Dk. Slaa aanza kuimarisha CHADEMA Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa aanza kuimarisha CHADEMA Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jun 19, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameanza ziara ya ujenzi na kukagua uhai wa chama kwa mkoa wa Dar es Salaam.

  Katika ziara hiyo ya siku nane kuanzia juzi Juni 17, mwaka huu, Dk. Slaa amekutana na ataendelea kukutana na viongozi wa wilaya na majimbo ya mkoa huo katika vikao vya ndani.

  Taarifa ya Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, kwa vyombo vya haabri jana, ilisema kuwa ziara hiyo wa Dar es Salaam ni mwendelezo wa majukumu yake kama mtendaji mkuu wa chama ambayo amekuwa akiyafanya katika mikoa mbalimbali.

  Katika ziara hiyo, Dk. Slaa atatoa maelekezo kwa viongozi hao wa wilaya na majimbo namna ya kuendelea kuwafikia wananchi katika ngazi hizo na kuendelea kukipanua chama kwa ajili ya kukidhi mahitaji na matumaini ya watu wengi.

  Source:
  Tanzania Daima
   
 2. h

  hans79 JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Njema ila ajitahidi kutembea kila mkoa, lengo ni kujua zile sehemu zenye migogoro ya kiuongozi.
   
Loading...