Dk Shein atajwa kujitosa kinyang'anyiro cha urais Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Shein atajwa kujitosa kinyang'anyiro cha urais Zanzibar

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jun 9, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Makamu wa Rais Dk Ali Mohammed Shein ambaye jina lake linatajwa kuwa ni miongoni mwa wagombea wa urais Zanzibar

  Salma Said, Zanzibar na Boniface Meena

  MAKAMU wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein ametajwa kuwa ni mmoja wa wanachama wa CCM wanaotarajiwa kuchukua fomu za kuwania urais Zanzibar Juni 21 mwaka huu.Kwa muda mrefu, Dk Shein amekuwa akiombwa na rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume achukue fomu ya kuwania nafasi hiyo kubwa ya kisiasa visiwani humo. Rais Karume anamaliza vipindi vyake viwili vya urais mwaka huu baada ya kuingia Ikulu mwaka 1995.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijini Dar es salaam na Zanzibar, Dk Shein alikuwepo visiwani humo na kufanya mazungumzo maalumu na Rais Karume na habari zinasema kuwa kiongozi huyo wa Zanzibar alimuomba Dk Shein kukubali kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo moto.


  Hamu ya Rais Karume kumtaka Dk Shein kuwa mrithi wake inatokana na makamu huyo wa rais kuonekana ana msimamo wa wastani katika siasa za Zanzibar zisizo na chuki za Upemba na Unguja, huku akionekana kuwa hana makundi kulinganisha na wagombea wengine.


  Sababu nyingine ni Dk Shein kuonyesha dhamira ya kutaka kuendeleza maridhiano yaliyofikiwa Novemba 5 mwaka jana kati ya Rais Karume na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

  Hata hivyo, msemaji wa makamu wa rais, Said Ameir alisema hajui lolote kuhusu taarifa hizo kwa kuwa yuko likizo.

  "Hakuna taarifa kama hizo. Mimi niko likizo na sijui lolote kuhusu hilo... kama mmepata taarifa na mnataka kushirikisha watu sawa, lakini sijui lolote," alisema Ameir.


  Mwandishi wa habari wa makamu wa rais, Penzi Nyamungumi alisema hajawahi kusikia hilo kwa kuwa hata Dk Shein mwenyewe hajawahi kutamka lolote kuhusu hilo.


  "Sijui lolote ndio nasikia kutoka kwako; sina uhakika na hilo kwa kuwa makamu wa rais hajawahi kutamka kuhusu urais wa Zanzibar," alisema Nyamungumi.


  Lakini chanzo chetu kimesema awali, Dk Shein alikuwa mgumu kukubali ombi la Rais Karume kutokana na wana CCM wahafidhina wanaotoa salamu za chuki dhidi ya wana CCM wenye asili ya Pemba wanaowatishia kwamba kamwe wasijaribu kugusa fomu za kuwania urais.


  "Kwanza Dk Shein alisita kwa sababu anawajua vizuri wana-CCM wenzake hasa hawa wa Zanzibar ambao wanajifanya wao ndio wana mapinduzi na wao ndio wenye haki ya kuchukua fomu. Wanataka watu kutoka Pemba wasijaribu kuchukua fomu na wameanza kutoa vitisho kwa hiyo kama mnavyomjua dokta huwa hapendi mazonge.


  Amekuwa na hofu kwa sababu anataka heshima yake ibaki, lakini baada ya kuelezwa mengi amekubali na inshaallah tutamshindikiza akachukue fomu," kilisema chanzo chatu.


  Kujitokeza kwa Dk Shein kunaelezwa kupata baraka zote za Rais Karume na baadhi ya viongozi wengine wa serikali ya Zanzibar na ile Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  "Mtu ambaye hana upande hadi sasa kati ya wanaotaka kuwania urais wa Zanzibar ni Dk Shein; kwanza anaweza kufanya kazi na mtu yeyote, hana chuki na watu na tabia yake ya upole inachangia kuonyesha uadilifu wake.


  ''Katika suala la maridhiano anaonyesha kuliunga mkono tofauti na wenzake ambao wanasema wazi wazi kupitia wapambe wao kwamba wakiingia watalitupilia mbali," kilieleza chanzo hicho.


  Kabla ya kuwa makamu wa rais, Dk Shein aliwahi kuwania uwakilishi wa jimbo la Mkanyageni mwaka 2000 kisiwani Pemba Kijiji ambacho amezaliwa. Kiti hicho kinashikiliwa na mwakilishi wa CUF Haji Faki Shaali.


  Kuingia kwa Dk Shein katika kinyanganyiro cha urais wa Zanzibar kutasababisha mfadhaiko kwa baadhi ya watu wanaotaka kuwania nafasi hiyo kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na rekodi zake za uadilifu na nidhamu ndani ya chama kikongwe cha CCM.


  Pia kutaibua changamnoto mpya kwenye siasa za Zanzibar ambako tayari wanachama wa CCM wameshaanza kupigana vijembe kuhusu nia ya baadhi yao kuwania urais. Katika siasa za Zanzibar, watu kutoka Pemba wamekuwa wakilaumu ndani ya CCM kuwa wanabaguliwa.


  Hata hivyo, baadhi ya viongozi wanaotaka kuwania kinyanyanyiro cha urais wa Zanzibar wameelezwa kutaka kumuunga mkono Dk Shein iwapo atatangaza nia yake ya kutaka kuchukua fomu ya kuwania urais wa Zanzibar.


  Viongozi hao wameelezwa kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mambo ya Muungano, Mohammed Seif Khatib anayetokea Bambi Unguja na Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud Mohamamed ambaye anatokea Wawi Kisiwani Pemba.


  Wengine wanaotajwa kutaka kuwania urais wa Zanzibar ni Dk Mohamed Gharib Bilal ambaye aliwahi kuwa waziri kiongozi wa SMZ kipindi cha utawala wa Dk Salmin Amour Juma.


  Wengine wanaoelezwa kuwa wanataka nafasi hiyo ni Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Karume, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman na Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna.


  Takriban wajumbe wote wanaotajwa kutaka kuingia katika kinyang'anyiro hicho hawajaeleza waziwazi nia zao, lakini kila mmoja alisema ikifika wakati atatangaza na baadhi yao wamesema wiki ijayo watatangaza nia zao za kutaka kuchukua fomu muda utakapofika.


  Wakati hayo yakitarajiwa kufanyika wiki ijayo, tayari CCM imewataka watendaji wake, wakiwemo makatibu wa itikadi na uenezi kutenda haki kwa wagombea wote watakaojitokeza katika zoezi hilo pamoja na ubunge na uwakilishi katika kura ya maoni na kuacha tabia ya kuwabeba wagombea.


  Akizungumza katika mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa chama, katibu wa idara ya itikadi na uenezi ya kamati maalumu ya halmashauri kuu ya CCM upande wa Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema sio busara kwa sasa watendaji hao kuwabeba wagombea kabla ya kutangaza nia zao na kuwataka kujiepushe na vitendo vya kupokea au kutoa rushwa.


  Dk Shein atajwa kujitosa kinyang'anyiro cha urais Zanzibar
   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  haiwezi mikikimikiki ya kule huyu..polite sana. kule yataka mbabe
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hapa sijui error ni ya nani kati ya muanzisha mada au mwandishi. Lakini Karume kaingia madarakani mwaka 2000.
   
 4. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusubiri huo muda wa kutangaza nia na kuchukua fomu.
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  maanake naona hata nyumbani kwake papo RAHISI SANA!....
  au ndo ''mjanja kuliko wenzie??..'' i mean haintatein ''SHOW-OFF''
   

  Attached Files:

 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  maanake naona hata nyumbani kwake papo RAHISI SANA!....
  au ndo ''mjanja kuliko wenzie??..'' i mean haintatein ''SHOW-OFF''

  View attachment 10929
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  :A S tongue::A S tongue::A S tongue:
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nadhani yuko simple huyu. Ulishasikia skendo yake ya ufisadi au nyingine yeyote?
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  lakini saa ingine huenda kawazidi wenzie ''akili''...
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yaani anakula kwa ustaarabu? Anything is possible, but still we could have heard something.
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  au anajua ''kula na vipofu?''....
  lakini mi naona kama MSAFI FULANI HIVI
   
 12. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mi nadhani huyu mzee apumzike awachie wengine kwani ki protocal VP ni mkubwa kwa rais wa Z.bar
   
 13. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  In short Mpemba dini imemkaa hana makuu..
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kama zile hadithi kuhusu mtandao zilikuwa kweli, Dr Shein sio chagua la JK! So, inawezekana pia ni njia ya kumtoa kwenye nafasi hiyo ya VP ili mtandao waweke 'mtu wao'.
   
 15. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  uonevu mwingine...kwanini wamtese ivyo jamaa? hawamwonei huruma?
   
 16. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Inaonyesha jinsi gani tulivyo corrupt sisi wenyewe kiasi kwamba ni vigumu kuamini kuwa wapo waliopo katika nafasi lakini wasiwe corrupt....chughulieni zaidi wapo ingawa wanazidiwa nguvu na vishawishi ikiwemo kutoka kwa "wapiga kura" na wanafamilia, ndugu, jamaa, marafiki na wapambe...

  Kuna kijana mwenzangu aliniambia kuwa huyu jamaa hafai kuwa kiongozi (rais znz) kwa kuwa ameshindwa kuwa hata na gari lake binafsi na hana makundi. Kwa kweli niliinshiwa nguvu na hoja hiyo...

  omarilyas
   
 17. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ebwana huyu jamaa hata ukimwangalia wife wake yupo sipo tu.
  Inawezekana ni 'mswafi'
   
 18. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1) Sikuwahi kujua mkapa fisadi mpaka alipotoka ikulu
  2) Usikijaji kitabu kupitia kava
  3) Yote yawezekana chini ya jua (kuwa fisadi na kutokuwa fisadi)

  mix with yours
   
 19. W

  WaMzizima Senior Member

  #19
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katika viongozi wa juu hapa Tz ambae anaoneka hana makuu ni huyu jamaa, sijasikia madudu kwake na vilevile ni mtu muungwana sana ukikutana nae. Ana unyenyekevu bila ubabe na nafikiri Znb hata Tz kwa ujumla inahitaji kiongozi ambae ni mnyenyekevu asie na ubabe ambae atakuwa tayari kusikiliza hoja za pande zote na kutoa maamuzi ya busara.

  Sasa hivi katika siasa za hapa kwetu na zaidi ndani ya CCM huyu bwana ni mmoja wa watu wachache (labda na Pinda kwa kiasi fulani)ambae anaheshimika na watu wengi na anajulikana kuwa hana makundi. Hivyo mi namshabikia huyu kwa unyenyekevu na ustaarabu wake. Labda kama kuna mtu ana madudu yake aweke wazi ama sivyo ni kweli bora aongoze dola maana ofisi ya makamu wa rais haina meno.
   
 20. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu nadhani ni daktari wa kusomea kwaiyo ni kichwa. siyo hawa wenye vichwa mbofu mbofu wanaotuongoza ambao vichwa vyao havihitajiki nchi nyingine. Jaribu kufanya research watu wenye elimu ya kuunga unga wakipewa nafasi na hawa wazuri darasani utaona utofauti.
   
Loading...