Dk Rwaya Saud Al Busaid waziri wa elimu Oman ni kitukuu cha Tip Tippu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
15,685
2,000
Monday, 2 January 2017
DR. RAWYA SAUD AL BUSAID KITUKUU CHA TIP TIP

Utangulizi

Kila unapoitafiti historia ya Zanzibar ndipo inapozidi kukushangaza na kukustaajabisha khasa katika muingiliano wa Zanzibar na Oman na udugu uliojengeka kwa miaka isiyo na hesabu. Rais mmoja wa Tanzania akiwa Unguja kwenye mkutano wa hadhara kama ilivyo ada ili kunogesha hotuba yake na kuwafurahisha wanamapinduzi alitoa maneno ya kuwakashisifu, ''Waarabu wa Omani.'' Akisema huku shingo ametoa kuwa waliopinduliwa wamsikie anachosema.

Ghafla nyuma yake walipokaa waheshimiwa wote wa serikali Chama Cha Mapinduzi na Memba wa Baraza la Mapinduzi wengi wakawa wamejiinamia wameshika vichwa kwa fadhaa. Wamefadhaika kwa kuwa maneno yale yalikuwa moja kwa moja yawamagusa wazazi wote, babu, baba mama waliotangulia mbele ya haki na kwa kwengine wakwe zao ambao kwa hakika wana asili ya Oman wala hili halina shaka kwani ukiwatazama tu wanaonyesha kuwa wamechanganya damu. Hotuba ile haikuwa muafaka kwa wakati huu kwani mengi yalikuwa yamepita. Watoto wa mahasimu walikuwa kwengine mke na mume na walikuwa jukwaani katika orodha ya waheshimiwa sana wakimsikiliza Rais akihutubia akiwakejeli wazee wao waliowazaa na kuwaleta duniani lakini kwa rehma za Allah ingawa wazee wao walikuwa ‘’maadui,’’ wao wakaja kuwa wapenzi kiasi cha kuoana na kujenga familia. Leo wako katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama viongozi wakuu na wake zao wake wa viongozi. Hawa hawakuwa tena ‘’maadui wa mapinduzi.’’ Hawa sasa ni ni wakwe, mababu na mabibi wa watoto zao majumbani na wazazi hawa wanafanya juhudi kubwa sana kuwakinga watoto wao na historia ya kuhuzunisha kuwa babu zao kiumeni na kikeni walikuwa maadui wa kufikia ukomo wa kutoana roho. Iweje leo Rais wa Tanzania awe jukwaani anakwangua makovu yaliyokuwa yamepona na kuanza kusahaulika kwa koo zilizokuwa hasimu watoto wao kuoana na Allah kujaalia wajukuu watakaounda Zanzibar mpya ijayo?

Kwenye chakula cha jioni Ikulu mmoja wa waheshimiwa akamnong'oneza Rais kwa kumwambia kuwa katika hotuba yake mchana kamuumiza sana mwenzake na kumtia fadhaa ''First Lady,'' kwani vijembe vile vimewahusu baadhi ya wazazi wa viongozi wa juu katika serikali ya mapinduzi. Rais akadai maelezo. Alipoelezwa zile nasaba aliinamisha kichwa aliponyanyua kichwa chake juu alisema kwa Kiingereza, ''I will never come to understand you Zanzibaris.''

Mheshiwa akamwambia Rais, ‘’Shida yenu nyie watu wa Bara hamtaki kabisa kutujua wala kuijua historia yetu. Sisi sote hapa utuonavyo ni ndugu.’’
Angalia nasaba ya Waziri wa Elimu wa Oman Dr. Rawya Saud Al Busaid hapo chini kama iliyoelezwa na Ummie Mahfoudha Alley Hamid ambae yeye mwenyewe ni kitukuu cha Tip Tip:

img_8090.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Waziri wa Elimu ya Juu wa Nchini Oman, Dk.Rawya Saud Al Busaid, Ikulu Mjini Zanzibar

img_8057.jpg

Dr. Rawya Albusaidy ni kitukuu cha Tip Tip. Mama yake Marhuma Bi Samira ni mjukuu wa Tip Tip. aliyezaliwa na Marhum Nassor Lamky mtoto wa Marhuma Fatma bint Hamed Bin Mohammed bin Juma Almarjeby (TipTip).
 
KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,525
2,000
Uchambuzi mzuri sana Sheikh Said ingawa umelihifadhi jina la aliyetamka maneno yaliyoleta ukakasi kwa ndugu zetu wa Zanzibar. Ni kweli inakuwa vigumu sana kutofautisha Wanzazibari na watu wa Oman. Wamekuwa na historia ya maingiliano kwa muda mrefu.
 
Kwezisho nawaiga watunga mashairi wao hupenda kufumba tungo ili msomaji mwenyewe afumbue...
 
Az 89

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
1,661
2,000
Al Akhy...utaniwia radhi, kwanini bwana Tip Tip aliitwa jina hilo( Tip tip)?.
 
authentic

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
661
250
Monday, 2 January 2017
DR. RAWYA SAUD AL BUSAID KITUKUU CHA TIP TIP

Utangulizi

Kila unapoitafiti historia ya Zanzibar ndipo inapozidi kukushangaza na kukustaajabisha khasa katika muingiliano wa Zanzibar na Oman na udugu uliojengeka kwa miaka isiyo na hesabu. Rais mmoja wa Tanzania akiwa Unguja kwenye mkutano wa hadhara kama ilivyo ada ili kunogesha hotuba yake na kuwafurahisha wanamapinduzi alitoa maneno ya kuwakashisifu, ''Waarabu wa Omani.'' Akisema huku shingo ametoa kuwa waliopinduliwa wamsikie anachosema.

Ghafla nyuma yake walipokaa waheshimiwa wote wa serikali Chama Cha Mapinduzi na Memba wa Baraza la Mapinduzi wengi wakawa wamejiinamia wameshika vichwa kwa fadhaa. Wamefadhaika kwa kuwa maneno yale yalikuwa moja kwa moja yawamagusa wazazi wote, babu, baba mama waliotangulia mbele ya haki na kwa kwengine wakwe zao ambao kwa hakika wana asili ya Oman wala hili halina shaka kwani ukiwatazama tu wanaonyesha kuwa wamechanganya damu. Hotuba ile haikuwa muafaka kwa wakati huu kwani mengi yalikuwa yamepita. Watoto wa mahasimu walikuwa kwengine mke na mume na walikuwa jukwaani katika orodha ya waheshimiwa sana wakimsikiliza Rais akihutubia akiwakejeli wazee wao waliowazaa na kuwaleta duniani lakini kwa rehma za Allah ingawa wazee wao walikuwa ‘’maadui,’’ wao wakaja kuwa wapenzi kiasi cha kuoana na kujenga familia. Leo wako katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama viongozi wakuu na wake zao wake wa viongozi. Hawa hawakuwa tena ‘’maadui wa mapinduzi.’’ Hawa sasa ni ni wakwe, mababu na mabibi wa watoto zao majumbani na wazazi hawa wanafanya juhudi kubwa sana kuwakinga watoto wao na historia ya kuhuzunisha kuwa babu zao kiumeni na kikeni walikuwa maadui wa kufikia ukomo wa kutoana roho. Iweje leo Rais wa Tanzania awe jukwaani anakwangua makovu yaliyokuwa yamepona na kuanza kusahaulika kwa koo zilizokuwa hasimu watoto wao kuoana na Allah kujaalia wajukuu watakaounda Zanzibar mpya ijayo?

Kwenye chakula cha jioni Ikulu mmoja wa waheshimiwa akamnong'oneza Rais kwa kumwambia kuwa katika hotuba yake mchana kamuumiza sana mwenzake na kumtia fadhaa ''First Lady,'' kwani vijembe vile vimewahusu baadhi ya wazazi wa viongozi wa juu katika serikali ya mapinduzi. Rais akadai maelezo. Alipoelezwa zile nasaba aliinamisha kichwa aliponyanyua kichwa chake juu alisema kwa Kiingereza, ''I will never come to understand you Zanzibaris.''

Mheshiwa akamwambia Rais, ‘’Shida yenu nyie watu wa Bara hamtaki kabisa kutujua wala kuijua historia yetu. Sisi sote hapa utuonavyo ni ndugu.’’
Angalia nasaba ya Waziri wa Elimu wa Oman Dr. Rawya Saud Al Busaid hapo chini kama iliyoelezwa na Ummie Mahfoudha Alley Hamid ambae yeye mwenyewe ni kitukuu cha Tip Tip:

img_8090.jpg

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Waziri wa Elimu ya Juu wa Nchini Oman, Dk.Rawya Saud Al Busaid, Ikulu Mjini Zanzibar

https://zanzibariyetu.files.wordp
ress.com/2015/01/img_8057.jpg

Dr. Rawya Albusaidy ni kitukuu cha Tip Tip. Mama yake Marhuma Bi Samira ni mjukuu wa Tip Tip. aliyezaliwa na Marhum Nassor Lamky mtoto wa Marhuma Fatma bint Hamed Bin Mohammed bin Juma Almarjeby (TipTip).

Mzee wangu mohammedi saidi.

naomba historia watawala wa zanzbar katika picha kutoka wa kwanza hadi wa mwisho na miaka yao ya utawala.

nilipata kusoma mahala kutoka kwako nadhani ila imenipotea.

kama utanisaidia link pia litakua jambo jema.

huwa nakuafuatilia sana.

kuna siku siku ulifanya kipindi na Yule Abasi wa Radio kheri ulinikosha sana.
 
Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
6,013

namimi akikupatia naomba unitag
 
NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,970
2,000
shikamoo mzee wangu!
Samahani nikuulize hili swali kwa nia njema tu mzee wangu:
Eti nasikia wale Masultan waliofukuzwa kwenye mapinduzi ya Zanzibar miaka hiyo 1964 walikuwa wana undugu wa damu Maalim Sharif Seifu ndio maana wakati alivyokuwa waziri wa elimu huko ZNZ alifuta somo la historia ili watoto wasijue matendo ya babu zake?
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,445

:D:D:D uzuri wa historia yetu wakala wa mchuuza watumwa ndio anajulikana kwa kuua, kutesa na kuwapeleka utumwani!!! Tukijua historia ya manamba ilikuwaje tutajua pia biashara ya watumwa iliendaje!!!
 
lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,472
2,000
Aisee, una maana yule Tip Tippu aliyekuwa akisubiria mashua ya 'mzigo' wa watumwa pale Ujiji alafu wakati ikiwasili na ghafla ikaanza kuzama. Naye badala ya kusikitika kwamba watu walikuwa wanakufa machozi yakawa yanamtoka mara kuulizwa ndio anasema "ooooh, oooh, mashua yangu inazama". ...ndiye huyo unayemuongelea!?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom