rreporter2010
Member
- Nov 7, 2010
- 34
- 1
RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, amemteua Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa
Maalim Seif amewahi kushika nyadhifa mbali mbali kabla ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Miongoni mwa nyadhifa hizo ni Waziri Kiongozi na Waziri wa Elimu, ambapo pia aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Mipango na Uchumi ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM.