Dk. Slaa ampa somo Mangula, Nyimbo naye adai Mangula anashindana na kivuli

pefla

Senior Member
Jan 31, 2012
105
74
SIKU chache baada ya Makamu Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Philip Mangula, kujibu mapigo ya wapinzani wake akisema wanaombeza wanasahau historia yake, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, amemtaka aweke mikakati hiyo katika vitendo.

Dk. Slaa alidai kuwa kwa sasa Watanzania wamechoka kusikiliza historia, hivyo kama Mangula ana uthubutu aanze kusafisha chama chake kwa kuwaondoa watuhumiwa magwiji wa ufisadi kabla ya kuhangaika na wale waliotoa rushwa kwenye uchaguzi wao. Wakati Dk. Slaa akitoa somo hilo kwa Mangula, naye mwanasiasa mkongwe nchini, Thomas Nyimbo, amemvaa kigogo huyo wa CCM akisema kuwa ni kama anashindana na kivuli chake kwa kujidanganya kuwa ataitokomeza rushwa ndani ya chama hicho.

Kauli hizo zinakuja siku chache baada ya Mangula kakaririwa na vyombo vya habari akitamba kuwa wanaombeza kuwa hawezi kuitokomeza rushwa CCM wanasahau rekodi yake akiwa Katibu Mkuu wa chama hicho. Mangula bila kumung'unya maneno aliwataja wafanyabiashara Yusuf Manji na Thomas Nyimbo kuwa ni miongoni mwa watu aliowafutia ushindi wasigombee ubunge baada ya kubainika kujihusisha na rushwa katika kura za maoni mwaka 2000.

Mwanasiasa huyo pia alikumbushia jinsi chama kilivyofuta matokeo ya baadhi ya washindi katika majibo 32 na kuamuru uchaguzi urudiwe baada ya kubaini uwepo wa mizengwe ya rushwa, hivyo akaahidi kuwa wanaombeza wangoje waone ndani ya miezi sita atakavyochukua hatua. Hata hivyo, katika mahojiano yake na gazeti hili jana, Dk. Slaa aliendelea kumbeza Mangula akisema kama anajisifu kuwa anaweza kuondoa wala rushwa katika CCM, basi aanze na watuhimiwa sugu walioshindikana kung'oka kwenye falsafa ya kujivua gamba.

Alisisitiza kuwa anamshangaa Mangula kwa kujisifu kwa jambo hilo, na kwamba kama kweli anaweza basi atekeleze sera ya kujivua magamba iliyomshinda mtangulizi wake Pius Msekwa na Wilson Mukama. Alisema kuwa watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho ambao wametajwa hadi na wana-CCM wenyewe bado wapo na wanaendelea vema na kazi za kila siku. "Hivyo kama Mangula ana ubavu aanze na hawa aache kujisifia historia, mambo anayoyataja kwanza Watanzania wengi hawayajui, wanataka kuona sasa," alisema.

Nyimbo ajibu mapigo

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Nyimbo alisema kitendo cha Mangula kumzungumzia mtu binafsi katika tatizo linalohitaji marekebisho ya mfumo mzima ni suala la kushangaza na kuonyesha kushindwa mapema. "Mangula amepewa nafasi, sasa kama atasema hawezi kutokomeza rushwa japo suala hilo ni la kihistoria unafikiri wanachama wake watamuelewa, si watamshangaa?" alihoji.

Nyimbo aliongeza kuwa historia ya rushwa ilikuwepo hata kwa manabii na kueleza kwamba kinachoweza kufanyika ni kupunguza tatizo kwa kuhakikisha wananchi hawaathiriwi kwa kiasi kikubwa. Kuhusu kuenguliwa kugombea ubunge ndani ya CCM kwa tuhuma za rushwa, kada huyo ambaye aliwahi kuhamia CHADEMA na kujitoa hivi karibuni na kubakia mwanasiasa huru, Mangula alimtaka Mangula kuwa mkweli juu ya hilo.

"Nyimbo ni mwanasiasa mwenye historia yenye kutukuka katika Tanzania huwezi ukanikuta katika kashfa yoyote; sasa huyo ndugu yangu anaposema aliniengua wakati huo alikuwa kiongozi wa wapi?"
 
Mangula anataka alete zile siasa zake za 1995 Leo hii tena!!!!!! Halafu anataka ajilinganishe na Dr wa ukweli mwenye phd labda aendelee kushindana na Dr wa kuforge Sultani Kikwete
 
Haka kakikongwe Mangula kanaropoka utafikiri kana hadithia hadithi wajukuu zake huku wakikoka moto. mdomo wake umeshachakaa kwa kula tumbaku. Na uhakika hata ofisini AC hakiwezi kuvumilia tena katakuwa kanataka kawashiwe moto kaote
 
Mangula hawezi kubadilisha lolote ndani ya CCM! Angekuwa anaweza angeanza na Kinana aliyehusishwa na Ujangili.
 
Siasa za Tanzania bana.

Hakuna ajenda zingine zaidi ya rushwa na ufisadi. Hivi vyama (CCM na CHADEMA) Kila siku nyimbo ni zilezile.

Wananchi wanahitaji zaidi ya hizo nyimbo ambazo mpaka zinachosha kuzisikiliza. Please, Come out of this antique shell. We deserve more..
 
Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Nyimbo alisema kitendo cha Mangula kumzungumzia mtu binafsi katika tatizo linalohitaji marekebisho ya mfumo mzima ni suala la kushangaza na kuonyesha kushindwa mapema. "Mangula amepewa nafasi, sasa kama atasema hawezi kutokomeza rushwa japo suala hilo ni la kihistoria unafikiri wanachama wake watamuelewa, si watamshangaa?" alihoji.

Hii kauli ya Nyimo ina ukweli 100%!
 
Siasa za Tanzania bana.

Hakuna ajenda zingine zaidi ya rushwa na ufisadi. Hivi vyama (CCM na CHADEMA) Kila siku nyimbo ni zilezile.

Wananchi wanahitaji zaidi ya hizo nyimbo ambazo mpaka zinachosha kuzisikiliza. Please, Come out of this antique shell. We deserve more..
Ukimpiga mtu ngumi tano sehemu ile ile na akaonekana inampa maumivu makali, utabadili sehemu ya kumpiga? Ndivyo ilivyo sasa, kama CDM wanaona ufisadi na rushwa ndo hoja isiyosafishika kirahisi ndani ya wapinzani wao, waendelee kukumbushia huku wakijipanga kimkakati zaidi.
 
unataka ufisadi usizungumziwe ili uzudi kuiba au?pamoja na kupigiwa kelele bado mnaiba ,chek bil.86 za tanesco.je wakikaa kimya! una maslahi na mafisadi wewe,si bure.
 
Wewe ni mmojawapo wa mafisadi Kama si mtoto wao
 
Mkuu,

Hapa ndiyo umeniacha wazi. Miaka 20 bado hawajajipanga kimkakati?. Miaka kama miwili na nusu hivi, nchi itaingia kwenye general election. That's scary

Je, kama huyo mpinzani wako aki recover na huku huna mkakati mwingine si ni hatari kwako.
 
Ufisadi... ufisadi mpaka kieleweke. Viongozi wanaibua miradi si kwa maslahi ya taifa bali kwa maslahi ya wachache! Kuendelea kupiga kelele ruksa. Hata kama maslahi kwa taifa yapo bado kunawekwa vipengele vya kuwanufaisha viongozi waliopo madarakani. Big up Dr Slaa!
 
pefla Ogopa sana Mwanasiasa ambaye kazi yake ni kutumia muda mwingi kuongelea mambo ya chama kisichochake kama SLAA. Sidhani kama hiyo ni njia sahihi ya kumdhoofisha adui.
 
Last edited by a moderator:
Ufisadi... ufisadi mpaka kieleweke. Viongozi wanaibua miradi si kwa maslahi ya taifa bali kwa maslahi ya wachache! Kuendelea kupiga kelele ruksa. Hata kama maslahi kwa taifa yapo bado kunawekwa vipengele vya kuwanufaisha viongozi waliopo madarakani. Big up Dr Slaa!

Hakika huku ni kupga kelele.
 
Siasa za Tanzania bana.

Hakuna ajenda zingine zaidi ya rushwa na ufisadi. Hivi vyama (CCM na CHADEMA) Kila siku nyimbo ni zilezile.

Wananchi wanahitaji zaidi ya hizo nyimbo ambazo mpaka zinachosha kuzisikiliza. Please, Come out of this antique shell. We deserve more..

Unajua haya mambo si riwaya bali ni halisi. Huwezi kwenda mbele wakati hayajatatulika ndiyo maana bado yanaendelea kuwepo. Serikali ya ccm itatue haya mambo ili tusonge mbele. Hakuna sababu ya kuyafunika wakati yananuka na yanazidi kututafuna bila kutatulika just because we want to move forward!. What for?
 
Mkuu,

Hapa ndiyo umeniacha wazi. Miaka 20 bado hawajajipanga kimkakati?. Miaka kama miwili na nusu hivi, nchi itaingia kwenye general election. That's scary

Je, kama huyo mpinzani wako aki recover na huku huna mkakati mwingine si ni hatari kwako.

Siku zote Wana wa si-hasa ni watu wa kijipanga tu, hawawezi kuwa na jipya, wanasubiri 2015 waimbe wimbo wa tumeibiwa, tumeobiwa, tumeibiwa wakati muda mwingi wanautumia kulumbana na Madiwani wao eti kisa wanashirikiana na CCM kuwaletea wananchi maendele, muda mwingi wanautumia kuongelea uchaguzi wa CCM wakati ndani kwa kunafukuta na mengine mengi yasiyo na tija kwa msatakabali wa Chama chao
 
unataka ufisadi usizungumziwe ili uzudi kuiba au?pamoja na kupigiwa kelele bado mnaiba ,chek bil.86 za tanesco.je wakikaa kimya! una maslahi na mafisadi wewe,si bure.

What's the point?. Kama wanazungumza na bado huo ufisadi unaongezeka maana yake mazungumzo yao hayabadilishi kitu zaidi ya kuchochea. They have failed. Kama wangekuwa makini wangeliona hilo na kubadilisha political strategy Kwa sababu wananchi siyo wajinga kiasi hicho ambapo kila siku wanaimbiwa wimbo huo huo.

We need more than merely rushwa and ufisadi song otherwise, they are doomed

Halafu siyo kila mtu anakuwa fisadi pale anapo question hizi kelele ambazo hazileti manufaa yoyote
 
Wewe ni mmojawapo wa mafisadi Kama si mtoto wao

Kwa sababu tu ya kutaka wanasiasa kubadilika kwa ajili maslahi ya watanzania na siyo kujitafutia umaarufu ndo umwite fisadi? acha hizo mkuu, hawa jamaa wamezidi kujitafutia umaarufu badala ya kujali matatizo ya wananchi.
 
Hii kauli ya Nyimo ina ukweli 100%!
CDM bwana. akitokea mwana-CCM machachari wanasema anapambana na mfumo, akipambana na mtu lugha hubadilika na kusema si hilo, nini tafsiri ya wanasiasa uchwara kama akina Nyimbo?
 
Mangula anataka alete zile siasa zake za 1995 Leo hii tena!!!!!! Halafu anataka ajilinganishe na Dr wa ukweli mwenye phd labda aendelee kushindana na Dr wa kuforge Sultani Kikwete

Hi kwa nini MANGULA ni subject wa CHADEMA hivi sasa? CDM Kazi mnayo, kutapatapa huku siyo kwa kawada lazima kuna kitu.
 
Back
Top Bottom