Dk. Slaa amlipua Lukuvi; Awarushia pia kombora Chami, Simbachawene | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa amlipua Lukuvi; Awarushia pia kombora Chami, Simbachawene

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 19, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  na Edward Kinabo, Mufindi  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataja vigogo na watendaji wa serikali wakiwamo mawaziri wawili na wabunge akiwatuhumu kufanya ufisadi wa kujigawia vitalu vya uvunaji magogo katika msitu wa taifa uliopo Mufindi mkoani Iringa.

  Miongoni mwa aliowataja ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, huku akisisitiza kuwa wamepata vitalu hivyo ‘kifisadi’.

  Dk. Slaa aliwataja mawaziri hao na watuhumiwa wengine wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Mafinga katika mfululizo wa mikutano ya hadhara na maandamano ya chama hicho yaliyoingia mkoani hapa jana.

  Alisema hatua ya mawaziri hao kumiliki vitalu hivyo si haki, kwani inasababisha kuwapo mgongano wa kimasilahi baina yao na msitu huo ambao kwa nafasi zao kama viongozi wa kiserikali walipaswa kuusimamia kwa haki na uwazi ili uwanufaishe wananchi, hususan wakazi wa Mufindi.

  Akifafanua hoja yake hiyo, Dk. Slaa alisema Dk. Chami kwa nafasi yake kama Waziri wa Viwanda na Biashara, ndiye mwenye jukumu la moja kwa moja kusimamia haki kwenye msitu huo unaotumiwa pia na Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi Paper Mills, lakini naye amechukua vitalu tena katika utaratibu aliosema si wa wazi.

  Alisema mwaka jana waziri huyo akiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ndiye aliyeongoza kamati maalumu ya serikali iliyokwenda Mufindi kuchunguza mgogoro wa kiwanda hicho pamoja na msitu kinaoutumia, lakini kinyume cha kanuni za kibunge, kiongozi huyo wa serikali sawa na wenzake akiwamo William Lukuvi aliowataja, hawakusema wazi kama wana masilahi katika msitu huo.

  “Naitaka serikali ieleze ugawaji huu wa vitalu vya msitu wa Mufindi ulitangazwa lini na utaratibu gani wa uwazi ulitumika ili kila Mtanzania wakiwamo wananchi wenyewe wa Mufindi wawe na haki ya kushindania vitalu hivyo.

  “Pili, namtaka Chami na viongozi wengine wa kiserikali waliochukua vitalu vya msitu huo wajieleze kwa nini wasiwajibishwe kwa kumiliki vitalu vya msitu bila kutangaza wazi masilahi waliyonayo ya kiuongozi katika msitu huo.

  “Tutawasha moto bungeni mpaka haki ya wananchi na msitu wao ipatikane, hawa ni mafisadi. Wakituzidi kwa wingi wao bungeni, basi tutafanya maandamano yasiyokoma nchi nzima hadi mafisadi hawa wawajibishwe na haki za wananchi zitimizwe,” alisema Dk. Slaa na kushangiliwa na umati wa watu.

  Katika orodha hiyo Dk. Slaa alimtaja pia Mbunge wa Kibakwe, Geogre Simbachawene (CCM) kugawiwa vitalu vya msitu huo.

  Alisema kwa ujumla anayo orodha ya vigogo na watendaji 540 ambao wamegawiwa vitalu vya msitu huo na kuwanyima fursa wananchi wa Mufindi kumiliki vitalu hivyo kinyume cha taratibu.

  Wakati huo huo, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Zitto Kabwe, wataongoza mashambulizi ya chama hicho bungeni kuhakikisha wananchi wakiwamo wafanyakazi walioachishwa kazi katika kiwanda cha karatasi Iringa wanalipwa mafao na stahili zao zote.

  Alisema wafanyakazi wa kiwanda hicho wanaidai serikali mafao ya jumla ya sh bilioni tano ambayo yalipaswa kulipwa mara baada ya serikali kuuza kiwanda hicho kwa wawekezaji lakini hadi leo hayajalipwa.

