Dk. Reginald Mengi: Waziri Muhongo ni muongo, takwimu zake za uongo pia!

Geeky

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Messages
307
Points
195

Geeky

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2013
307 195

TAARIFA YA DKT. REGINALD A. MENGI MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 20 DESEMBA 2013

Baada ya Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ((TNBC) uliofanyika tarehe 16 Desemba 2013, chini ya uenyekiti wa Mhe. Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, sikutegemea kwamba Mhe. Profesa Muhongo angeendeleza mashambulizi dhidi yangu kwa sababu katika mkutano huo ambao ulikuwa na mafanikio makubwa tulifikia maamuzi ya kudumisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kitu ambacho nimekuwa nikipigania. Hivyo basi, kauli ambazo Mhe. Profesa Muhongo amezitoa Bungeni tarehe 19 Desemba 2013, zimenishtua na kunisikitisha sana.

Ningependa kuwaeleza Watanzania wenzangu yafuatayo.

Profesa Muhongo ni muongo

Imefika wakati wa Watanzania kubaini kwamba Mhe. Profesa Muhongo ni mtu mwenye hulka ya kusema uongo. Kwa mfano:

1. Kwenye kongamano la tarehe 8 Desemba 2013, Mhe. Profesa Muhongo alisema kwamba moja ya kazi yake, alipokuwa akifanya kazi kama mwanasayansi huko nje, ilikuwa kutabiri umuhimu wa sayansi katika uchumi wa dunia miaka 3,000 ijayo. Huu ni uongo wa mchana kweupe.

2. Mnamo Julai 2012 Mhe. Profesa Muhongo aliwaahidi Watanzania kwamba hakutakuwa na mgawo wa umeme tena. Sote tunashuhudia mgao wa umeme ukiendelea hadi sasa.

3. Mnamo mwezi Septemba 2012, Mhe. Profesa Muhongo alinukuliwa akizungumzia mikataba ianayohusiana na vitalu vya gesi akisema kwamba "baadhi ya mikataba ni ya ovyo, na inahitaji kuvunjwa" na "sitovumilia mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi na inawanufaisha wachache". Baada ya hapo, Mhe. Profesa Muhongo aliamrisha Bodi mpya ya TPDC kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi uliopangwa kufanyika mwezi huo na kupitia upya mikataba yote iliyokuwepo awali. Sasa zaidi ya mwaka umepita na Mhe. Profesa Muhongo hajarekebisha mkataba hata mmoja.

Profesa Muhongo na takwimu zake za maeneo ya madini

1. Tarehe 8 Desemba 2013, alipokuwa anajibu swali la Mhe. Tundu Lissu kuhusu ni nani anamiliki migodi ya Tanzania, Profesa Muhongo alitoa takwimu za kuonyesha kwamba mimi ninamiliki eneo kubwa mara tatu ya Dar es Salaam kupitia kampuni zangu tanzu.

2. Jumapili iliyopita mimi nilimjibu Mhe. Profesa Muhongo kwa kumueleza kwamba takwimu zake kuhusu mimi ni za uongo, na vilevile hizo alizotoa Bungeni pia ni za uongo na nilimweleza kwamba swali la Mhe. Tundu Lissu lilikuwa ni "nani anamiliki maeneo ya migodi".

3. Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa utafutaji madini (mineral prospecting) ndiyo msingi wa maendeleo ya sekta ya madini kwa sababu bila utafutaji hakuna ugunduzi na uendelezaji wa migodi hapa nchini. Lakini kuanzia Julai mwaka jana Waziri Muhongo alipandisha tozo za vitalu kwa asilimia kati ya 100 na 500. Matokeo yake Watanzania wengi wanarudisha leseni zao na kasi ya ugunduzi wa migodi imepungua.

4. Nia ya mtu inajionyesha siyo tu kwa yale anayosema lakini bali pia kwa yale anayoacha kusema. Sasa kama kweli nia ya Mhe. Profesa Muhongo ni nzuri, kwa nini hatoi takwimu zinazohusu gesi? Kwa mfano, kwa nini hawaambii Watanzania kwamba:

a. Eneo ambalo limeshatolewa kwa ajili ya mafuta na gesi lina ukubwa wa kilomita za mraba 243,000 ambalo ni sawa na karibu robo ya eneo la Tanzania nzima au mara 175 ya eneo la mkoa wa Dar es Salaam au eneo la mikoa 9 ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga na Kagera.

b. Kwa nini Mhe. Profesa Muhongo hataki kuwaambia Watanzania kwamba hakuna hata mzawa mmoja anayemiliki kitalu cha kutafuta au kuchimba mafuta na gesi?

c. Kwa nini Mhe Profesa Muhongo hataki kuweka wazi kwamba vitalu vyote 27 vya gesi ambavyo vinaanzia katika mpaka wetu na Kenya hadi mpaka wetu na Msumbiji, vimegawiwa kwa wageni? Je, kugawa vitalu vyote vya gesi kwa wageni siyo hatari kwa mustakabali wa usalama wa taifa letu?

d. Lakini cha muhimu ni kwamba Watanzania wafahamu kwamba gesi ambayo imeshagunduliwa Tanzania inakadiriwa kuwa na thamani ya US$ 500 bilioni wakati dhahabu yote iliyokwishagunduliwa hadi sasa na bado haijachimbwa inakadiriwa kuwa na thamani ya US$ 60 bilioni kwa bei ya sasa ya dhahabu.​

Kwanini Profesa Muhongo hawaambii Watanzania takwimu hizi?

Profesa Muhongo na kauli zake kwamba Watanzania hawawezi kushiriki katika mchakato wa mafuta na gesi

1. Mara nyingi tumesikia kauli za Mhe. Profesa Muhongo kwamba Watanzania hatuwezi kufanya biashara ya mafuta na gesi kwa sababu biashara hiyo inahitaji mtaji mkubwa na utaalamu, vitu ambavyo Watanzania hawana. Mhe. Profesa Muhongo amewahi kusema kwamba Watanzania ni wavivu wa kufikiri, wavivu wa kusoma na washamba sana katika masuala ya uwekezaji na kwamba uwezo walionao Watanzania ni kuuza juisi au soda. Huu ni uongo. Watanzania wanajua wanachokisema na gesi yetu ni mtaji mkubwa sana.

2. Kwanza kabisa katika karne ya 21 utalaamu ni bidhaa ambayo mtu asiye nayo anaweza kuinunua. Mhe. Profesa Muhongo anaweza asilifahamu hili kwa sababu yeye mwenyewe hajawahi kufanya biashara katika maisha yake – anayasoma masuala ya biashara kwenye makaratasi tu.

3. Namsihi Mhe. Profesa Muhongo akumbuke kwamba gesi ni mali ya Watanzania na wana haki ya kuzaliwa ya kumiliki rasilimali yao ya gesi.

4. Mhe. Profesa Muhongo anataka Watanzania waamini kwamba kuna mwekezaji wa nje anaweza kumiliki na kuendesha kitalu kwa fedha zake yeye mwenyewe. Hii si kweli. Fedha zinazotumika ni za watu wengi waliowekeza katika masoko ya hisa. Sisi pia tungehamasishwa na kuwezeshwa, tunaweza kuunganisha nguvu zetu hivyo hivyo na kuwekeza katika gesi yetu kwa kushirikiana na wageni. Mimi sipingi uwekezaji wa wageni. Watanzania nao washirikishwe katika umilikaji. Mgeni aje mwenyeji apone, siyo mgeni aje mwenyeji akose fursa ya kushiriki katika umiliki wa uchumi wake.

Profesa Muhongo hana nia nzuri kuhusu ushirikishwaji wa Watanzania katika gesi ?

1. Katika kongamano lilofanyika tarehe 8 Desemba 2013 Mhe. Profesa Muhongo alisema Watanzania wenye uwezo wa kifedha wazipeleke TPDC tarehe 10 Desemba 2013 na watapewa vitalu vya gesi. Vilevile alisema kwamba baada ya tarehe hiyo, hoja ya suala la wazawa kumiliki vitalu litafungwa. Watu waliokuwepo kwenye hilo kongamano walipigwa butwaa kwa sababu Profesa Muhongo alishanukuliwa akisema kwamba kwenye uongozi wake wazawa hawatapewa vitalu vya gesi na kwamba "suala la vitalu halina mambo ya uzawa".

2. Kwa kuzingatia kwamba maagizo ya Mhe. Profesa Muhongo yalikuwa ni batilii (huwezi kutangaza zabuni kwenye kongamano) wafanyabiashara wa Tanzania walimpuuza na hakuna hata mmoja aliyejitokeza. Lakini kikubwa zaidi ni kwamba haya mazingaombwe ya Mhe. Profesa Muhongo yalitufumbua macho Watanzania kung'amua kwamba kumbe kazi ya TPDC ni kupokea maagizo tu na anayegawa vitalu vya gesi ni Profesa Muhongo mwenyewe.

