Dk. Slaa aigomea sheria ya maadili

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,087
Dk. Slaa aigomea sheria ya maadili

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya watu

MBUNGE wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuna haja ya kuzifanyia marekebisho sheria za nchi, ili ziweze kuwabana viongozi kutaja mali na kuwafikisha mahakamani pindi wanapokwenda kinyume cha maadili.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini hapa, Dk. Slaa alisema sheria za sasa zinatoa upenyo mkubwa sana kwa viongozi kufanya makosa na kuzitumia kama kinga ya kutoadhibiwa.

Alisema moja ya sheria ambayo inapaswa kubadilishwa na ile ya maadili ya watumishi wa umma, ambayo inatamka bayana kuwa si ruhusa kwa mtu yeyote kutangaza mali za kiongozi baada ya kuonyeshwa na Tume ya Maadili.

Dk. Slaa alisema ulegelege wa sheria za nchi hivi sasa umewafanya viongozi wa serikali kufanya makosa na kukimbilia kujiuzulu, huku wakiwa na uhakika wa kutoguswa na sheria.

“Nafikiri sasa ndiyo muda wa mabadiliko haya ya sheria zetu kama kweli tuna nia ya kukabiliana na hawa viongozi wanaotafuna mali zetu kwa masilahi binafsi,” alisema Dk. Slaa.

Alisema mchakato wa kubadilisha sheria hizo ni lazima uanzie kwa wabunge na wananchi waupokee, ili kuleta mabadiliko na kurudisha uwajibikaji kwa watawala.

Dk. Slaa alisema Bunge linapaswa kuanza kuonyesha meno yake kipindi hiki ambacho idadi ya viongozi wanaovunja maadili ya umma kwa kujilimbikizia mali inazidi kuongezeka siku hadi siku.

Aidha, alipendekeza kuwa kila waziri anayejiuzulu aachie pia na wadhifa wa ubunge kwani anakuwa hajawatendea haki wapiga kura wake kwa kuwanyonya.

“Hawa mawaziri wanaoachia ngazi sasa inabidi waachie na ubunge, kwani walichokifanya na kulazimika kujiuzulu nyadhifa zao ni sawa na kuwahujumu wapiga kura wao,” alisema Dk. Slaa.

Kauli hiyo ya Dk. Slaa, ilionekana kuwa na uzito zaidi kwani juzi katika kikao cha Bunge, Mbunge wa Koani Haroub Said Masoud (CCM), alitaka mwongozo wa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuhusu uwezekano wa kuundwa kwa kamati ya Bunge ya kuwashughulikia mafisadi.

Mbunge huyo alisema vitendo vya kifisadi hivi sasa vimeshamiri mno kiasi cha kurudisha nyuma maendeleo ya taifa, hivyo ni wakati muafaka wa kuunda kamati ya Bunge ya kuwashughulikia.
 
Sawa sawa baba,

Jitihada zifanywe ili initiative ya Zitto (proposed Bill currently being drafted see here) iwe makini kiasi cha kutoacha mwanya wowote wa kupenyea mafisadi.
 
Tuko wote Dr Slaa.......keep it up!

Ningependa kusikia msimamo wa Pinda katika hili.........waandishi siku mkikutana na huyu Pinda mtupieni hilo swali.........nini maoni yake kuhusu sheria ya maadili ya viongozi mali zao kutotajwa
 
Tujiulize kwanza ni nani alikwamisha hii hoja binafsi ya Zitto? Na alitoa sababu gani? Halafu tukishapata majibu ndio tuanzie hapo kuirudisha bungeni na kuhakikisha inapita, tena kwa haraka.
 
Kuna LIBABU LIMOJA LINAITWA MARMO ndilo LILILOZUIA (then) hoja ya Zitto

.....shame on you Marmo.......mijitu kama Marmo sijui inafanya kazi kwa faida ya nani
 
Back
Top Bottom