Dk. Shein Ziarani Nchini Viietnam

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=2]Wednesday, November 21, 2012[/h][h=3][/h]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,pamoja na Viongozi wengine wa Vyama na Serikali,katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo,akielekea Nchini Vietnam kwa ziara rasmi ya Kiserikali,katika ziara hiyo Rais amefuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Mawaziri na Maofisa mbali mbali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,pamoja na Viongozi wengine wa Vyama na Serikali,katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo,akielekea Nchini Vietnam kwa ziara rasmi ya Kiserikali,

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiagana na wazee wa chama na Maofisa mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi,katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,akielekea Nchini Vietnam kwa ziara rasmi ya Kiserikali,katika ziara hiyo Rais amefuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Mawaziri na Maofisa mbali mbali.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]




STATE HOUSE ZANZIBAROFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE

Zanzibar 21.11.2012


Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein ameondoka nchini leo kuelekea nchini Vietnam kwa ziara ya Kiserikali kufuatia mualiko rasmi wa kiongozi wa nchi hiyo.


Katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, Dk. Shein aliagwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd pamoja na viongozi wengineo wa vyama na Serikali.


Katika safari hiyo ya wiki moja Dk. Shein amefuatana na mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na viongozi wengine wa Serikali akiwemo Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe. Suleiman Othman Nyanga, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdillah Jihad Hassan.


Viongozi wengine ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Mhe. Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi Juma Maalim, Mshauri wa Rais, Ushirikiano wa Kimataifa na Uwekezaji Balozi Ramia Abdiwawa pamoja na Maafisa wengine wa Serikali.



Katika ziara yake hiyo, Dk. Shein anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tan Sang, Pia, atazungumza na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa nchi hiyo.


Aidha, Dk. Shein atazugumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenyeviwanda na Wawekezaji wa nchi hiyo.


Dk. Shein kabla ya kufanya mazungumzo hayo mapema anatarajiwa kuanza kuweka shada la maua katika makaburi ya mashujaa na kisha ataelekea katika jumba la rais wa nchi hiyo kwa makaribisho rasmi.


Pamoja na hayo, Dk. Shein anatarajiwa kufanya mazungumzo na vyombo vya habari ambayo yatafanyika mara baada ya Mhe. Dk. Shein kumaliza mazungumzo na mwenyeji wake rais wa nchi hiyo.


Pamoja na hayo, Dk. Shein atatembelea shughuli mbali mbali za maendeleo katika nchi hiyo yakiwemo maeneo ya kilimo, uvuvi, ufugaji pamoja na kuangalia shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi.





Imewekwa na MAPARA at 2:52 PM
 
Back
Top Bottom