Dk. Slaa apiga kambi kwa Freeman Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa apiga kambi kwa Freeman Mbowe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Sep 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, akimnadi mgombea ubunge katika Jimbo la Hai kupitia chama hicho, Freeman Mbowe, wakati wa mkutano wa kampeni zilizofanyika Bomang'ombe, Hai jana.  Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameweka kambi katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro na siku nzima ya jana alihutubia mikutano katika jimbo hilo tu.
  Akiwa jimboni humo, Dk. Slaa aliweka rekodi kwa kuhutubia mikutano 12 kwa siku moja, akimnadi mgombea ubunge wa jimbo kupitia Chadema, Freeman Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho.
  Dk. Slaa ambaye yupo mkoani Kilimanjaro akiendelea na kampeni zake za urais, alifanikiwa kufanya mikutano hiyo ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuliko iliyotangulia.
  Alipokewa jimboni humo kwa msafara wa pikipiki na magari na jana kwa mara ya kwanza Dk. Slaa alibadilisha gari analotumia kila siku aina ya Toyota Hiace, na kutumia Toyota Land Cruiser VX.
  Katika mikutano ya jana, Dk. Slaa alihutubia kwa dakika chache na kumuachia Mbowe kutumia muda mrefu zaidi.
  Pia Dk. Slaa alimkabidhi Mbowe jukumu ya kuielezea ilani ya Chadema kwa wakazi wa Hai, atakapokuwa akihutubia mikutano ya kampeni zake.
  Dk. Slaa alisema anashangaa kuona taarifa ya serikali ikieleza kuwa wilaya ya Hai ina jumla ya walimu 15 wa shule za msingi, jambo alilosema anaamini kuwa si la kweli.
  “Hii ni taarifa ya serikali iliyotolewa bungeni Julai na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, inaonyesha kuwa wilaya yenu ina walimu wa shule za msingi 15 tu…hivi ni kweli,” alihoji huku akionyesha kitabu cha serikali.
  Alisema takwimu hizo zinaonyesha pia kuwa wilaya ya Hai imetengewa Sh. bilioni 13 za maendeleo, na kwamba kama hazitasimamiwa vizuri, zitaishia mifukoni mwa viongozi wachache.
  Dk. Slaa aliwataka wananchi wa Hai kuwachagua wabunge na madiwani wa Chadema, ili wasimamie vyema fedha zao katika halmashauri hiyo.
  Kwa upande wake, Mbowe alisema ni aibu mikutano ya kampeni za CCM kupambwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya na vikundi vya vichekesho, wakati taifa linakabiliwa na matatizo makubwa kama vile umasikini na huduma mbaya za jamii. Alisema hali ya maisha ya Watanzania wengi inasikitisha kwani hawana uwezo wa kupata milo mitatu kwa siku.
  “Lakini katika hali kama hiyo, mgombea urais kupitia CCM, Rais Jakaya Kikwete, anaambatana na wasanii wa kizazi kipya pamoja na kikundi cha vichekesho cha ze komedi,” alisema.
  Aliongeza: “Hauwezi kuzungumzia matatizo ya taifa kimzahamzaha, tuna mambo mengi kuhusu mustakabali wetu na sio kutazama vichekesho ...huwezi kucheka wakati tupo kwenye msiba wa umasikini, wizi wa rasilimali zetu na huduma mbovu za afya na elimu.”
  Mbowe alisema baadhi ya watendaji wa serikali wamekuwa wakitumia vibaya fedha za wananchi, jambo linalokwamisha maendeleo.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,147
  Likes Received: 1,242
  Trophy Points: 280
  Mbowe anashangaa nini sasa!!!! Kikwete si anaandamana na WASANII wenzake kwneye mikutano yao ya Kisanii.
   
Loading...