  Alisema CHADEMA itahakikisha inapigania masilahi ya wafanyakazi hao pamoja na wengine nchi nzima huku akisisitiza kuwa kama wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatumia ubunge wao bungeni, CHADEMA itafanya maandamano yasiyokoma nchi nzima kuhakikisha haki zao zinalipwa. Alisema maandamano hayo pia watayafanya kama serikali haitasikiliza hoja nyingine zitakazowasilishwa na wabunge hao bungeni za kupigania wananchi, kama kupigania kushushwa kwa kodi, Katiba na nyinginezo.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,842
  Trophy Points: 280
  watajibeba mwaka huu
   
 3. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  duu kwann Dr triple hakuacha hichi kichwa kikachukua nchi maisha yangekuwa tambarare .MUNGU MPE UMRI MREFU DR PHD SLAA
   
 4. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  • Awarushia pia kombora Chami, Simbachawene

  na Edward Kinabo, Mufindi


  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataja vigogo na watendaji wa serikali wakiwamo mawaziri wawili na wabunge akiwatuhumu kufanya ufisadi wa kujigawia vitalu vya uvunaji magogo katika msitu wa taifa uliopo Mufindi mkoani Iringa.
  Miongoni mwa aliowataja ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, huku akisisitiza kuwa wamepata vitalu hivyo ‘kifisadi'.

  Dk. Slaa aliwataja mawaziri hao na watuhumiwa wengine wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Mafinga katika mfululizo wa mikutano ya hadhara na maandamano ya chama hicho yaliyoingia mkoani hapa jana.
  Alisema hatua ya mawaziri hao kumiliki vitalu hivyo si haki, kwani inasababisha kuwapo mgongano wa kimasilahi baina yao na msitu huo ambao kwa nafasi zao kama viongozi wa kiserikali walipaswa kuusimamia kwa haki na uwazi ili uwanufaishe wananchi, hususan wakazi wa Mufindi.
  Akifafanua hoja yake hiyo, Dk. Slaa alisema Dk. Chami kwa nafasi yake kama Waziri wa Viwanda na Biashara, ndiye mwenye jukumu la moja kwa moja kusimamia haki kwenye msitu huo unaotumiwa pia na Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi Paper Mills, lakini naye amechukua vitalu tena katika utaratibu aliosema si wa wazi.

  Alisema mwaka jana waziri huyo akiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ndiye aliyeongoza kamati maalumu ya serikali iliyokwenda Mufindi kuchunguza mgogoro wa kiwanda hicho pamoja na msitu kinaoutumia, lakini kinyume cha kanuni za kibunge, kiongozi huyo wa serikali sawa na wenzake akiwamo William Lukuvi aliowataja, hawakusema wazi kama wana masilahi katika msitu huo.
  "Naitaka serikali ieleze ugawaji huu wa vitalu vya msitu wa Mufindi ulitangazwa lini na utaratibu gani wa uwazi ulitumika ili kila Mtanzania wakiwamo wananchi wenyewe wa Mufindi wawe na haki ya kushindania vitalu hivyo.
  "Pili, namtaka Chami na viongozi wengine wa kiserikali waliochukua vitalu vya msitu huo wajieleze kwa nini wasiwajibishwe kwa kumiliki vitalu vya msitu bila kutangaza wazi masilahi waliyonayo ya kiuongozi katika msitu huo.
  "Tutawasha moto bungeni mpaka haki ya wananchi na msitu wao ipatikane, hawa ni mafisadi. Wakituzidi kwa wingi wao bungeni, basi tutafanya maandamano yasiyokoma nchi nzima hadi mafisadi hawa wawajibishwe na haki za wananchi zitimizwe," alisema Dk. Slaa na kushangiliwa na umati wa watu.

