Dk. Slaa amvaa Lowassa Monduli

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
572
579
Nauliza waandishi wa magazeti mengine hawajakuwapo katika huu mkutano wa Slaa? Jamani hii inatisha.

Dk. Slaa amvaa Lowassa Monduli


Oktoba 27, 2010 | Mwandishi wa Raia Mwema, Monduli


MGOMBEA urais kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Slaa, amemshambulia Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya kifisadi vilivyotokea jimboni na kwenye Taifa.

Mashambulizi hayo ya Dk. Slaa kwa Lowassa ni mwendelezo wa mengi ambayo amekuwa akiyafanya kwa chama tawala na vigogo wake katika mikutano yake ya kampeni inayoendelea.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika hapa Ijumaa iliyopita katika viwanja vya Bomani, Dk. Slaa alisema hana ugomvi binafsi na Lowassa kwani ni moja wa
viongozi aliofanya nao kazi kwa karibu na ni rafiki yake, lakini wanatofautiana katika masuala ya msingi yanayohusu maslahi ya Taifa.

"Sina ugomvi na Lowassa. Nimefanya naye kazi akiwa Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Arusha na mimi nikiwa Katibu wa Wabunge hao kwa muda mrefu. Ni rafiki yangu, ila tunatofautiana katika masuala mawili ya msingi ambayo ni ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka," alisema Dk. Slaa katika mkutano huo alioutumia pia kumnadi mgombea ubunge wa CHADEMA, Amani Silanga Mollel.

Alieleza kuwa katika Jimbo la Monduli kuna kiasi cha shilingi bilioni 45, fedha za mradi wa maji za mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) lakini ambazo zimetumika vibaya na mradi huo wa maji haukuwa na ufanisi wowote kutokana na fedha kupitia katika nyendo za ufisadi.

"Kiasi cha fedha kilichotumika kutekeleza mradi huo ni kidogo sana na fedha hizo ningepewa mimi ningesambaza maji kwa Mkoa mzima wa Arusha na si Jimbo moja la Monduli…..fedha zilizotumika kwa mradi huo ni kidogo nyingine zimepotelea kusikojulikana," alieleza.

Alisema mradi mwingine ambao ulikuwa na harufu ya ufisadi katika Jimbo hilo la Monduli ni wa ujenzi wa nyumba moja ya mwalimu katika shule moja ya sekondari iliyopo Mto wa Mbu ambako kiasi cha shilingi milioni 70 zilitafunwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo.

Alidai kuwa aligundua uifisadi huo akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa. Alisema Mkurugenzi wa Halmashauri katika maelezo yake alieleza kuwa walitumia milioni 70 kujenga nyumba ya mwalimu mkuu lakini walipofika shuleni hapo walielezwa na uongozi wa shule kuwa nyumba hiyo ilijengwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama msaada wa ujirani mwema na wao walikabidhiwa funguo baada ya nyumba kukamilika.

"Wakati ufisadi ukifanyika katika miradi hiyo Lowassa alikuwa Mbunge wa Jimbo hili na pia allikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania… Kwa hiyo kama kiongozi alishindwa kuzuia ufisadi huo na pia alishindwa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika baada ya kubainika kwake," alisema huku akishangailiwa na umati wa watu waliohudhuria.

Aidha Mgombea huyo alidai kuwa wakati Lowassa akiwa Waziri Mkuu alihusishwa katika kashfa ya kutumia madaraka yake vibaya kwa kushinikiza kutolewa zabuni kwa kampuni ya kufua umeme ya Richmond na baadaye tuhuma hizo zilisababisha ajiuzulu u waziri mkuu.

"Kampuni ya Richmond iliitia hasara Serikali ya Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 122 kutokana na mkataba wake tata. Baadaye yaliyotokea kila Mtanzania ni shahidi. Katika suala hilo Lowassa alitajwa sana," alisema mgombea huyo.

Aliongeza Dk. Slaa: " Ndugu zangu linapokuja suala la matumizi mabaya ya fedha za umma mimi sina urafiki na mtu yeyote lakini pia sina urafiki na kiongozi anayetumia madaraka yake vibaya… kwa hiyo wana Monduli nawaomba msimchague tena Lowassa kwani amewatia aibu watu wa jamii ya Wamasai kutokana kushiriki kwake katika ufisadi wa Richmond na mengineyo."

Mgombea huyo wa CHADEMA alilaani pia kitendo cha kufanyiwa hujuma na mamlaka zinazohusika katika mikutano yake ya kampeni katika jimbo hilo ikiwamo kunyimwa uwanja wa kufanyia mkutano na madai ya kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni makada wa CCM kuwakodishia magari wananchi wa mji wa Monduli na kuwahamishia katika vijiji vya Monduli Juu ili wasihudhurie mkutano wa Dk.Slaa.

"Sisi tunaposema tutatoa elimu bure CCM wanajenga hoja kuwa tutaoa fedha zote hizo wapi? Lakini hata wao wanashindwaje ikiwa wanaweza kuwa na fedha za kuchezea za kukodisha magari kuwahamisha watu ili wasihudhurie mkutano wangu? Ndugu zangu fedha zipo nyingi tu ila CCM hawataki watoto wa masikini wapate elimu," alisema.

Alisema iwapo chama chake kitafanikiwa kuingia madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu, watahakikisha kuwa baadhi ya mali zinazomilikiwa na CCM zikiwamo viwanja vya wazi, majengo na mali nyingine zitataifishwa na kurudishwa serikalini kwani mali hizo zilipatikana kwa jasho la wananchi wote.

Akizungumzia katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alilalamikia kitendo cha Msimamizi wa Uchaguzi kukataa chama chake kutumia uwanja ulioko Soko Kuu la Monduli kwa madai kuwa uwanja huo unamilikiwa na CCM.

"Mkutano wa Monduli umefanyika katika mazingira magumu kutokana na mizengwe kutoka kwa baadhi ya watendaji wa Serikali wanaoshirikiana na CCM na hali hii pia imekuwa ikimkabili mgombea wetu wa ubunge ambaye amekuwa akifanyiwa mambo ya hovyo na watendaji hao," alilalamika Mwigamba.

Akitoa mfano, Mwenyekiti huyo alieleza kuwa saa chache kabla ya kuwasili kwa Dk. Slaa Monduli watu wanaodaiwa kuwa ni makada wa CCM walikodisha magari makubwa ya abiria na yale ya kubebea mizigo kuwahamisha watu kutoka mjini Monduli na kuwapeleka eneo la Monduli Juu lengo likiwa mkutano wa CHADEMA ukose watu.

"Lakini pamoja na njama hizo mkutano wetu kama unavyoona umejaa watu na wamepata fursa ya kumsikiliza Dk.Slaa na ujumbe umefika kwa asilimia 100…na hali hii inapaswa iwe fundisho kwa watu wanaojaribu kuhujumu demorasia ya vyama vingi," alisema.

Akiwa eneo hili la Kaskazini mwa Tanzania wiki iliyopita, Dk.Slaa alifanya kampeni katika majimbo ya Ngorongoro, Mbulu, Karatu, Monduli, Arumeru Mashariki, Rombo, Vunjo na Muheza mkoani Tanga.
 
Inabidi haya mabomu yawekwe sehemu kama mkusanyo, harafu baada ya uchaguzi tuyafuatilie na kuhoji kulikoni serikali ya awamu ya nne? Waandishi wetu wa habari naomba watusaidie kujumlisha tuhuma zote zilizoibuliwa na Dr Slaa na kuzirusha hewani.
 
Swali halijajibiwa, waandishi waliokuwapo Monduli mbona hawajaandika!? wahariri mbona hawajajibu? Hebu tupeni majibu jamani
 
Swali halijajibiwa, waandishi waliokuwapo Monduli mbona hawajaandika!? wahariri mbona hawajajibu? Hebu tupeni majibu jamani

Halisi, Kibanda na wenzako mko wapi?
 
Sasa amekuwa mtamu wanamtaka kwa hali na mali wachaga kwa maslahi watafanya kolote mladi lao litimie.
 
TITI LA MAMA NI TAMU HATA KAMA NI LA.......mulitoka Dom wamoja mukabakia na team CCM...ingefurahisha kama hiyo spirit inge endelezwa...lakini hizi chokochoko zinaweza rudisha zile team nyingi ambazo zilivunjika na kuwa moja tu.
 
Back
Top Bottom