Dk. Slaa amshukia tena Gwajima. Amtaka awaombe radhi Maaskofu na Watanzania...

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Kauli za Dk. Slaa zimekuja baada ya Mchungaji Gwajima kujitokeza kwenye media na kudai hakuwahi kuwa mfuasi wa Lowassa bali ni mfuasi wa mabadiliko ya nchi na siyo mfuasi wa mtu au personality ya mtu.

Ikumbukwe Dk. Slaa aliamua kuwa mkimya katika kipindi ambacho taifa likikuwa katika harakati za kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Dk. Slaa ameyasema haya kupitia akaunti yake rasmi (verified user) ya Jamiiforums.

Dk. Slaa amesema,
Ndiyo maana siku chache zilizopita nilisema:

i) Ni muhimu kwa "Mshenga Gwajima" kutubu na kuwaomba Radhi Watanzania kuliko kuendelea kuwapotosha.
ii) Mungu hamilikiwi na binadamu awaye yote. Watanzania tunawajibu wa kumshukuru sana Mungu kwa kutukomboa na kutuokoa na " Mabadiliko" ya " Kuzungusha Mikono". Mshenga na UKAWA yake walitaka kutuaminisha sote kuwa Mabadiliko ni kuzungusha mikono! Walitaka kutuaminisha kuwa "Mabadiliko ni Lowassa na Lowassa ni Mabadiliko".

Lowassa aligeuzwa kuwa "Ajenda" badala ya ajenda za Msingi za Wananchi. Mungu amesikiliza Sala za Wanyonge na Walalahoi. Namshukuru sana Mungu aliyenionyesha kuwa kati ya wawili hao, japo wote kila mmoja ana uchafu, Magufuli ni "Nafuu mara eflu" kuliko fisadi Lowassa. Asante sana Mungu Mwema kwa kulinusuru Taifa lako lililotaka kuingizwa "mjini" na makuwadi kwa ulaghai na upotoshwaji uliopitiliza.

iii) Nilimtaka Gwajima awaombe radhi Maaskofu aliosema "wamehongwa na Lowassa na kuwa fedha hizo waligawiwa mbele ya Mavho yake. Alisema bila kumumunya maneno, kuwa.... Maaskofu wa ki lutheri alikwisha malizana nao" na kuwa kati ya "Maaskofu wa Kikatoliki 34 wamehongwa Maaskofu 30 na kumtaja kwa jina Askofu Mkuu mmoja, ambaye yeye kapewa fedha za kununulia gari la kiaskofu." Fedha hizo alidai zimetolewa na Lowassa kupitia Rostam Azizi. Gwajima, Tambua kuwa kama ni kweli toka tena hadharani wakemee Maaskofu wanaopokea Rushwa, na kama si kweli Waombe Radhi hadharani Maaskofu hao kwani kauli hiyo ilitaka kuwagawa Maakofu na kuwachafua.

Lakini, alitamka hayo akiona ni sifa, ndiyo maana nilimshangaa kiongozi wa dini ambaye badala ya kukemea anaona ni sifa. Kama wenzangu waliokuwepo na wao wana Misingi ya kusimamia basi watatoa ukweli wao, na kama wanachukia ufisadi basi watatoka hadharani kukemea tamko hilo lililotolewa mbele yetu watu 4 akiwemo Mshenga.

Nilipotamka hivi wengi walidhani Dr. Slaa ndiye Katamka kuwa Maaskofu "Wamehongwa". Kama Askofu anaweza kufika mahali akawasingizia wenzake ni hatari sana na halihitsji kufungiwa Macho na masikio. Kama anavyosema Gwajima ni " kweli". Basi wote tunaopenda kupiga vita Ufisadi ni lazima tupaze sauti zetu, na kukemea kitendo hicho kama kweli kimefanywa na wale tunaotegemea kusimamia maadili katika Jamii yetu. Wako walioniambia Dr. Slaa unapata wapi ujasiri wa kuwasema viongozi wa dini. Sijawahi kuyumba wala kuyumbishwa. Ukweli utatamkwa hata kama ni mchungu, na uovu na uozo utasemwa tu hata kama umetendwa na nani. Ukitazama nyuso za wazi " haki haitatendeka milele.

iv) Katika busara ya kawaida, hatukutegemea Gwajima kujitokeza "Kumkana Lowassa" hasa kabla ya kuomba radhi. Aidha Kauli " Live" kwenye YouTube na mitandao mbalimbali ziko bado kibao. Ama kweli Gwajima ni kiongozi asiye na dhamira kukanusha kauli zake hizo kabla ya kuomba radhi.

v) Wako watakaodhani kuwa Dr Slaa ana "bifu" binafsi na Gwajima. Ni kweli kibinadamu nimeumia sana kwa kuwa kuumizwa na rafiki kunaumiza sana, lakini nawaonea huruma zaidi Watanzania Waliobebwa kwa ushabiki mkubwa na kupoteza nguvu zao nyingi na labda "kupoteza fursa ya kuiondoa CCM kwa muda mrefu ujao" kwa kuwaamini watu kama kina Gwajima. Hiki ndicho kinachonisukuma zaidi kuendelea kumkaba Gwajima hadi atakapoomba radhi kwa watanzania wanyofu.

