Dk Slaa afichua wakuu wa wilaya wanaoisadia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa afichua wakuu wa wilaya wanaoisadia CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jul 2, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  KATIBU mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Willbroad Slaa amesema anazo nyaraka maalumu za CCM zinazowaagiza wakuu wa wilaya kuwaita wafanyabiashara ili wakichangie chama hicho fedha wakati huu wa uchaguzi.

  Dk Slaa alisema kwamba, nyaraka hizo pia zinawaagiza Watendaji wa Vijiji wakichangishie chama hicho.

  Dk Slaa ambaye ni mbunge wa Jimbo la Karatu mkoani Arusha aliibua suala hilo bungeni jana katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Alisema katika wakaraka huo wa CCM, wafanyabiashara wanatakiwa kuchangia kuanzia Sh20,000 na watendaji wa wijiji wachangiekuanzia Sh10,000.

  Katika swali lake kwa Waziri Mkuu, Dk Slaa alisema; “Mheshimiwa Waziri Mkuu, hivi sasa wakuu wa wilaya wanatumia ofisi, vyombo vya umma na mali nyingine za serikali kuwaita ofisini wafanyabiashara bila ya hiari yao ili waichangie CCM na kila mtendaji wa kijiji aichangie CCM?”

  Pinda alijibu; “Kiufupi, kama hawajalazimishwa wala kusurutishwa kuchangia fedha hizo hakuna tatizo, lakini kama watalazimishwa hilo ni tatizo.”

  Kufuatia majibu hayo, Dk Slaa alilazimika kusimama tena na kusema kuwa anazo nyaraka maalumu kutoka CCM zinazowaelekeza wakuu wa wilaya kuzunguka katika kata pamoja na vijiji vyote kutekeleza maagizo hayo.

  “Ninazo nyaraka maalumu za CCM zinazowaelekeza wakuu wa wilaya kuzunguka katika kata pamoja na vijiji vyote kuichangishia fedha pamoja na kuwataka watendaji wa Vijiji kufanya hivyo pia,” alisema

  Alisema nyaraka hizo zinawataka wakuu wa wilaya kuwataka wafanyabiashara kukichangia chama hicho kuanzia Sh20,000 na Mtendaji wa Kijiji achangishe kuanzia Sh10,000.

  Dk Slaa ambaye ameonekana kuwa mwiba kwa CCM, aliitaja Wilaya ya Nzega kuwa ni moja ya wilaya iliyokwisha anza kutekeleza maagizo hayo.

  Dk Slaa alilalamika kuwa kitendo cha wakuu wa wilaya kutumia vyombo vya serikali na ofisi zao ni aina nyingine ya ufisadi unaotumia fedha za umma.

  “Wakuu wa wilaya kutumia vyombo vya serikali pamoja na nyaraka zake ni aina nyingine ya ufisadi unaotumia fedha za umma,” alisema Dk Slaa

  Dk Slaa alisema kitendo cha watumishi wa umma kutumia ofisi na vyombo vya serikali kwa ajili ya chama ni kinyume na maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  “ Maadili ya Nec hayaruhusu mtumishi wa umma yoyote kutumia nyaraka za serikali katika masuala yanayohusu chama,” alisema Dk Slaa.
  Chanzo: Mwananchi
   
 2. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ni ngumu sana kwa Nchi hii kuwatenganisha viongozi wa Serikali/Umma na shughuli za CCM
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  another ujambazi wa chama cha majambazi.iko siku atakula kwao mazima.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Hapana, nchi nyingine zote zilizoendelea hazichanganyi mambo ya chama na yale ya serikali. Kwa Marekani iwapo Rais anataka kwenda kwenye mambo ya Chama chake, basi chama kinatakiwa kiilipe hazina gharama za rais kutumia ndege ya serikali Air Force One kwenye shughuli hizo.
   
 5. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Shame on you Mkuu wa Wilaya Nzega, somebdoy Horombe; anashirikiana na afisa biashara wa wilaya kukusanya wafanyabiashara wote wa nzega na kuwaeleza wamchangine JK kima cha chini 200k. Nimemwambia meneja wangu na yeye kwa ujumbe mfupi kuwa NAMSUBIRI MGOMBEA WA CHADEMA ndo hiar yangu ya kuchangia. Anatumia muda ya kazi, ofisi ya UDC, simu za serikali kukusanya pesa za kampeni za JK?

  Shame on you MAMA na sihitaji na wala sijawahi kulazimisha kufanya biashara na CCM wala serikali. Nimejiandaaa na nitasimama bila serikali onevu na ya vitisho.
   
Loading...