk. Slaa hakutokea mahakamani hapo wala wakili wake na hakukuwa na taarifa zozote za kutokuwepo kwao.
Katika hatua, pande zote mbili zilitarajiwa kujadiliana juu ya kumaliza suala hilo kukubaliana kulimaliza nje ya mahakama na hivyo kesi kufikia tamati.

Wakili wa mlalamikaji, Abduel Kitururu aliwaleza waandishi wa habari kuwa kitendo cha upande wa mdaiwa kutokufika katika kikao hicho cha usuluhishi bila kutoa taarifa zozote kinatafsiriwa na msuluhishi pamoja na upande wa madai kuwa mdaiwa hayuko tayari au hataki usuluhishi.

Alisema hatua inayofuata ni Jaji Mruke kuandika taarifa yake na kupeleka jalada la kesi hiyo kwa jaji mfawidhi kwa lengo la kuipangia jaji wa kuisikiliza rasmi kesi hiyo.
Wakili Marando alipoulizwa kuhusu kutoonekana kwao kwenye kikao hicho, alisema kuwa alimtuma mwenzake kuhudhuria lakini alishangaa kupata habari kuwa hawakutokea mahakamani na kusema hajui huyo mwenzake alikwama wapi.
Hata hivyo, Marando alisema kuwa pamoja na hayo mteja wake anasema hayuko tayari kulipa pesa hiyo na kwamba kumdai fidia hiyo ni kumnyanyasa kwa kuwa mwanamke hamtaki mlalamiaji.

Wakati pande hizo zilipokutana katika hatua ya kupanga kesi hiyo Oktoba 15 mwaka huu, zilikubaliana kuwa iwapo usuluhishi utashindikana, kesi itaendelea kwa kila upande ukuwaita mahakamani mashahidi wanne.
Katika maelezo yake ya utetezi, Dk Slaa alikiri kuwa na uhusiano na mwanamke huyo, lakini akajitetea kuwa alikuwa hajui kuwa ni mke wa mtu kwa kuwa mwanamke huyo hakuwahi kumwambia kuwa ameolewa.
Dk Slaa alidai kuwa alijua kwa mara ya kwanza kuwa mwanamke huyo ameolewa baada ya kusoma na kusikia taarifa hizo katika vyombo vya habari.

Licha ya kukiri kuwa na uhusiano na mwanamke huyo ambao hata hivyo hakuufafanua kuwa ni wa aina gani, Dk Slaa alikanusha tuhuma za kuzini naye wala kumtambulisha kuwa mke wake.
Lakini katika majibu, Mahimbo alisisitiza kuwa Dk Slaa alifanya uzinzi na mke wake na kwamba alifanya hivyo akiwa anajua kuwa ni mke wa mtu.
Alidai baada ya Dk Slaa kumtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe, habari hizo ziliandikwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini jambo ambalo lilitosha kumjulisha kuwa alikuwa akifanya uzinzi na mke wa mtu, lakini aliendelea kuzini naye.
Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010 ilifunguliwa mahakamani hapo Septemba 7 mwaka huu, siku chache baada ya Dk Slaa kumtambulisha Josephine mara kadhaa kupitia kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa ni mchumba wake.
 
si ilikuwa ni kesi ya kuhamasisha kampeni za uchaguzi? uchaguzi umeisha na kesi imekwisha. dr slaa siyo mwiba kwa serikali wala ccm tena kwa sababu pia hayupo bungeni. kwa maneno mengine ccm wala serikali hawataendeleza hiyo kesi hivyo huyo bwana atafute mambo mengine ya kufanya. wamemtosa, na habari ndiyo hiyo!
 
Source: Gazeti la Mwananchi
 
Sasa ina kitu gani cha maana cha kunifanya niitume kwa friends???

Anyway, usuluhishi hapa unamaanisha nini, Mke arudi kwa Mahimbo au??? ukosefu wa akili na kupenda kutumiwa kama ......kisha unatupwa kwenye dust-bin ni matatizo matupu. We mwanamke anakuambia hakutaki kwani amempata anaemtimizia 'khaaaajaaa' zake we unamng'ang'ania na mausuluhishi na mamahakama??!!!!!!!!!!!!!!!!!

Ah mie nachoka kabisa hapa
 
Bila kuweka taratibu za kidini mbele yetu, Hivi kufanya mapenzi na mke/mume wa mtu ni kuzini? Na je, ni kosa?
Kama ni hivyo huko Bungeni kuna asiye na kosa?

Huyo anayejiita mume naye ktk kipindi chote hicho anazini na nani?
 
Hapa swali kubwa ni je nini maana ya mke??

na je jamaa alikuwa anaishi nae kama mke?

na je alikuwa anatimiza majukumu yake kama mwanaume?

Mimi naamini majibu ya maswali ya mwisho ni hapana maana kama angekuwa anaishi nae kama mke angetambua mapema na asingengoja mpaka uchaguzi uje na pia kama angekuwa anatimiza majukumu yake vema kama mwanamume basi mwanamke asingeenda kutafuta 'dume la shoka' limsaidie kuangusha mbuyu...hahhaaaaa
 
Mbona huyo bwana kabla ya kampeni za uchaguzi hakuwa anamfuatilia huyo mwanamke? Kwa kweli Njama hizo in the open air; they have to find something to distract DR maana wanamwogopa; at least it shows that ni kiboko chao. If the so called Mr. Mahimbo wants to raise issue it has to be with Josephine and not Dr. kwani is Josephine a minor? It looks as if he is taking advantage of a minor, or that Josephine is Mahimbo's property? Watu wengine bwana, hata akili hawana
 
mahimbo kwa ccm sasa hivi ni takataka,na kwasababu walimtumia he's supposed to be vrycareful with his mouth for it will cost his life,akijaribu tu kuropoka ccm watammaliza kimafia 'maitihaiongei' awe mwangalifu wani this guy ni mlevi sana.sijui kama aliliona hili kabla hajakurupukia zoezi lake la kiovu dhidi dr.mimi namhesabia kwani i know him he cant zip up his dirty mouth.
 
kama sijakosea dr.slaa alisema hizo hela walizodai wao ndio watamlipa!

Na usuluhishi uikuwa unaendana na kumlipa fidia jamaa ili yaishe,na dokta wa ukweli anataka waende mahakamani ili akishinda yeye ndo alipwe
Ngoja tuone hili game.
 
Huyo Bwana Mahimbo kama hakuchukua chake mapema kabla ya uchaguzi ndo imekula kwake, He should have understood that he was just a proxy, and therefore he should have taken his gratitude beforehand.

Ananikumbusha ule wimbo wa TOT una ubeti ufuatao:

Yamekuushinda, kelele sasa za ni umesahau

ule msemo usemao ukiona cha nini, wenzio wasema watapata lini

acha sasa wajidai, wajivinjali o o hooo

Kwa hiyo kama Bw. Mahimbo gari limemshinda amwachie doctor aliendeshe. Lakini doctor naye wembe wake mkali, unakata kote kote, mafisadi na wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa ndoa kama akina Mahimbo !!!!
 
kama sijakosea dr.slaa alisema hizo hela walizodai wao ndio watamlipa!

Na usuluhishi uikuwa unaendana na kumlipa fidia jamaa ili yaishe,na dokta wa ukweli anataka waende mahakamani ili akishinda yeye ndo alipwe
Ngoja tuone hili game.

Na ndugu yangu bora usuluhishi ungefanywa na mtu mwingine ambaye kwa vyovyote vile hapatikaniki hapa Tz, kama Dr Slaa amekataa basi naweza sema Dr anaongozwa na mungu wake kwani kesi hiyo kwa huyo mama ninavyomjua kwa pesa haramu Slaaa asingesuruhishwa kwa haki, Dr komaa nao mpaka wakulipe hao mafisadi kwani tayari umeshawabana ktk angle ileile ya mahakamani waliyoitaka wao
 
Hivi kuiba mke wa tu maana yake nini? Yaani mke wa mtu ni "object", inaibiwa, haiwezi kijitetea! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu. Hakuna mtu anaweza kuibiwa. Ni kuondoa utu wa mtu na kumfanya "kitu" (Object)". Mie naona huyo mama hamtaki tena Mahimbo, full stop!
 
Mahimbo hana jipya!
ccm walimpa m50 na gari la kutembelea wakati wa kampeni za uchaguzi ili kumharibia jina Dk.Slaa bahati mbaya ccm wakaona issue imebaunce wakamtupa jamaa. Mahimbo kwakuwa ni mlevi akaanza kutanua na kubadili viwanja hapa mjini, akageuza viwanja vya pombe, movenpik, newafrica n.k sasa kaishiwa hela na gari keshauza na aangalie sana coz waliompa ulaji wanampango wa kumnyamazisha so iz better akaremain mute afanye michakato mingine.
Kwanza kajidharirisha kumfanya mkewe bidhaa kwa ccm!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom