John Mhala, Arusha
HabariLeo; Saturday,December 08, 2007 @00:04
MKURUGENZI wa Taasisi ya Utafiti wa Dawa za Mimea na Wadudu (TPRI) iliyopo mkoani Arusha, Dk. Ratian Bamwenda, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na tuhuma mbalimbali ndani ya taasisi hiyo, ameondolewa kwenye wadhifa huo.
Uamuzi huo ulitangazwa juzi mbele ya wafanyakazi wa taasisi hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya TPRI, Profesa Pili Sibuga, baada ya kumalizika kwa kikao cha Bodi ya taasisi kilichofanyika siku hiyo.
Profesa Sibuga aliwaambia wafanyakazi hao kuwa Dk. Bamwenda ameondolewa katika nafasi hiyo na ataripoti wizarani kupangiwa kazi nyingine na tayari Bodi hiyo imekwishakumteua mtu mwingine wa kukaimu nafasi hiyo.
Uamuzi wa kuondolewa katika wadhifa huo Dk. Bamwenda umefanyika huku akiwa nje ya nchi na nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Dk. Roshan Abdallah.
Baada ya kutoa taarifa hiyo, pia Mwenyekiti wa Bodi alimtaja Kaimu Mkurugenzi kuwa ni Dk. Boaz Uranu, atakayekaimu nafasi hiyo hadi serikali itakapotangaza mkurugenzi mpya.
Dk. Bamwenda amekuwa akituhumiwa kwa muda mrefu na wafanyakazi wa taasisi hiyo kwa ubadhirifu wa fedha za utafiti za taasisi hiyo, kwa ununuzi wa magari hewa ya taasisi na kufanya taasisi ishindwe kufanya utafiti kama ilivyokusudiwa.
Kuondolewa kwa Dk. Bamwenda katika taasisi hiyo kumetangazwa huku serikali ikiwa imefanya mabadiliko makubwa ya wakurugenzi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, miongoni mwa waliokumbwa na mabadiliko hayo ni Mkurugenzi wa Wanyamapori, Emmanuel Severe.
Severe kwa muda mrefu sasa amekuwa akituhumiwa kukwamisha utendaji wa viongozi wengine wa serikali na aliwahi kukataa uhamisho uliofanywa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo, wa kumpeleka kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) Arusha.
Mkurugenzi huyo na wenzake wameelezwa kuwa watapangiwa kazi nyingine, lakini taarifa zinadai wengi wao akiwamo Severe watapelekwa kwenye vyuo vya wizara hiyo, huku Severe akitajwa kuwa anakwenda katika Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori cha Mweka, Kilimanjaro.