3. Nimekuwa nikirudia mara kwa mara kwamba mtaji sio tu fedha hata rasilimali kama gesi ni mtaji.

Hitimisho

1. Ningependa kutofautiana na Mhe. Profesa Muhongo na kusema kwamba adui wa maendeleo ya Watanzania siyo Watanzania wenyewe kama alivyosema ila ni Watanzania wachache sana wenye kauli za dharau za kutuambia kwamba Watanzania hatuwezi.

2. Katika suala la gesi mimi sipiganii mambo yangu binafsi, kwa sababu mimi nimeshafanikiwa kibiashara. Ninachopigania ni Watanzania wenzangu nao wapate fursa. Naomba nieleweke kwamba ninaposema Watanzania nina maana kuanzia yule mfanyabiashara mdogo wa sekta isyo rasmi, mfanyabiashara wa kati na wafanyabiashara wakubwa. Nataka kuwepo sera ambayo itahakikisha kwamba wanawezeshwa na siyo kusema tu kwamba hawawezi. Nafanya hivyo kwa sababu ninaamini kwamba utajiri uliobarikiwa ni ule uliopatikana kwa njia halali na unatumika kusaidia wanaohitaji msaada.

3. Ni wazi kwamba Mhe. Profesa Muhongo anachuki binafsi na mimi. Hii ni utashi wake, siyo lazima anipende na mimi siyo lazima nimpende. Lakini suala la gesi ni kubwa mno kuliko mahusiano kati ya Mhe. Profesa Muhongo na mimi – linagusa kila Mtanzania wa leo na wa vizazi vijavyo. Kwahiyo napenda kumsihi ndugu yangu Mhe. Profesa Muhongo aache kuchanganya chuki zake binafsi kwenye suala la gesi.

Dr. Reginald Mengi
Dar es Salaam

Disemba 20, 2013

Mpanzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2011
Messages
784
Points
225

Mpanzi

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2011
784 225
Aksante dr Mengi naamini ni Mtanzania wa kweli hata kama ana mapungufu lakini ni mara mia kuliko Pro Muongo
Hakuna popote duniani bepari akatetea maslahi ya wanyonge, angeanza kwanza kulipa mishahara mizuri kwenye makampuni yake pamoja na kulipa kodi stahiki
 
POMPO

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
6,690
Points
1,195

POMPO

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
6,690 1,195
Hakuna popote duniani bepari akatetea maslahi ya wanyonge, angeanza kwanza kulipa mishahara mizuri kwenye makampuni yake pamoja na kulipa kodi stahiki
Mkuu umeshawahi kulinganisha mishahara ya IPP na makampuni mengine?

Fanya utafit kwanza, angalia bakhreasa, na migodi na makampuni makubwa yapi yanalipa kodi vizuri.

Mengi ni mzalendo wa ukeli...
Go on go go go Menji
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Messages
8,410
Points
2,000

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2010
8,410 2,000
Mzee Mengi acha kubishana na kichaa, huyo Sospeter Muhongo amewehuka na tamaa za kukutana na hela nyingi uzeeni za rushwa ya vitalu vya gesi. Sospeter Muhongo hana consistence yoyote kwenye kauli zake, anarukaruka kama Mbulumundu, leo kaongea hiki na kesho kaongea hiki. Sijui Kikwete huwa anashauriwa na nani wakati anaokoteza watu kama Prof Muhongo. Ni wazi kuwa wasomi wa nchi hii ndio chanzo cha umaskini wa kutupwa wa taifa letu. Ukiwa na maprofesa 10 kama Muhongo kwenye serikali nchi haiwezi KUTAWALIKA. Muhongo ni hatari kwa usalama wa Taifa.
 
taffu69

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2007
Messages
2,088
Points
1,195

taffu69

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2007
2,088 1,195
Hakuna popote duniani bepari akatetea maslahi ya wanyonge, angeanza kwanza kulipa mishahara mizuri kwenye makampuni yake pamoja na kulipa kodi stahiki
Kwa Tanzania mshahara mzuri ni upi kwani hata Serikali yenyewe hailipi mshahara mzuri na hata huo ambao sio mzuri hailipi kwa wakati stahili, Kwenye suala la kodi naamini TRA ndiyo mamlaka husika kwenye masuala hayo na kama inajiaminisha kuwa makampuni yanayomilikiwa na Bw. Mengi na wengineo hayalipi kodi kama inavyotakiwa basi kwayo wanazo sheria za kupambana na kudhibiti jambo hilo,

Kwa kauli ya Bw. Mengi ni ukweli usiopingika kuwa watawala wetu wamejawa jeuri, kiburi na dharau isiyoendana kabisa na majukumu ama dhamana waliyopewa kwa minajili ya kuitumikia jamii.
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Messages
8,410
Points
2,000

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2010
8,410 2,000
Hakuna popote duniani bepari akatetea maslahi ya wanyonge, angeanza kwanza kulipa mishahara mizuri kwenye makampuni yake pamoja na kulipa kodi stahiki
Nyie ndio wale wale,, division five yako haiwezi kukujulisha kuwa Business is a separate entity from the owner

Upuuzi wa watanzania wengi ni kutoelewa maana ya private sector na mchango wake kwenye uchumi. As aspiring businessman watu kama Mengi nawaona ni Idols. Kupitia ujasiriamali wake maelfu ya watanzania wameajiriwa, lakini mijitu mipuuzi kama Sospeter Muhongo ambayo haijawahi kuajiri na hata housegirl nyumbani kwake hana mkataba wa ajira ndio inayohusika kunegotiate business contract na kufanya maamuzi ya kibiashara kama ya vitalu vya gesi. Muhongo hajawahi hata kufanya biashara ya maandazi but now anafanya business decisions, what a shame to my country.
 
nguvumali

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,893
Points
1,250

nguvumali

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2009
4,893 1,250
2. Katika suala la gesi mimi sipiganii mambo yangu binafsi, kwa sababu mimi nimeshafanikiwa kibiashara. Ninachopigania ni Watanzania wenzangu nao wapate fursa. Naomba nieleweke kwamba ninaposema Watanzania nina maana kuanzia yule mfanyabiashara mdogo wa sekta isyo rasmi, mfanyabiashara wa kati na wafanyabiashara wakubwa. Nataka kuwepo sera ambayo itahakikisha kwamba wanawezeshwa na siyo kusema tu kwamba hawawezi. Nafanya hivyo kwa sababu ninaamini kwamba utajiri uliobarikiwa ni ule uliopatikana kwa njia halali na unatumika kusaidia wanaohitaji msaada.
 
Sword

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Messages
864
Points
0

Sword

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2013
864 0
Hizi nazo ni stori za Abunwasi, toka lini Mengi ukawa na nia thabiti ya kusaidia watanzania? Hapa ni maslahi binafsi yanatafutwa kwa kutaka support kutoka kwa Watanzania ili maslahi hayo yatimie.

Kama kweli Mengi angekua na nia kabisa ya kusaidia watanzania, basi ama kwa hakika angeanzia hapo hapo kwake (Charity begins at home). Angehakikisha anatoa ajira za kudumu kwakuwa wengi wanaofanya kazi katika kampuni zake hawana ajira za kudumu, wengi vibarua.

Pili, angehakikisha mishahara wanayolipwa watanzania inaendana walau namapato yatokanayo na biashara hizo, yani yeye anapata faida kubwa sana katika biashara zake wakati watumishi/wafanyakazi wake wanalia mishahara ni kidogo.

Tatu. bwana mengi kwa kutumia vyombo vya habari anavyomiliki hufanya show-off nyingi ili tu kujipatia umaarufu na si kweli ana nia ya dhati, mfano kuandaa chakula cha pamoja na walemavu, hii haimaanishi kuwa anahuruma sana na hawa watu bali hufanya kwa lengo la kujionyesha, fuatilia katika vyombo vyake vya habari utaona hili, sioni umuhimu wa yeye kuandaa chakula hicho halafu kurusha kwenye vyombo vya habari, ni vyema angekua na nia thabiti ya kuwasaidia ya kuwapa chakula cha siku moja tena mara moja haimsaidii mtu kujikwamua na umasikini.

Namalizia kwa kusema huenda pia kuna mgogoro binafsi wa hawa watu wawili yani Mengi na Muhongo, sasa nashauri mkutanishwe mtatue hizo tofauti zenu na msitake kutuchanganya watanzania japo kwa kiasi fulani hivi nahisi kama Muhongo yupo sawa.
 
nguvumali

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,893
Points
1,250

nguvumali

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2009
4,893 1,250
1. Ningependa kutofautiana na Mhe. Profesa Muhongo na kusema kwamba adui wa maendeleo ya Watanzania siyo Watanzania wenyewe kama alivyosema ila ni Watanzania wachache sana wenye kauli za dharau za kutuambia kwamba Watanzania hatuwezi.
 
nguvumali

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,893
Points
1,250

nguvumali

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2009
4,893 1,250
Hizi nazo ni stori za Abunwasi, toka lini Mengi ukawa na nia thabiti ya kusaidia watanzania? Hapa ni maslahi binafsi yanatafutwa kwa kutaka support kutoka kwa Watanzania ili maslahi hayo yatimie.

Kama kweli Mengi angekua na nia kabisa ya kusaidia watanzania, basi ama kwa hakika angeanzia hapo hapo kwake (Charity begins at home). Angehakikisha anatoa ajira za kudumu kwakuwa wengi wanaofanya kazi katika kampuni zake hawana ajira za kudumu, wengi vibarua.

Pili, angehakikisha mishahara wanayolipwa watanzania inaendana walau namapato yatokanayo na biashara hizo, yani yeye anapata faida kubwa sana katika biashara zake wakati watumishi/wafanyakazi wake wanalia mishahara ni kidogo.

Tatu. bwana mengi kwa kutumia vyombo vya habari anavyomiliki hufanya show-off nyingi ili tu kujipatia umaarufu na si kweli ana nia ya dhati, mfano kuandaa chakula cha pamoja na walemavu, hii haimaanishi kuwa anahuruma sana na hawa watu bali hufanya kwa lengo la kujionyesha, fuatilia katika vyombo vyake vya habari utaona hili, sioni umuhimu wa yeye kuandaa chakula hicho halafu kurusha kwenye vyombo vya habari, ni vyema angekua na nia thabiti ya kuwasaidia ya kuwapa chakula cha siku moja tena mara moja haimsaidii mtu kujikwamua na umasikini.

Namalizia kwa kusema huenda pia kuna mgogoro binafsi wa hawa watu wawili yani Mengi na Muhongo, sasa nashauri mkutanishwe mtatue hizo tofauti zenu na msitake kutuchanganya watanzania japo kwa kiasi fulani hivi nahisi kama Muhongo yupo sawa.
mengi anabaki kuwa raia mzalendo mwenye mafanikio makubwa yakusisimua
 
MjuviKitambo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Messages
640
Points
500

MjuviKitambo

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2013
640 500
Huyu mzee abarikiwe sana. Kwanza nikiri biashara ni ngumu sana, mpaka kufikia mafanikio aliyonayo ni dhahiri kwamba ametumia akili na nguvu nyingi Kweli Kweli. HONGERA ZAKE.
Prof. Muhongo sio kwamba hana akili, au labda haelewi afanyalo na madhara yake kwa taifa...anako atoako Hizi jeuri...anako apatumainiapo. Kuna Genge pengine linaloratibu haya mauzo ya nje yetu( nasi tukiwemo) ...nalo si dogo wala sio la kunuachia mzee Mengi peke yake. Nguvu kubwa zaidi inahitajika sasa. Tuungane.
 
Sword

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Messages
864
Points
0

Sword

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2013
864 0
Mkuu umeshawahi kulinganisha mishahara ya IPP na makampuni mengine?

Fanya utafit kwanza, angalia bakhreasa, na migodi na makampuni makubwa yapi yanalipa kodi vizuri.

Mengi ni mzalendo wa ukeli...
Go on go go go Menji
Mimi nimefanya utafiti na ukweli ndio huo, Mengi analipa mishahara midogo sana na tena ni mkabila. Mimi nimejikita zaidi katika vyombo vya habari anavyomiliki, waandishi wengi wanaofanya kazi kwa Mengi mishahara yao ni duni huwezi kulinganisha na Mwananchi. Kingine nikufahamishe jina lake sio Menji ni Mengi na hilo jina alipewa kwasababu ni mpenda mengi, yani anatamaa ndio maana wakampachika hilo jina kwa tamaa zake ya kutaka kumiliki kila kitu huku akiwahadaa wananchi eti yeye yupo kwa maslahi ya wanyonge.
 
Forum statistics

Threads 1,389,189
Members 527,870
Posts 34,019,484
Top