  Katika orodha hiyo Dk. Slaa alimtaja pia Mbunge wa Kibakwe, Geogre Simbachawene (CCM) kugawiwa vitalu vya msitu huo.
  Alisema kwa ujumla anayo orodha ya vigogo na watendaji 540 ambao wamegawiwa vitalu vya msitu huo na kuwanyima fursa wananchi wa Mufindi kumiliki vitalu hivyo kinyume cha taratibu.
  Wakati huo huo, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Zitto Kabwe, wataongoza mashambulizi ya chama hicho bungeni kuhakikisha wananchi wakiwamo wafanyakazi walioachishwa kazi katika kiwanda cha karatasi Iringa wanalipwa mafao na stahili zao zote.
  Alisema wafanyakazi wa kiwanda hicho wanaidai serikali mafao ya jumla ya sh bilioni tano ambayo yalipaswa kulipwa mara baada ya serikali kuuza kiwanda hicho kwa wawekezaji lakini hadi leo hayajalipwa.

  Alisema CHADEMA itahakikisha inapigania masilahi ya wafanyakazi hao pamoja na wengine nchi nzima huku akisisitiza kuwa kama wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatumia ubunge wao bungeni, CHADEMA itafanya maandamano yasiyokoma nchi nzima kuhakikisha haki zao zinalipwa.
  Alisema maandamano hayo pia watayafanya kama serikali haitasikiliza hoja nyingine zitakazowasilishwa na wabunge hao bungeni za kupigania wananchi, kama kupigania kushushwa kwa kodi, Katiba na nyinginezo.
   
 5. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Mawaziri Wengine Tieni maji tieni Maji Fagio La Chuma Lishapatikana Kwa Wananchi Si Lilifichwa..
   
 6. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Terrible story again on gvtal officials
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ingawaje inataka roho ya mwendawazimu kumkosoa Dr. Slaa humu JF lakini mimi naridhia matokeo ya kitendo hicho.

  Nilikuwa namuangalia Lukuvi katika ITV usiku huu na alitoa maelezo ambayo kwa kweli yana-make sense ya hali ya juu kwa vile kule Mafinga kuna msitu ambao upande mmoja unamilikiwa na SPM na upande wa pili unamilikiwa na Sao Hill na haujabinafsishwa kiasi cha watu kumiliki vitalu.

  Kinachotokea ni kwamba mtu akitaka kibali cha kuvuna msitu anaomba kwa Meneja wa Msitu kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii halafu ukifanikiwa ndo unavuna. Utaratibu huu ndiyo ninaoufahamu mimi na nakumbuka hata jamaa zangu ninaowafahamu ambao ni wachuuzi wa mbao wamekuwa wakifanya.

  Hii kiu ya kutaka kuonekana kwamba wewe ni mtu wa kulipua mabomu, wakati mwingine bila kufanya utafiti wa kina kuhusu usahihi wa taarifa ambazo mara nyingi huzipata kupitia kwa watu wengine, inaweza kumvunjia heshima na mwisho anaweza kujikuta akiwa kama bwana Lyatonga alivyokuwa katika miaka ya 90 mpaka akaonekana mzushi. Natoa tahadhari tu!
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Surely we don't have officials but predators who just use their influence kujigawia na sio vipaji vya ujasiriamali!
   
 9. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wewe roho yako ya nani?
  mbona hujamkosoa Dr Slaa bali umejitolea kumtetea Lukuvi... na bado
   
 10. S

  SURNAME Member

  #10
  May 19, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe,sheria ya misitu ni tofauti na ya wanyamapori,huko waweza milikishwa kitalu but sio kwa misitu.Tatizo hapo utashambuliwa vibaya coz sie chadema hatujazoea kukosolewa na kuamini tupo sahihi kila kitu,tutarudi kule zidumu fikra za mwenyekiti.
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Tayari nimeshaanza kukiona cha mtema kuni lakini ukosoaji ambao unazingatia mapenzi badala ya hoja ni upuuzi ambao haunitishi. Habari ya Slaa imekosa umakini na matokeo yake ni kumuaibisha!
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280

  hawa walikuwa wapi kusema haya jamani...si ndo wanakataa wafanyabiashara kwenye chama hawa au/yaani nchi hii ina sanaa mpaka basi
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Kama wewe unatafsiri kwamba huo ni utetezi kwa Lukuvi basi uelewe kwamba utetezi huo ni ukosoaji wa kauli ya Slaa ambayo kimsingi ni ya uongo na upotoshaji na kufikiria kwamba kila unapokwenda ni lazima utoe bomu jipya ili watu wakuone kwamba wewe una uchungu na rasilimali za nchi wakati wenzio wote ni wezi.
   
