Dk. Slaa aizidi ujanja CCM

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Dk. Slaa aizidi ujanja CCM

na Moses Ng'wat, Mbeya

amka2.gif
WAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikimnyemelea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Sambwee Shitambala, aliyejiuzulu siku za hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, amemrejesha kiongozi huyo kundini. Mara baada ya kumrejesha Shitambala kwenye nafasi yake, Dk. Slaa aliwaonya na kuwasuta baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho ambao wanafikiri kuwa majungu na fitina ni mtaji unaoweza kuwanufaisha na kufikia malengo binafsi ambayo hayana tija kwa chama hicho.
Shitambala alijiuzulu nafasi hiyo hivi karibuni kupisha uchunguzi baada ya kutuhumiwa kupokea rushwa ya sh milioni 600 ili kukihujumu chama hicho dhidi ya CCM katika uchaguzi mkuu, jimbo la Mbeya Vijijini.
Uamuzi wa CHADEMA kumrejesha Shitambala katika nafasi hiyo na yeye kuridhia, ulitangazwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Mashauriano la Mkoa, uliofanyika katika Hoteli ya Royal Zambezi na kuhudhuriwa na zaidi ya wajumbe 100 kutoka wilaya za mkoa wa Mbeya.
Dk. Slaa alisema baada ya kupokea taarifa na chama hicho kufanya uchunguzi, kimebaini kuwa tuhuma zilizotolewa dhidi ya kiongozi huyo si za kweli na kwamba chama hakikuhusika kutoa tuhuma hizo bali ni baadhi ya maofisa wa chama hicho makao makuu ya chama na wanachama mkoani humo ndio walizusha tuhuma hizo bila kuwa na uhakika.
“Sisi kama CHADEMA tulipokea taarifa za kujiuzulu kwa Mwenyekiti Shitambalaa na kuamua kuunda jopo la watu walioshughulikia sakata hilo, hivyo kilichobainika ni maofisa wa chama ambao ni mavoruntia walitoa tuhuma hizo koridoni na si kwenye chama na hata walipobanwa waliishia kusema nao wamesikia,” alisema Dk. Slaa.
Aidha, aliongeza kuwa hata kikao cha Baraza la Mashauriano la Mkoa huo lililokaa Novemba 27, mwaka huu, mkoani hapo, kimethibitisha kuwa Shitambala hakuhongwa kiasi hicho cha fedha ambacho baadhi ya wanachama walikuwa wakimtuhumu.
Kadhalika Dk. Slaa amempongeza Shitambala kwa ujasiri wake wa kukubali kuachia ngazi ya nafasi hiyo kubwa ndani ya chama ili kupisha uchunguzi kwa kuwa kitendo hicho ni nadra kutokea kwa viongozi wa kisiasa hasa inapofikia wanatuhumiwa iwe kwa rushwa au sababu nyingine zinazosababisha mtafaruku ndani ya chama.
Alimwelezea Shitambala kuwa ni kiongozi asiye na tamaa na mwenye uwezo mkubwa wa kulinda maadili ya uongozi kwani amehimili tamaa ambazo zingeweza kutumiwa na wabaya wa CHADEMA kumnunua kwa gharama yoyote.
Ingawa hakuwataja wabaya wa CHADEMA ni wazi alikuwa akiihusisha CCM kwa kuwa ndio chama kinachoonekana kuiogopa CHADEMA hasa baada ya kutoa upinzani mkubwa katika uchaguzi mkuu uliopita, hali iliyosababisha kupoteza wabunge wengi.
Lakini pia hali hiyo ingekuwa imewarahisishia mafisadi ambao wanaiona CHADEMA hatari kwao kutokana na kuwaumbua hadharani kumrubuni kiongozi huyo wa mkoa wa Mbeya kwa lengo la kubaini siri na mikakati ya chama hicho dhidi ya mafisadi ndani ya CCM na serikali.
Hata hivyo kukosekana kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, aliyetajwa kuwa ni sehemu ya mgogoro ulioibuka na kusababisha Shitambala kujiuzuru, Dk. Slaa alisema kiongozi huyo hakufika mkoani Mbeya kwa kuwa alikuwa mkoani Kilimanjaro katika zoezi la kutafuta Meya.
“Baada ya uongozi wa taifa kualikwa kwenye mkutano wa baraza hili na kujikuta tarehe za mkutano zimeingiliana na mambo muhimu kama hayo ya uchaguzi wa Meya, tulishauriana na mimi kuja hapa kwa kofia mbili,” alisisitiza Dk. Slaa.
Wakati huohuo Dk. Slaa ametoa tahadhari kwa wabunge wote wa chama hicho wanaotengeneza urafiki wa kufungamana na wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwa hizo ni dalili za kutoa mwanya wa kufungwa midomo na kuvunja nguvu ya mapambano.
“Ole wenu nyinyi wabunge…akiwageukia wabunge watatu wa mkoa Mbeya, Joseph Mbilinyi Mbeya Mjini, David Silinde Mbozi Magharibi, na yule wa viti maalum walikuwepo ukumbini hapo, mkianza tabia ya kujipendekeza kwa wakurugenzi maana ukishafikia hapo utajikuta unajaziwa mafuta, mara hiki na hapo ujue fika mapambano dhidi ya ukombozi wa wananchi yamekwisha.”
Akipokea uamuzi wa chama chake kumrudishia nafasi aliyojiuzulu baada ya kubainika kuwa hakuhusika na tuhuma za rushwa zilizotolewa dhidi yake, Shitambala alipokea kwa furaha na kuahidi kuendeleza kazi za chama hicho kwa moyo safi.
Hata hivyo alikebehi uvumi ulioenezwa na wabaya wake na propaganda za CCM kuwa alikuwa na mpango wa kuhamia chama hicho kwa kusema yeye ni mtu makini aliye na msimamo usioyumba yumba.
 
I salute you Shitambala. Umekuwa mfano wa viongozi ambao Tanzania inawahitaji.
 
Mkisikia mengine msianze tena kumponda, kwani haya ni pati gazeti tu, mchezo kamili haujaanza!
 
Huyu jamaa kaumbua wana ccm na viongozi wa serikali ambao wakituhumiwa hawawajibiki. Ni mfano mkubwa sana, naomba wengine waige, kuanzia na zitto ambaye hata ameshapigiwa kura ya kutokuwa na imani lakini bado kang'ang'ania
 
Hii hi hatua ya ukomavu kwa CDM hasa kwa kiongozi aliyekubali kujiudhuru na kupisha uchunguzi juu yake halafu baadae anakubali kuwa kuendelea na nafasi yake baada ya uchunguzi kukamilka. Najua wapo wenye kukiombea mabaya CDM hasa baada ya kusikia harufu ya kinyesi cha mpasuko wa uongozi nawaonea sana huruma maana CDm wanajua kuwa wao ndio wamebeba matumaini mapya ya watanzania ndio maana wakaaminiwa kwa kupata kura nyingi na wabunge achilia mbali zile zilizochakachuliwa ambazo ushahidi wake upo.

Naomba kuwasilisha.
Mtoi
 
Aliwabeep CCM wakapiga jamaa akakata simu. Bomba Shitambala, wewe mwanaume kweli, huna tamaa, ni wachache viongozi wenye uzalendo wa kweli kama wewe.
Kwa ccm kiongozi kutuhumiwa halafu akajiuzulu kupisha uchunguzi ni ndoto, labda kwa mtutu wa bunduki.
 
huu ndio uwajibikaji katika jamii, sio kung'anga'nia madaraka tu hata unapokuwa unatuhumiwa
bravo Shitambal na Chandema
 
Dk. Slaa aizidi ujanja CCM

na Moses Ng'wat, Mbeya

amka2.gif
WAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikimnyemelea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Sambwee Shitambala, aliyejiuzulu siku za hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, amemrejesha kiongozi huyo kundini. Mara baada ya kumrejesha Shitambala kwenye nafasi yake, Dk. Slaa aliwaonya na kuwasuta baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho ambao wanafikiri kuwa majungu na fitina ni mtaji unaoweza kuwanufaisha na kufikia malengo binafsi ambayo hayana tija kwa chama hicho.
Shitambala alijiuzulu nafasi hiyo hivi karibuni kupisha uchunguzi baada ya kutuhumiwa kupokea rushwa ya sh milioni 600 ili kukihujumu chama hicho dhidi ya CCM katika uchaguzi mkuu, jimbo la Mbeya Vijijini.
Uamuzi wa CHADEMA kumrejesha Shitambala katika nafasi hiyo na yeye kuridhia, ulitangazwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Mashauriano la Mkoa, uliofanyika katika Hoteli ya Royal Zambezi na kuhudhuriwa na zaidi ya wajumbe 100 kutoka wilaya za mkoa wa Mbeya.
Dk. Slaa alisema baada ya kupokea taarifa na chama hicho kufanya uchunguzi, kimebaini kuwa tuhuma zilizotolewa dhidi ya kiongozi huyo si za kweli na kwamba chama hakikuhusika kutoa tuhuma hizo bali ni baadhi ya maofisa wa chama hicho makao makuu ya chama na wanachama mkoani humo ndio walizusha tuhuma hizo bila kuwa na uhakika.
"Sisi kama CHADEMA tulipokea taarifa za kujiuzulu kwa Mwenyekiti Shitambalaa na kuamua kuunda jopo la watu walioshughulikia sakata hilo, hivyo kilichobainika ni maofisa wa chama ambao ni mavoruntia walitoa tuhuma hizo koridoni na si kwenye chama na hata walipobanwa waliishia kusema nao wamesikia," alisema Dk. Slaa.
Aidha, aliongeza kuwa hata kikao cha Baraza la Mashauriano la Mkoa huo lililokaa Novemba 27, mwaka huu, mkoani hapo, kimethibitisha kuwa Shitambala hakuhongwa kiasi hicho cha fedha ambacho baadhi ya wanachama walikuwa wakimtuhumu.
Kadhalika Dk. Slaa amempongeza Shitambala kwa ujasiri wake wa kukubali kuachia ngazi ya nafasi hiyo kubwa ndani ya chama ili kupisha uchunguzi kwa kuwa kitendo hicho ni nadra kutokea kwa viongozi wa kisiasa hasa inapofikia wanatuhumiwa iwe kwa rushwa au sababu nyingine zinazosababisha mtafaruku ndani ya chama.
Alimwelezea Shitambala kuwa ni kiongozi asiye na tamaa na mwenye uwezo mkubwa wa kulinda maadili ya uongozi kwani amehimili tamaa ambazo zingeweza kutumiwa na wabaya wa CHADEMA kumnunua kwa gharama yoyote.
Ingawa hakuwataja wabaya wa CHADEMA ni wazi alikuwa akiihusisha CCM kwa kuwa ndio chama kinachoonekana kuiogopa CHADEMA hasa baada ya kutoa upinzani mkubwa katika uchaguzi mkuu uliopita, hali iliyosababisha kupoteza wabunge wengi.
Lakini pia hali hiyo ingekuwa imewarahisishia mafisadi ambao wanaiona CHADEMA hatari kwao kutokana na kuwaumbua hadharani kumrubuni kiongozi huyo wa mkoa wa Mbeya kwa lengo la kubaini siri na mikakati ya chama hicho dhidi ya mafisadi ndani ya CCM na serikali.
Hata hivyo kukosekana kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, aliyetajwa kuwa ni sehemu ya mgogoro ulioibuka na kusababisha Shitambala kujiuzuru, Dk. Slaa alisema kiongozi huyo hakufika mkoani Mbeya kwa kuwa alikuwa mkoani Kilimanjaro katika zoezi la kutafuta Meya.
"Baada ya uongozi wa taifa kualikwa kwenye mkutano wa baraza hili na kujikuta tarehe za mkutano zimeingiliana na mambo muhimu kama hayo ya uchaguzi wa Meya, tulishauriana na mimi kuja hapa kwa kofia mbili," alisisitiza Dk. Slaa.
Wakati huohuo Dk. Slaa ametoa tahadhari kwa wabunge wote wa chama hicho wanaotengeneza urafiki wa kufungamana na wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwa hizo ni dalili za kutoa mwanya wa kufungwa midomo na kuvunja nguvu ya mapambano.
"Ole wenu nyinyi wabunge…akiwageukia wabunge watatu wa mkoa Mbeya, Joseph Mbilinyi Mbeya Mjini, David Silinde Mbozi Magharibi, na yule wa viti maalum walikuwepo ukumbini hapo, mkianza tabia ya kujipendekeza kwa wakurugenzi maana ukishafikia hapo utajikuta unajaziwa mafuta, mara hiki na hapo ujue fika mapambano dhidi ya ukombozi wa wananchi yamekwisha."
Akipokea uamuzi wa chama chake kumrudishia nafasi aliyojiuzulu baada ya kubainika kuwa hakuhusika na tuhuma za rushwa zilizotolewa dhidi yake, Shitambala alipokea kwa furaha na kuahidi kuendeleza kazi za chama hicho kwa moyo safi.
Hata hivyo alikebehi uvumi ulioenezwa na wabaya wake na propaganda za CCM kuwa alikuwa na mpango wa kuhamia chama hicho kwa kusema yeye ni mtu makini aliye na msimamo usioyumba yumba.
Huyu SLAA ni genious, ningekuwa na uwezo wa kumfanya mwenyekiti wa taifa wa CDM??????
Nimeufurahia uamuzi
 
Mkisikia mengine msianze tena kumponda, kwani haya ni pati gazeti tu, mchezo kamili haujaanza!
mchezo utauanzisha wewe!???
nenda kamalize mgogoro wako ndani ya chama chako usijeshabikia yawenzio wakati makamba anamaliza chama!
 
Back
Top Bottom