Elections 2010 Dk. Slaa akataa matokeo

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kusitisha mara moja kutangaza matokeo ya urais kwa madai kuwa kuwa kura hizo 'zimechakachuliwa'.

Dk. Slaa anataka uchaguzi urudiwe na si kurudia kuhesabu kura.

Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame amemshangaa Dk. Slaa kwa kuwa hajafanya mawasiliano yoyote na tume hiyo.

Jaji Makame amesema, kama Dk. Slaa ana uhakika , apeleke nyaraka zake ili zilinganishwe na nyaraka zinazotumika kutangaza matokeo.

Akizungumza jana katika mkutano aliouitisha wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Dk Slaa aliitaka Nec isitishe kutangaza matokeo ya urais, ambayo mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiongoza, mpaka haki itakapotendeka.

Dk. Slaa ambaye katika matokeo yaliyokwishatolewa na Nec mpaka sasa ameachwa mbali na Kikwete.

Alidai katika matangazo ya kura hizo, maeneo mengi yanayotangazwa, kura zake zimebadilishwa ili kuiwezesha CCM kuibuka na ushindi.

“Baada ya kuona hali hii niiombe Nec kama tuna utashi mwema na nchi, ifute matokeo yote ya urais kwa nchi nzima na kurudia kama ilivyofanya katika jimbo moja kwa kuwa hatuwezi kukubali matokeo ya vyombo vya dola kwa kuwa tulihisi muda mrefu,” alisema Dk. Slaa.

Ametoa mfano wa Jimbo la Same Mashariki, ambako alidai ni kielelezo cha wizi wa kura.

Amedai kuwa, katika fomu yenye namba 03182, CCM ilipata kura 92 wakabadilisha na kujipa kura 123, Chadema ilipata kura halali 66 zikapunguzwa na kubaki 33.

“Tumetumia njia nyepesi ya sampuli kujua wizi huo maana aina ya pili ya wizi waliotumia ni kubuni kituo hewa, kuna kituo hewa Na 002586, kituo halali ni namba 002582 kura zinafanana katika fomu halisi hapo CCM walijipa kura 190 na Chadema 26,” alieleza.

Hata hivyo katika utangazaji wa matokeo ya urais, Nec haitangazi matokeo ya vituo vya uchaguzi kama mifano ya Dk. Slaa inavyoonesha, bali imekuwa ikitangaza matokeo ya jumla ya jimbo.

Dk Slaa pia amemtaka Mkuu wa Usalama wa Taifa , kujiuzulu mara moja wadhifa huo kwa madai kuwa, kwamba ameshindwa kuwajibika ipasavyo na kuonekana kuwa upande wa chama kimoja.
 
Wabunge waliochaguliwa kupititia chama hicho wasikubali kuingia bungeni kwa kuwa zoezi zima halikua huru na haki. la sivyo tutajua kua kila mtu walikua wanatafuta kula na sio kura.

Hapo kweli ndio tutajua kama wamechukia kweli.

KUDADADEKI
 
BABA tupo mwongozo nini kifanyike. tumesikia parapanda jana sasa tunataka uhalisia.
 
Yule mzee wa nec sio muungwana hata kidogo. Muonekano wake ni wa kikatili zaidi. Hafai kuwa kiongozi wa mahala pale.
 
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kusitisha mara moja kutangaza matokeo ya urais kwa madai kuwa kuwa kura hizo 'zimechakachuliwa'.

Dk. Slaa anataka uchaguzi urudiwe na si kurudia kuhesabu kura.

Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame amemshangaa Dk. Slaa kwa kuwa hajafanya mawasiliano yoyote na tume hiyo.

Jaji Makame amesema, kama Dk. Slaa ana uhakika , apeleke nyaraka zake ili zilinganishwe na nyaraka zinazotumika kutangaza matokeo.

Akizungumza jana katika mkutano aliouitisha wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Dk Slaa aliitaka Nec isitishe kutangaza matokeo ya urais, ambayo mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiongoza, mpaka haki itakapotendeka.

Dk. Slaa ambaye katika matokeo yaliyokwishatolewa na Nec mpaka sasa ameachwa mbali na Kikwete.

Alidai katika matangazo ya kura hizo, maeneo mengi yanayotangazwa, kura zake zimebadilishwa ili kuiwezesha CCM kuibuka na ushindi.

"Baada ya kuona hali hii niiombe Nec kama tuna utashi mwema na nchi, ifute matokeo yote ya urais kwa nchi nzima na kurudia kama ilivyofanya katika jimbo moja kwa kuwa hatuwezi kukubali matokeo ya vyombo vya dola kwa kuwa tulihisi muda mrefu," alisema Dk. Slaa.

Ametoa mfano wa Jimbo la Same Mashariki, ambako alidai ni kielelezo cha wizi wa kura.

Amedai kuwa, katika fomu yenye namba 03182, CCM ilipata kura 92 wakabadilisha na kujipa kura 123, Chadema ilipata kura halali 66 zikapunguzwa na kubaki 33.

"Tumetumia njia nyepesi ya sampuli kujua wizi huo maana aina ya pili ya wizi waliotumia ni kubuni kituo hewa, kuna kituo hewa Na 002586, kituo halali ni namba 002582 kura zinafanana katika fomu halisi hapo CCM walijipa kura 190 na Chadema 26," alieleza.

Hata hivyo katika utangazaji wa matokeo ya urais, Nec haitangazi matokeo ya vituo vya uchaguzi kama mifano ya Dk. Slaa inavyoonesha, bali imekuwa ikitangaza matokeo ya jumla ya jimbo.

Dk Slaa pia amemtaka Mkuu wa Usalama wa Taifa , kujiuzulu mara moja wadhifa huo kwa madai kuwa, kwamba ameshindwa kuwajibika ipasavyo na kuonekana kuwa upande wa chama kimoja.

kama akipata uraisi si kila siku watu wataachishwa kazi?
unafikri kujiuzulu rahisi?
 
Yule mzee wa nec sio muungwana hata kidogo. Muonekano wake ni wa kikatili zaidi. Hafai kuwa kiongozi wa mahala pale.

Dr.Slaa ndio sio muungwana kwa kutaka majibu yatangazwe anavyotaka yeye. lol
 
kama akipata uraisi si kila siku watu wataachishwa kazi?
unafikri kujiuzulu rahisi?

Ni rahisi tu ndugu yangu kama huamini fuatilia kinachotokea kenya sasa hivi. Ukiwa na tuhuma na ukaanza uchunguzi unajiuzulu hata kama hupendi. Na huko ndiko tunakoelekea.
 
DOMO KAYA ntakutafutia picha nzuri kama yako muonekano wako nimeupenda...kuhus jina nadhani nilizaliwa nikaitwa hivyo kama ambavyo wewe unaitwa Domo Kaya....point yangu ni kuwa kura zimechakachuliwa wanamapinduzi wamedhulumiwa haki yao mchana kweupe hivyo basi ni jukumu la wale tuliowachagua watuongoze lakini kura zetu zikaibwa. watuambie ama tufanye maandamano ya amani nchi nzima kupinga matokeo, ama wabunge wao wagome kuingia bungeni, ama tutumie kile kilichonenwa kuwa AMANI haiji ila kwa njia ya UPANGA...kaka Kenya, Zimbabwe, South Africa (Apartheid), Liberia, Sierra leone, Congo na Africa zote unazozijua wewe ambapo watu walipochoka tumeona mabadiliko zikafanikiwa...leo hii bado Somalia, nadhani ni muda muafaka kuwaunga mkono hawa jamaa... Mifano mingine ongezea wewe!
 
Domo Kaya napenda nikukosoe hapa pia. Haisemwi kuwa Dr. Slaa anataka matokeo yatangazwe kama anavyotaka yeye, anachokisema ni kwamba matokeo yatangazwe kwa idadi ya kura zilizopatikana baada ya wasimamizi na mawakala kuhesab kwenye vituo vyao. Lakini hapa kinachotokea kwenye tume ni kwamba L. Makame na wenzake wanatangaza matokeo tofauti na yale yaliyokwishatolewa kwa mawakala baada ya zoezi la uhesabuji wa kura. Na kwa taarifa yako kila wakala nchi nzima ile siku ya jumapili baada ya kura kuhesabiwa walikabidhiwa nakala za matokeo ya udiwani, ubunge na urais. Wale mawakala walikabidhi nakala zile kwa viongozi wao ili matokeo yatakapoanza kutangazwa yalingane na yao. lakini kinachotokea hapa matokeo yanayotangazwa sasa sio sawa na yale ambayo chama cha CHADEMA wanayo, na ndio maana Dr. Slaa kaiambia tume isitishe mara moja zoezi hilo kwani ushahidi wanao. na sisi tuliopiga kura hasira yetu iko hapo baada ya kugundua ukweli huu. Domo Kaya hebu jiulize mwenyewe yaliyotokea Segerea ni halali (tuanzie hapo).
 
Back
Top Bottom