 14. A

  Ame JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  ameeleza kwa 'kwa kufuata utaratibu' sasa tuambie huo utaratibu walifuata wangapi wakapata kama alivyopata huyo waziri? Je huoni conflict of interest hapo yeye kama government official tena kwenye high rank office kumiliki hivyo vitalu? Je nikiasi gani hiyo information imekuwa revealed kwa watanzania wakawaida ili kuwe na free compitition; je japo kuwa ni utaratibu then inawezekana kabisa huo utaratibu unafahamika na hao ambao ndiyo walio upitisha ndiyo maana huyo akapata hicho kitalu maana kwake ni rahisi kujua taratibu zote? There are many questions than answers ndiyo maana tunasema hata kama ni haki yake lakini haki yake inazidi wengine kwani yeye ndiye mwamuzi na hapo hapo mfaidikaji na ndiyo ufisadi tunaouongelea..
   
 15. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kwa hiyo wewe ni mwendawazimu haya tunashukuru kwa taarifa
   
 16. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama huo ndo utaratibu, je ni busara Lukuvi na Dr.chami, na mawaziri wengineo, au wakuu wa... kupata vibali kwa ajili hiyo????? wewe unaonaje hiyo, itakaa vema??? hakuna mgogoro wa ki masilahi hapo???
   
 17. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bado unaendelea kupotosha. Hakuna suala la vitalu kwa hiyo kusema hivyo ni kuendelea kusema uongo ambao Slaa ameusema. Suala la vibali vya kuvuna misitu ni suala ambao wale walio wafanyabiashara wa mazao ya misitu wanafanhamu na wanaujua msimu wanaotakiwa kupeleka maombi na hiyo hoja ya kwamba habari hazikuwekwa wazi ni kukosa uelewa maana hata vibali vya kuwinda au shughuli zozote vinahitaji kuwasiliana na mamlaka husika ambao ndiyo hutoa maelekezo. Ni nani alikuwa anahitaji vibali akafuata taratibu lakini asisikilizwe? Tuache kulalamika bila sababu!
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hawa ni watanzania kama wengine wote na nafasi zao haziwazuii kufanya kazi ya ujasiriamali mradi tu wanafuata taratibu. Je mgogoro hapa uko wapi? Au ni wapi walipokiuka taratibu?
   
 19. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndiyo. Machoni mwa bootlickers and syncofants!
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  huwa ninapingana na Slaa kwenye mambo mengi tu. Lakini wewe utetezi wako kwa watuhumiwa umepitiliza. Whether ni vitalu au kuvuna bado kuna tatizo la conflict of interest km hulioni unahitaji kutafutiwa dawa ya uendawazimu. Yaani mtu waziri aombe kuvuna misitu na mtu wa kawaida unategemea nini? Hapo bwana ni simple arithmetic aidha kafanye biashara au ongoza. Hili ndilo ambalo sisi km nchi ttunalipigia kelele. Ni muda upi huyu bwana anafanya biashara? Na katika hali ipi anatofautisha muda wa kuwatumikia wananchi wake kule Ismani, wannchi wa Tanzania kwa nafasi ya uwazirri na pia kuhakikisha haibiwi? Tuache kutetea yasiyoteteeka. Hata kama si kitalu, kukodi tu tayari kuna tatizo la conflict of interest. Uko wapi mpaka wa independence in mind na appearance. Yaani km Watanzania tutashindwa kuona tatizo hapa, safari yetu ni ndefu.
   
Loading...