Dk. Slaa aivuruga Kamati Kuu CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa aivuruga Kamati Kuu CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kasyabone tall, Oct 13, 2010.

 1. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Dk. Slaa aivuruga Kamati Kuu CCM
  • CHADEMA yashtukia mkakati wa kuiba kura zao

  na Mwandishi wetu


  [​IMG] ZIKIWA zimesalia siku 18 kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu, Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC), imekiri kuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ni tishio, hivyo imepanga mikakati mizito kumkabili, Tanzania Daima Jumatano imebaini.
  Moja ya mikakati hiyo ni pamoja na kuwaangukia viongozi na marais wastaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, ambao sasa wamekubali kwenda kumpigia kampeni Rais Kikwete.
  Uamuzi huo wa Kamati Kuu ya CCM, umefikiwa mwishoni mwa wiki wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, ambacho pamoja na mambo mengine, kilifanya tathmini ya mwenendo wa kampeni na kuweka mikakati ya kumkabili Dk. Slaa katika kipindi hiki kilichobaki.
  Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, CC ililazimika kuwaangukia wastaafu hao ambao wamekubali kumpigia debe Kikwete siku chache kabla ya uchaguzi.
  Chini ya mkakati huo, CC imeazimia kuongeza nguvu ya fedha na hata kukodisha helikopta nyingine zinakazotumiwa na wastaafu hao na kuongeza matangazo kwenye vituo vya televisheni na redio ili kuwashawishi wananchi wampigie kura Kikwete.
  “Kwa kifupi CC imekiri kwamba Dk. Slaa ana nguvu na anaungwa mkono na wengi, hivyo wazee; Mkapa, Mwinyi, Malecela na wengine, wanaanza kumpigia kampeni JK na watapita maeneo yale ambayo Dk. Slaa amepita,” kilisema chanzo chetu cha habari.
  Awali mgombea wa CCM ambaye anatetea kiti chake alikuwa akipita huku na kule akijinadi mwenyewe kama mtoto mkiwa.
  Jambo la kustaajabisha ni kwamba wazee na viongozi wengine wastaafu wa serikali zilizopita ambao wanavikwa heshima kubwa na Watanzania, ukiachia siku ya uzinduzi, hawakushiriki kampeni za Kikwete, hali iliyoibua hisia kwamba ama wamewekwa kando kwa makusudi au wamejiweka pembeni wenyewe.
  Mbali na Mwinyi na Mkapa kutokuwapo kwenye kampeni, makamu wenye viti wa CCM, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Pius Msekwa Bara, nao wamekacha kampeni hizo.
  Mawaziri wakuu wastaafu, Joseph Warioba, Cleopa Msuya, Frederick Sumaye, Salim Ahamed Salim na wengi wengineo, hawajaonekana hata mara moja kwenye majukwaa ya CCM.
  Kada pekee aliyebakia Dar es Salaam, Abdulrahman Kinana, akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Mkakati wa Kampeni ya CCM, amekuwa akijibu hoja kwa waandishi wa habari kila inapotokea Dk. Slaa amerusha kombora.
  Habari zaidi zilisema kuwa CC pamoja na mambo mengine, ilitumia muda mwingi kujadili kasi ya Dk. Slaa tangu alipoanza kampeni na uwezo alionao kifedha na kujiridhisha kwamba si wa kumbeza kutokana na mvuto wa kisiasa alionao kila alipokwenda.
  Hadi sasa CCM imekwisha kutumia mbinu tatu za kutaka kummaliza kisiasa Dk. Slaa na kupunguza kura zake kwa kuibua kashfa na uzushi ili kumchonganisha kwa wananchi bila mafanikio.
  Mbinu ya kwanza iliyotumiwa na makachero wa chama hicho tawala ni pamoja na kuibua hoja ya udini kwamba Dk. Slaa anaungwa mkono na Wakristo.
  Pia waliibua kashfa ya maisha yake binafsi kuhusiana na mwanamke aliyenaye sasa na anayetarajia kufunga naye ndoa, Josephine Mshumbusi, kwamba ni mke wa mtu. Kesi hiyo sasa ipo katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
  Pia ameibuliwa hoja kwamba anachochea wananchi kumwaga damu. Katika hoja hiyo, makachero wa CCM wanasambaza ujumbe mfupi kupitia kampuni za simu za mikononi wakidai Dk. Slaa ni mropokaji, anayetaka kumwaga damu.
  Hata hivyo Dk. Slaa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wamekana kutoa kauli hiyo na kulitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua viongozi wanaodaiwa kutoa kauli hiyo.
  Katika hatua nyingine, CHADEMA imedai kubaini mkakati wa kuiba kura kwa kutumia mtandao wa kompyuta.
  Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, aliiambia Tanzania Daima Jumatano kuwa tayari wameijulisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), juu ya kuwapo mpango huo na kwamba chama chake kimejiandaa kukabiliana na hujuma hiyo.
  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tayari chama hicho ambacho kinapewa nafasi kubwa ya ushindi kimebaini kuwapo kwa vituo hewa vya kupigia kura na makachero wao wanaendelea na uchunguzi wa kina.
  Hata hivyo Mnyika hakutaka kuuweka wazi mkakati huo kwa hofu ya kuwapa wapinzani wao mbinu nyingine ya kuiba kura.
  Wakati huohuo, Dk. Slaa amewataka wanachama wa CHADEMA kuwa wa mwisho kuanzisha vurugu kabla na baada ya uchaguzi.
  Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wake wa kampeni, uliofanyika Kibondo, mkoani Kigoma.
  Alisema kuwa CHADEMA haitakubali kuona wafuasi wake wakianzisha vurugu na kusisitiza kuwa hata wakichokozwa wasilipe kisasi, kwani CCM itapata kisingizio.
  Pia amemtaka Rais Kikwete kuacha kuhubiri amani majukwaani kama hatakuwa tayari kutekeleza azima hiyo kwa vitendo, kwa kuvifuta vikundi vya Green Guard, ambao alisema wamekuwa chanzo cha kuvuruga amani.
  Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ametangaza majimbo ambayo CHADEMA ina uhakika wa kushinda.
  Aliyataja majimbo hayo kuwa ni Kigoma Kaskazini, Mhambwe, Kigoma Mjini na Manyovu
   
 2. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kuna wazee ambao hawaungi mkono hali iliyopo sasa kama Mkapa. Lakini Mzee mwinyi naweza kukubali kwa sababu ya ile kawaida yake ya Ruksa.

  Lakini Kwao wao kama viongozi wa CCM lazima wapige campaign za CCM. Si tatizo maana hata Mwal. Nyerere alimpigia Mkapa. Huo ni wajibu wao. Chamaana hapa ni hizi Rafu wanazocheza CCM. Kumchafua wazi wazi Dr. Slaa kwa msg za simu na Vyombo husika vinakwepa kusema kuwa ni wao.

  Kithibitisha hilo Leo tena CCM wanatuma jumbe kama hizo wao wenyewe kutumia mtandao wao. Msg ni za aina ile ile ila tu wamerekebisha kidogo. Kutuibia hela CCM ni kawaida yao sana tu, si ajabu. na ndiyo maana hata mgombea urais wetu anajinadi kwa kusema ametumia mamilioni kwa Maji, shule, hospitali bila ya kupima kama zimetumika kweli. THEY ARE NOT SERIOUS OF OUR MONEY!

  So CCm watashinda nionavyo hali ya kampeni lakini kwa rafu nyingi na nguvu nyingi sana.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Hivi REDET mnaosema Dr. Slaa anakubalika kwa asilimia 12 na SYNOVATE mnaodai anakubalika kwa asilimia 16 mna utetezi gani?

  Hao wastaafu sana sana watawakumbusha wapigakura machungu mengi waliyoyapata chini ya himaya zao. Kukaa kwao pembeni kunatokana na kutokubalika kwao.

