Dk. Reginald Mengi: Waziri Muhongo ni muongo, takwimu zake za uongo pia!

Mkuu umeshawahi kulinganisha mishahara ya IPP na makampuni mengine?

Fanya utafit kwanza, angalia bakhreasa, na migodi na makampuni makubwa yapi yanalipa kodi vizuri.

Mengi ni mzalendo wa ukeli...
Go on go go go Menji

kama hunamaslahi na mengi huwezi kumtetea mengi ni fisadi ni bepari mbaya sana tumechoka na wizi wake sasa basi atuachie taifa letu.
 
Mimi nimefanya utafiti na ukweli ndio huo, Mengi analipa mishahara midogo sana na tena ni mkabila. Mimi nimejikita zaidi katika vyombo vya habari anavyomiliki, waandishi wengi wanaofanya kazi kwa Mengi mishahara yao ni duni huwezi kulinganisha na Mwananchi. Kingine nikufahamishe jina lake sio Menji ni Mengi na hilo jina alipewa kwasababu ni mpenda mengi, yani anatamaa ndio maana wakampachika hilo jina kwa tamaa zake ya kutaka kumiliki kila kitu huku akiwahadaa wananchi eti yeye yupo kwa maslahi ya wanyonge.

mkuu chukua like yangu.
 
1. Ningependa kutofautiana na Mhe. Profesa Muhongo na kusema kwamba adui wa maendeleo ya Watanzania siyo Watanzania wenyewe kama alivyosema ila ni Watanzania wachache sana wenye kauli za dharau za kutuambia kwamba Watanzania hatuwezi.

mkuu mlaumu mengi anayemiliki dar es salaamu tatu.
 
Naona Watu wanamshambulia Mzee Mengi. Napata taabu sana na uelewa wa Watu juu ya biashara. Biashara yake ina changamoto nyingi kama zilivyo biashara za wengine. Wala haiondoi uhalali wa hoja ushiriki wa wazawa kwenye mafuta na gesi.
 
yeye mbona anajiita 'Dr' wakati doctorate yake hatambuliki kokote duniani?

Kwenye kanusho lake linalodai Prof Mhongo ni Muongo Mengi amedai hivi:



"Ukweli ni kwamba mimi ninamiliki kwa ubia na Watanzania wenzangu mgodi mmoja wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite wenye eneo lisilofikia hata kilomita moja ya mraba na siyo Dar es Salaam 3 kama alivyosema."


Ujanja hapo ni kuwa ana-imply kwamba kamgodi hako ndio the only investment he has in the mining sector. Kwa taarifa zilizoko mtandaoni tu (kabla prof hajaleta za kwake za Dar x 3) zinathibitisha kuwa Mengi anaongea kisiasa siasa kwenye hili la 1sq.km.


"IPP Holding is highly diversified company with a focus in acquisition, exploration, development and mining. We have IPP Base Metals, IPP Gem Stones, IPP Industrial minerals, IPP Energy and IPP Gold,"
"The Bukwimba Gold prospect lies in the Kahama greenstone belt in the Lake Victoria gold field in NW Tanzania, it's 58km squared that has been explored by company Reef Golf Limited, a subsidiary company of IPP, since 2006"

"The Handeni gold project, another one of the leading gold projects in which IPP has a majority share is located in the Tanga region, Handeni district of the Republic of Tanzania."
"We acquire mineral properties and assets that have high potential for success," Dr. Scheepers explains, "We then explore these, ensuring the owning of the mining interests, for example we have a majority % interest of Handeni. It's about ownership, following on up potential joint ventures, selling them to companies and then enjoying the benefit of royalty payments."

Source: IPP resources finding the gold

1. Handeni Gold Inc (OTC-QB: HNDI) (the "Company") is an emerging gold exploration company focused on exploring and developing gold mining opportunities in the Republic of Tanzania. The Company's principle area of focus is the 800 square kilometer Handeni Gold Project located in the Handeni district, within the Tanga region of the Republic of Tanzania.

2. The Mkuvia Alluvial Gold Project is comprised of four prospecting licenses covering a total area of 380 square kilometers and is located in the Nachingwea District, Lindi Region of the Republic of Tanzania.

Source: handeniGold.

Hata hapa JF ilishawahi kuja hii thread mwaka juzi!: Mengi IPP Gold strikes deal
"Douglas Lake Minerals Inc. (the "Company" or "Douglas Lake") (OTCBB:DLKM)(FRANKFURT:D60) is very pleased to announce that the Company has recently received approval from its Board of Directors to both enter into and immediately close upon the terms and conditions of a certain Mineral Property Acquisition Agreement (the "Acquisition Agreement"), with IPP Gold Ltd. ("IPP Gold"), to acquire a 100% interest in four prospecting licences (the "PLs"), totaling approximately 800 square kilometres, located in the Handeni District of Tanzania and which are owned or controlled by IPP Gold and its affiliates."

"..In accordance with the closing today of the Acquisition Agreement IPP Gold has now become a major stakeholder in the Company. Pursuant to the terms of the Acquisition Agreement the Company has now issued 133,333,333 restricted shares of common stock to IPP Gold in exchange for 100% interest in the four PLs of the new Handeni Project, with no further payments in shares or cash required."

Mpaka hapo tu kwa haraka haraka tayari ana km za mraba 1238. Na hapo bado hatujui zingine low profile. Je Nani muongo?
 
2. Katika suala la gesi mimi sipiganii mambo yangu binafsi, kwa sababu mimi nimeshafanikiwa kibiashara. Ninachopigania ni Watanzania wenzangu nao wapate fursa. Naomba nieleweke kwamba ninaposema Watanzania nina maana kuanzia yule mfanyabiashara mdogo wa sekta isyo rasmi, mfanyabiashara wa kati na wafanyabiashara wakubwa. Nataka kuwepo sera ambayo itahakikisha kwamba wanawezeshwa na siyo kusema tu kwamba hawawezi. Nafanya hivyo kwa sababu ninaamini kwamba utajiri uliobarikiwa ni ule uliopatikana kwa njia halali na unatumika kusaidia wanaohitaji msaada.

No vigumu kuwapata watu wenye upeo wa kufikiri kama wewe.Nakuunga mkono kwa sehemu hii....Tunachozungumzia hapa ni mtanzania mwenzetu kupata nafasi ya kuinvest katika rasilimali ya ardhi yake.
Kuwa professa sio kwamba kila kitu upo sahii hapana.
Prof. Muhongo si Muongo mbinafsi anayetaka kuutumia uproffessa wake kama ngao ya kumdemise mengi.
Namkubali Mengi hata kama amenizidi saaaaaaaaaaaana kipato lakini ni mtanzania pekee anayejituma kuinvest katika ardhi yake.

Kuna mtu kasema hapa kwamba eti mengi anatoa mishahara midogo kwa waajiri wake,Je mbona hatujiulizi kuhusu ajira alizowapa watz kutokana na ivestment alizonazo?
 
mengi mwizi ata mtoto mchanga hawezi kuamini maneno yake ya kwamba robo ya tanzania imegaiwa vtalu mengi muongo huyu fsad tu
 
mbona lile kongamano la tarehe 8 Desemba 2013,,hakulionyesha kwenye TAARIFA YA HABARI KAMA ANAVYOPENDA KUJIPA MDA WAKUTOSHA KUUZA SURA,,,AU KWAKUA PRO ALISEMA UKWELI,,,KUWA ANAMILIKI DAR 3,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mimi binafsi sipo tayari kutetewe na mengi kuhusu swala la gesi kama anavyosema kuwa anatetea watanzania wote,,mimi sitaki kabisa,,nasema sitaki kabisa anihusushe na mambo yavitalu,,nasema sitaki,,watetee watanzania wengine lakini sio mimi,pleeeeeeeeeeeeeeas
 
Hivi Mengi hajui kama vitalu vya gesi vinamilikiwa 100% na Watanzania na hao wageni wanapewa leseni tu za exploration na itapopatikana gas 65% ni mali ya Watanzania na wawekezaji ni 35% tu.

Kama hayajui hayo basi ni mburula wa kutupwa na kama anayajuwa hayo basi ni mpotoshaji wa hali ya juu.
 
kama hunamaslahi na mengi huwezi kumtetea mengi ni fisadi ni bepari mbaya sana tumechoka na wizi wake sasa basi atuachie taifa letu.

Hacha porojo na wivu wa kutoshirikisga elimu,tupe facts za ufisadi na wizi wa Mengi,vyombo vya sheria mbona havimchukulii hatua?hacha kujifariji kwa wivu na vitu unavyojua havina ukweli!kuhusu kua bepari hizo ni jitihada za matunda yake,ametumia elimu yake vizuri ikamkomboa yeye na jamii ya Watanzania,wewe utabaki kujifariji kwa porojo na wivu tu wakati umri unakwenda na hauna mafanikio kielimu na hata kimaisha
 
Prof Muhongo ni uzao wa mafisadi MaCCM, hivyo ndivyo walivyo hawajali Watanzania wazawa!!
Kwani boss wake alisemaje, kwa nini amsahihishe??
Hizi rasilimali zote ni za Watanzania woote kwa nini wazawa wabaguliwe??
 
Hizi nazo ni stori za Abunwasi, toka lini Mengi ukawa na nia thabiti ya kusaidia watanzania? Hapa ni maslahi binafsi yanatafutwa kwa kutaka support kutoka kwa Watanzania ili maslahi hayo yatimie.

.

Tatizo lako best kubwa sana, dhan yako inukutuma umasiki ndo uzalendo halisi.

. Kingine nikufahamishe jina lake sio Menji ni Mengi na hilo jina alipewa kwasababu ni mpenda mengi, yani anatamaa ndio maana wakampachika hilo jina kwa tamaa zake ya kutaka kumiliki kila kitu huku akiwahadaa wananchi eti yeye yupo kwa maslahi ya wanyonge.

Njia ya mwongo ni fupi, ona unvyochanganya mambo
 
Mengi ni bepari tu hana lolote. Na pia tunaomjua Prof. Muhongo tunafaham kabisa jinsi alivyo chizi. Hata ndugu zake takribani wote hapatani nao.
 
Huyu mzee anafikiri gesi ni sawa na biashara ya soda. Hiyo hela ya nyanya akae nayo ale vizuri tu.anaingia na gia ya uzawa wakati ameambiwa kuwa kama anaweza masharti ajitose. Mpuuzi sana huyu jamaa. Umefika wakati anyamazishwe sasa.
 
Dr. Mengi songa mbele Watanzania tunakuelewa huyo muongo tunajua moja moja anamtetea aliemchagua lakini ilo halitakiwi kutakatisha tamaa Watanzania tunaelewa kinachoendelea hao tutawaonesha kwamba hii nchi ni ya wote kwenye sanduku la kura mapema 2015.
Kila siku wanaenda Norway kujifunza sijui hawaoni ni kiasi gani wazawa walivyoneemeka na rasilimali zao.
 
Kwa Tanzania mshahara mzuri ni upi kwani hata Serikali yenyewe hailipi mshahara mzuri na hata huo ambao sio mzuri hailipi kwa wakati stahili, Kwenye suala la kodi naamini TRA ndiyo mamlaka husika kwenye masuala hayo na kama inajiaminisha kuwa makampuni yanayomilikiwa na Bw. Mengi na wengineo hayalipi kodi kama inavyotakiwa basi kwayo wanazo sheria za kupambana na kudhibiti jambo hilo,

Kwa kauli ya Bw. Mengi ni ukweli usiopingika kuwa watawala wetu wamejawa jeuri, kiburi na dharau isiyoendana kabisa na majukumu ama dhamana waliyopewa kwa minajili ya kuitumikia jamii.

Kwa nini hamumuombi muambatane naye aonyeshe vitalu vyake?????
 
Wakuu naomba kuelimishwa. Jana nimeenda kununua mtungi wa gesi ya kupikia hapa Moro nikakuta ni sh 65,000 instead of 52,000 ya awali. Huyu Prof kila siku anaimba tumegundua matrilioni ya mita za ujazo za gesi, je hii gesi mbona haiwi processed na kuwekwa kwenye mitungi ili kupunguza bei?? sijasikia kabisa mikakati inayohusiana na hili, hata gesi ya songosongo toka imeanza kutumika sijasikia mikakati hii.
 
Back
Top Bottom