Nawaomba Watanzania tuwe na kumbukumbu. Tuzisikilize tena Kauli mbalimbali alizozitoa Gwajima, tena wakati mwingine kwa njia ya Maombi kwa jina la Mungu. Hali hii isipokemewa kwa ukali sana ni hatari sana.

Ndugu zangu wanaJF na Watanzania wote,
Pamoja na yote haya, ninawatakia Heri nyingi kwa sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2016 uwe wa Baraka na mafanikio.

Baadhi ya wanaJF wakataka kufahamu zaidi kuhusu kauli yake. Mmojawapo alimuuliza swali hili,
Samahani Dokta kabla hujaondoka, hivi ni kweli Dokta ulianzisha motion ya kumleta Lowassa Chadema? Na kama ni kweli, nini hasa yalikuwa malengo yako? ni hayo tu kiongozi wangu.
Dk. Slaa alijibu na kusema,
Kamanda,

Naona hujalala saa hizi! Msimamo wangu ulikuwa wazi. Mshenga alikuja kwangu kunijulisha yaliyotokea Dodoma na kunitaka tuone namna ya kumpokea. Nikampeleka kwa Mwenyekiti wa Chama. Hiyo ndiyo "Mimi kuanzisha mchakato". Nimeeleza mara kadhaa lakini naona watu wameshindwa kupambanua.

Nilieleza kuwa nilishiriki majadiliano ya Kumpokea Lowassa. Tofauti ya mimi na wenzangu ni kuwa niliweka Masharti kama Katibu Mkuu ili kukilinda Chama changu. Moja ya Sharti ni kutaka kujua kama Lowassa ni "Asset au ni Liability". Hadi tarehe 27/8 hoja hizo zikawa hazijajibiwa na nikaona wenzangu tayari wamefikia uamuzi wa kumpokea bila kuangalia athari kwa CHADEMA.

Kama mwanademokrasia, Wengi wakifikia uamuzi wewe ambaye hukubaliani nao ndio unakaa pembeni. That is what I did Kamanda.

Motion kama unavyoita wewe ilianzishwa na Mshenga siyo na mimi. Japo taarifa ninazopata sasa ni kuwa move hiyo ilikuwepo mapema hata kabla mshenga hajanifikishia. Inasemekana kuja kwangu ilikuwa changa la macho tu kwa lugha ya siku hizi. Taarifa nyingi ndiyo zinaanza kupatikana sasa, nisingelipenda kuzizungumzia kabla sijazichambua vizuri.

CHANZO: Mjadala huu => https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ga-kuwahi-kuunga-mkono-mwanasiasa-yeyote.html
 
asubuhi ya tarehe 27 Dec 2015 naona inakucha vizuri.namshukuru mungu kwa kuamka salama.
 
Dah Dr. hajasikika siku nyingi tulishaanza kumsahau...ameibuka kipindi muhimu wakati zimebaki nafasi NNE za wabunge wa kuteuliwa na katibu mkuu wa CDM bado hajapatikana. Ila nimkumbushe tu katika uchaguzi wowote minyukano ni ya kawaida bahati mbaya ndani ya chama chako ukaibuka mshindwa, uchaguzi ulishaisha, na siasa za uchaguzi ziliisha. Sasa tunajenga nchi chini ya Rais Magufuli. Malumbano na kusutana tena havina nafasi sasa kazi tu.
 
Tunafunga mwaka kwa mastori moto moto kama tulivyoufungua mwaka 2015 kwa viapo na mbija.

Merry christmas and prosperous 2016 to you and your families.

Best regards
 
asubuhi ya tarehe 27 Dec 2015 naona inakucha vizuri.namshukuru mungu kwa kuamka salama.
Mshukuru Mungu pia kwa kuwafunulia waanzilishi wa Jamiiforums kwa sababu wamekuwezesha kupata habari motomoto kupitia Jamiiforums pindi unapoamka asubuhi!
 
Dah Dr. hajasikika siku nyingi tulishaanza kumsahau...ameibuka kipindi muhimu wakati zimebaki nafasi NNE za wabunge wa kuteuliwa na katibu mkuu wa CDM bado hajapatikana. Ila nimkumbushe tu katika uchaguzi wowote minyukano ni ya kawaida bahati mbaya ndani ya chama chako ukaibuka mshindwa, uchaguzi ulishaisha, na siasa za uchaguzi ziliisha. Sasa tunajenga nchi chini ya Rais Magufuli. Malumbano na kusutana tena havina nafasi sasa kazi tu.

