Yethero Mgale
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 525
- 228
Wakati aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa anagombea Urais mwaka 2010, CHADEMA ilikuwa na wabunge wa kuchaguliwa na viti maalumu wasiozidi 10 ( Ndesamburo, Zitto Kabwe, Dk. Slaa, Halima Mdee na wengineo) baada ya uchaguzi CHADEMA ilivuna viti vya ubunge zaidi ya 30 na kuifanya iwe na wabunge wa kuchaguliwa na viti maalumu wapatao 48 na hivyo kuunda kambi ya rasmi ya upinzani bungeni.
Lakini hali ya mambo imekuwa tofauti kabisa mwaka huu wa 2015 ambapo CHADEMA ilimsimamisha ndugu Edward Lowassa kama mgombea wa Urais huku akiungwa mkono na vyama vya CUF, NCCR na NLD kwani CHADEMA imepata wabunge wa kuchaguliwa na viti maalum wapatao 70 ambalo ni ongezeko la wabunge 22 tu kutoka wabunge 48 waliowapata mwaka 2010.
Hivyo basi CHADEMA kwa kumsimamisha Lowassa mwaka 2015 kama mgombea wake kimepata wabunge wachache ukilinganisha na wabunge waliowapata mwaka 2010 kwa kumsimamisha Dk. Slaa kama mgombea wake bila ya kuungwa mkono na chama chochote.