  Mkapa tutamwuliza juu ya machimbo ya KIWIRA.

  Mwinyi tutamwuliza juu ya hivi ni kwanini anatetea mafisadi?

  Msuya tutamwuliza alikuwa anaamanisha nini pale aliposema "kila mmoja abebe msalaba wake"?

  Sumaye tutamwuliza atueleze mmiliki wa hoteli ya kitalii ya MOUNT MERU ni nani?

  Warioba tutamwuliza atueleze ubia wake kwenye EPA unaanzia wapi na unaishia wapi?


  Na wengine tutawauuliza watueleze ubia gani wanao na utawala wa kiimla wa JK ambaye tayari ametangazia umma URAISI ni suala la kifamilia?


   
 4. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MTWA, jibu ni moja mimi na wewe tumwage chini hapo october 31, hakika hata wakishinda roho zetu zitakuwa siyo kama tungewachagua, tutakaa tukiwacheka hao wanaowachagua kwa kuwa watashuhudia jinsi watakavyorudisha hela zao.

  CCM wanauroho wa mali, kila kiongozi anagombea ili apate siyo kuifanyia kitu hii nchi. Uzalendo haupo tena kwa viongozi wetu, inatisha saaana unapoona hata vijana wanakimbilia siasa kwa nia ya kujitajirisha. Tumpeni kura Dr Slaa, tuone katiba itakavyoabadilika tutajaa humu tukipongezana hata kama hatujuani tutacheers!
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wao bana wafanye wafanyavyo, ukweli ni kuwa maji shingoni na yanaelekea puani!!

  VOTE FOR CHADEMA!
   
 6. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkapa ametoa masharti kwa CC kabla ya kukubali kumpigia debe Kikwete
  1. Kufuta kesi inawakabili Basil Mramba, Yona na Mgonja
  2. Kuwazuia familia ya Kikwete kuendelea kukampeni wazi wazi kwa sababu wanakiharibia chama cha mapinduzi zaidi ya kukijenga.
  3. Chama chao kikanushe kwamba hakitumii mbinu za kuendekekeza udini kwenye kampeni.

  Huyu Mzee Mkapa anaonyesha kukerwa na Kikwete kwa jinsi alivyoharibu mafanikio aliyokuwa amefikia wakati wa utawala wake. Anakumbuka sana usemi ule wa Baba wa taifa wa Watanzania kuwa watu wa ajabu sana, wanaacha mambo mazuri na mafanikio tuliyokuwa tumepata na kukumbatia mabaya tu ( ufisadi ) tuliyofanya.
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,887
  Trophy Points: 280
  CCM wanaogopa nini wakati wameshasema Mgombea wao anakubalika kwa kiwango kikubwa? Na hao wazee kama watasimama na kutetea uozo uliopo sasa hivi,nasi tutawaingiza katika kundi moja na wa sasa. Kutunza heshima yao wajitenge na hii CCM ya sasa mpaka hapo itakaporejea kwenye misingi yake ya awali.
   
 8. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  tena hao wastaafu ndio tuliokuwa tukiwasubiri sana, mkapa anapaswa kuwaeleza watanzania kuhusu mgodi wa kiwira aliojimilikisha, namna familia yake na mama anna makapa walivyoshiriki kuifilisi ttcl, namna alitoa amri wa wachimbaji wadogo wadogo kufukiwa wakiwa hai huko bulyanhulu na mauaji ya wapemba mwaka 2001. Mkapa ndiye alitoa ruksa ya kuchotwa kwa bilioni 133 fedha za epa kutoka benki kuu akiwa kama rais.

  Mzee mwinyi anapaswa kuwaeleza watanzania kuhusu ufisadi wa ubinafisishaji wa loliondo ambapo mwarabu brigedia alimilikishwa ardhi ya wamasai na hivyo kupelekea wamasai kuhama na mifugo yao na kuhamia maeneo ya wakulima na hivyo kuwepo mapigano ya mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima

  wengine weny data za ufisadi uliofanyika wakati wa uongozi wa wazee hao waanze mapema kuweka hapa ili tujikumbushe ufisadi huo
   
 9. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  HAYATI Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alitumia nguvu za ziada kumnadi Mkapa kwavile ni ukweli usiopingika kwamba Mkapa alikuwa hakubaliki. Mrema alikuwa tishio sana kwa Mkapa na ndio maana kulihitajika nguvu ya ziada ambayo pamoja na jitihada zote hizo bado Mkapa alishindwa hata kufika 65%!! Hii ni tofauti na Kikwete! Katika uchaguzi ule(1995) Nyerere alikuwa anakubalika zaidi kuliko Mkapa na ndio maana ilibidi mzee wa watu(Nyerere) aache kila kitu kumnususru Mkapa! Ni ukweli usipingika kwamba Dr. Slaa ana nguvu lakini naamini hajafikia kabisa nguvu zile ambazo alifikia Mrema 1995 na anayekataa ukweli huu basi asubiri Oct 31 tuone endapo atapata angalau 20% (Mrema alipata abt 28%)!
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nyie jiandaeni kuiba tuuu hakuna njia nyingine ya kufanya zaidi ya hiyo, Ila bila hivyo Slaa ataingia madarakani wala msijidanganye na kujipa moyo! MUIBE NA LAANA IWE JUU YENU!
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Bila kuiba CCM haina kitu hapa. Wakati wa Mrema mambo yalikuwa tofauti sana na leo. Watu walikuwa bado na uwoga wa mabadiliko na CCM iliogopewa sana. Leo tuko huru na tunaweza hata kujadili freely kweny mitandao na magazeti. Unafikiri 1995 akina Ulimwengu, Mwanakijiji, n.k. wangeweza kuja na article zao kwenye magazeti kuwaeleza watu uhuru wao wa kuchagua kiongozi bora??

  CCM bila kufanya kama Kenya na Zimbabwe, Dr. Slaa atakuwa Magogoni 5 November 2010.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  SYNOVATE NA REDET wanasema CCM iko juu sasa hao wastaafu wa nini mtaishia kuamsha hasira za wananchi bure
   
 13. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Washajivuruga wenyewe. Sanasana slaa kamalizia walichoanza.. hayati baba wa taifa angekuepo angehama chama
   
 14. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2010
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  YAANI HATA WAKAMLETE BARAKA OBAMA NA CONVINCING POWE YAKE, mimi bado kura yangu ni kwa Dr Slaa
  Hao wanataka kumpigia campaign, baada watamwacha mwenyewe atakaposhindwa hawatamsaidia. Cha msingi ni watu kutodanganyika mkwa muda huu uliobaki, tumeshamjua Rais ajaye kilichobaki ni kuweka kitambulisho ya kupigia kura vizuri
   
 15. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Yaani nimecheka sana kusoma kuwa Kikwete amempigia magoti Mkapa ili aje kusaidia kampeni. Huyu ni the same Kikwete ambaye ametumia kila anachoweza kumpondea Mkapa na Sumaye kwa kutumia vyombo vya habari for the last four years.

  Ama kweli ngoma inogile
   
 16. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tangu mwanzo wastaafu walikataa kuingia kwenye kampeni wakatoa masharti kuwa makamba aondolewe kwani anaharibu chama na kikwete aache kutumia kampeni kama suala la kifamilia.

  Sijui masharti hayo yamefikia wapi!!
   
 17. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mungu inusuru Tanzania
   
 18. p

  pierre JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tupe kiongozi bora ee Mungu
   
 19. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...akuanzae mmalize...nimeshafanya maamuzi tutakutana nao Oct 31
   
 20. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Iwapo nitaaga dunia kabla ya CCM kung'oaka madarakani roho yangu itaondoka ikiwa na huzuni kubwa sana na laiti kama nitakutana na Mwl Nyerere nitamueleza kuwa chama chake kimemezwa na Mafisadi na Tanzania imevunda kwa rushwa.
   
Loading...