Duh Watu wengine cjui mnajickia tu kuongea au ndo mnasema ni akl ya asbh huwezi fkr sana na ka n hvyo bc uwe una subr sa nne ukoment mana opi zngne ni na wacwac na elimu zenu kabisa, huwezi ukashindwa kuchambua kauli ya dokta ht ka huna akili na haya yote yamewekwa waz kwa kupitia gwajima na magufuli coz jinc alivyoongea ndvyo jinc yalivyotokea, zaidi amani iwe nanyi
 
Dah Dr. hajasikika siku nyingi tulishaanza kumsahau...ameibuka kipindi muhimu wakati zimebaki nafasi NNE za wabunge wa kuteuliwa na katibu mkuu wa CDM bado hajapatikana. Ila nimkumbushe tu katika uchaguzi wowote minyukano ni ya kawaida bahati mbaya ndani ya chama chako ukaibuka mshindwa, uchaguzi ulishaisha, na siasa za uchaguzi ziliisha. Sasa tunajenga nchi chini ya Rais Magufuli. Malumbano na kusutana tena havina nafasi sasa kazi tu.

CHADEMA is dying my dear,mwambie Mbowe aende popote pale nchini kufanya mkutano wa hadhara,kama atapata hata watu 100 nitakupa shilingi 100,000,uchaguzi mkuu ujao utakuwa mgumu zaidi kwa CHADEMA, mna hatari ya kupoteza wabunge zaidi.
 
Tunafunga mwaka kwa mastori moto moto kama tulivyoufungua mwaka 2015 kwa viapo na mbija.

Merry christmas and prosperous 2016 to you and your families.

Best regards
This is Jamiiforums where people dare to give mastori and habari motomoto!
 
asante dr. slaa kwa kuweka mambo sawa. kuna upotoshaji mkubwa kuhusu ujio wa el cdm. unasingiziwa mengi na viongozi wahuni wachache ndani ya cdm. makamanda wengi wamesombwa na unafiki wao. kwa kukupoteza, cdm imepata hasara kubwa. andika kitabu kuhusu maisha yako ya kisiasa maadam umestaafu siasa. utarudi lini?
 
Dr Slaa hatupendi watu walio ughaibuni wanaojifanya wanaipenda sana Tanzania. Rudi home au vipi kaa kimya. By the way gazeti la Mawio laililopita limekutuhumu kuhujumu upinzani mapeeema hata kabla Gwajima hajaanza mbwembwe zake. Jibu hoja za Mawio ili tu balance mawazo yetu, vinginevyo na wewe ni msaliti na huna moral authority ya kumshambulia Gwajima.
 
Dr.naye mnafiki kwanini Gwajima alipoenda kwake kumpelekea habari za Lowasa asingemkatalia pale pale ilikuwaje hadi akampeleka hadi kwa kina Mbowe,ni kama mtu x ambaye ni mlevi anampeleka mtu y ambaye si mlevi kwenye klabu cha pombe halafu huyu y akianza kunywa pombe anamlaumu.

Dr.Slaa ulijua lowasa fisadi na chama chako kilimtaja mara elfu kuwa fisadi na wewe ulimtangaza mwembe yanga kuwa fisadi kwanini habari za yeye kuhamia chadema ulizipeleka kwa kina Mbowe?kwanini usingemkatalia mshenga pale pale ulipoletewa habari zake?
 
Kwanini kila akiongea Gwajima,Dr.slaa naye hujitokeza ku-comment hapa JF,Kwanini asijitokeza japo kuongelea swala uchaguzi kule Zanzibar,au Ajitokeze kutoa ushauri katika hiki kinachoendelea hapa nchini kama bomoabomoa inayowacha watu katika hali ngumu ya maisha..Yeye adui yake ni Gwajima tu..Aanze na yeye kuongea tuone kama Gwajima naye atakuja kumjibu.
 
Kwanini kila akiongea Gwajima,Dr.slaa naye hujitokeza ku-comment hapa JF,Kwanini asijitokeza japo kuongelea swala uchaguzi kule Zanzibar,au Ajitokeze kutoa ushauri katika hiki kinachoendelea hapa nchini kama bomoabomoa inayowacha watu katika hali ngumu ya maisha..Yeye adui yake ni Gwajima tu..Aanze na yeye kuongea tuone kama Gwajima naye atakuja kumjibu.

Siku zote unapovunja sheria uwe tayari kukumbana na athari zozote zitakazo jitokeza mbeleni. Huwezi kufanya ujambazi wa kutumia silaha...halafu ukamatwe na uhukumiwe miaka 30 jela uanze kusema..."Mahakama imenionea"...Watu wote waliovamia maeneo ya wazi au maeneo hatarishi kwa mujibu wa sheria yetu ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 hawawezi kuachwa salama...ni kubomoa tu nyumba zao. Sasa kama wewe na watu wa aina yako mmeamua kutetea wavunja sheria...basi bakini na upumbavu na ulofa wenu. Ila Watanzania wengi wanaunga mkono juhudi zinazo endelea za kurudisha utawala wa sheria.
 
Katika watu ambao sijawahi kujua kama kweli mungu husikia maombi yao ni pamoja na gwajima hajitambui kabisa.

Mungu kama ni ccm kama unavyoonekana kuamini ni sawa maombi ya Gwajima hayatasikilizwa ila kama ni Mungu wa Mbinguni haachi kumsikiliza awaye yoyote.Tatizo mnahis Mungu ni kama ccm acheni kumfhihaki ghadhabu yake ni kubwa.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom