Dk. Rashidi, Kazaura hawaivi

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,546
845
Mmoja alipokonywa gari na ofisi

KUJIUZULU Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Dk. Idris Rashidi, pamoja na mambo mengine, kunaelezwa kutokana na msuguano wa muda mrefu kati yake na Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Fulgence Kazaura.

MKURUGENZI Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idris Rashidi

Habari zinasema katika moja ya misuguano hiyo, mara baada ya kuingia Tanesco, Dk. Rashidi alifanya mabadiliko kadhaa yaliyolenga kupunguza matumizi na uboresha huduma kwa wateja, uamuzi ambao ulimgharimu Balozi Kazaura, aliyepunguziwa baadhi ya huduma.

Kazaura alikua na ofisi katika majengo ya Tanesco barabara ya Samora yalipokua makao makuu ya shirika hilo, ofisi ambazo sasa zinatumiwa na Meneja shirika hilo Mkoa wa Ilala.

Mkurugenzi aliamua ofisi aliyokua akiitumia Mwenyekiti wa Bodi itumiwe na Meneja Mkoa wa Ilala, na gari alilokua akitumia nalo lifanye kazi nyingine za kiutendaji na Mwenyekiti apatiwe huduma hizo wakati wa vikao husika pekee, kinasema chanzo chetu cha habari ndani ya Tanesco.

Kwa mujibu wa habari hizo, Balozi Kazaura alikuwa pia na Katibu Muhtasi, aliyetajwa kwa jina la Rukia Wandwi, ambaye alikua katika ofisi hiyo iliyokabidhiwa Tanesco Mkoa wa Ilala.

Kwa mujibu wa habari hizo, hatua hiyo haikumfurahisha Balozi Kazaura na baadhi ya watumishi ambao baadhi walisema pamoja na kuwa utaratibu hauruhusu Mwenyekiti kuwa na ofisi inayohudumiwa wakati wote na shirika, ilipaswa busara na diplomasia itumike kumnyanganya ofisi Mwenyekiti.

Unajua kwanza bodi yenyewe ndiyo inamaliza muda wake kwa hiyo ingekuwa busara kumwacha amalize muda wake ndipo uwekwe utaratibu mwenyekiti mpya anapokuja asiwe na ofisi badala ya kumuondoa na kumdhalilisha mzee wa watu, anaeleza mfanyakazi mwingine wa Tanesco anayelifahamu sakata hilo vizuri.

Habari zaidi zinaeleza kwamba tofauti kati ya Dk. Rashidi na Mwenyekiti wake zilianza wakati Balozi Kazaura akiwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, yeye (Dk. Rashidi) akiwa Gavana wa Benki Kuu (BoT).

Hawa watu hawakuwa na mawasiliano mazuri tokea wakiwa serikalini, Kazaura akiwa Wizara ya Fedha na Dk. Rashidi akiwa BoT, lakini sina hakika walitofautiana kwa jambo gani. Kila mmoja ni mtu mwenye kujiamini, anasema mtumishi mmoja mstaafu wa Serikali.

Balozi Kazaura alipoulizwa na Raia Mwema kuhusu kuondolewa baadhi ya huduma, alijibu, huo ni uongo, na kukata simu yake ya mkononi ambayo baadaye ilipokewa na mtu mwingine aliyedai kwamba mzee ametoka, sijui amekwenda wapi.

Kwa upande wake, Dk. Rashidi alisema yuko katika kikao na hivyo hawezi kuzungumza jambo lolote na hadi tunakwenda mitamboni hakuweza kupatikana kuzungumzia mahusiano yake na Mwenyekiti wa Bodi.

Awali ilielezwa kwamba bodi nzima ya Tanesco imegawanyika katika makundi mawili - moja likimuunga mkono Mwenyekiti na jingine Mkurugenzi huku wengine wote wakionyesha kutofurahia msuguano kati ya viongozi hao wawili.

Balozi Kazaura amenukuliwa na mtoa habari wetu akisema kwamba Dk. Rashidi anawajibika kwa Bodi kwa mujibu wa sheria ya kuundwa kwa Tanesco na si Rais kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakimtaka (Mwenyekiti) amheshimu kwa kuwa ni mteule wa Rais.

Tukio la hivi karibuni la Tanesco kukata umeme wa kiwanda cha Saruji cha Tanga, lilielezwa kutonesha kidonda cha msuguano wa muda mrefu kati ya Dk. Rashidi na Mwenyekiti wake, ambaye anaelezwa kupewa maelekezo ya kuhakikisha umeme unarudi.

Haijafahamika mara moja ni nani aliyemuagiza Mwenyekiti ahakikishe umeme unarudi, japo kuna taarifa kuwa amri hiyo inaweza kuwa imetoka kwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ambaye hata hivyo amekwisha kukanusha kuhusika katika suala hilo.

Kiwanda hicho cha Saruji cha Tanga ambacho hutumia umeme wa zaidi ya milioni 400/- kwa mwezi, kilikatiwa umeme kikidaiwa milioni 49/- ambazo zilitokana na madai ya kuchezea mita ya Tanesco.

Kujiuzulu kwa Dk. Rashidi kulikotokana kwa kiasi na msuguano huo wa umeme wa kiwanda hicho, na hatimaye, kubadili kwake uamuzi na kuifuta barua yake ya kujiuzulu, kumezua maswali mengi katika kipindi hiki ambacho shirika analoliongoza limo katika hali mbaya ya kifedha kutokana na matumizi kuwa makubwa kuliko mapato.

Wako wanaodai kwamba Rais Jakaya Kikwete, ndiye aliyemuomba Dk. Rashidi kubadili uamuzi wake wa kujiuzulu, huku baadhi wakidai kwamba aliombwa na Waziri Karamagi.

Lakini jambo lililo dhahiri ni kwamba aliombwa kubadili uamuzi wake huo. Habari za ndani zaidi zinaeleza kwamba mbali ya kuombwa kubadili uamuzi wake huo, Dk. Rashidi sasa amepewa uwezo zaidi wa kufanya maamuzi mazito zaidi ndani ya shirika hilo ili aweze kulikwamua kiuchumi.

Tayari shirika hilo limekwisha kuomba idhini ya kupandisha bei ya umeme ili kufidia sehemu ya gharama za umeme wakati shirika hilo limetakiwa kujiendesha kibiashara.

Dk. Rashidi anaelezwa kupelekwa Tanesco ili kulikwamua shirika hilo katika matatizo ya kifedha kutokana na uzoefu wake katika masuala ya fedha na uchumi, lakini wachunguzi wa mambo wanasema hawezi kufanikiwa hadi Serikali ilisaidie kwa kulipa fedha za kulipa madeni na kuepuka mikataba mibovu.

Tanesco inaelezwa kuwa katika hali ngumu kutokana na kuwa na matumizi makubwa kuliko mapato lakini zaidi kutokana na kuelemewa na mikataba kadhaa mibovu inayowalazimu kulipa sehemu kubwa ya mapato yake.

Shirika hilo hivi sasa linalazimika kulipa mamilioni ya shilingi kwa mradi wa umeme wa gesi wa Independent Power Limited (IPTL) huku ikiwa na mikataba mingine inayoashiria hatari zaidi kama ule wa Kiwira Coal Power na ule wa Richmond Development ambao Bunge limeunda Kamati ya kuuchunguza.

Shirika hilo linaelezwa kupoteza shilingi bilioni 6.4/- kwa mwezi kutokana na kushindwa kupandisha bei ya umeme kama lilivyoomba.

Taarifa za Tanesco zinaeleza kwamba shirika hilo ni lazima lipandishe bei ya umeme kwa asilimia arobaini (40%) maombi ambayo yamewasilishwa kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

Shirika hilo kwa sasa linatoza wateja wake Shilingi 84/- kwa uniti moja wakati gharama za uzalishaji ni shilingi 183/- kwa uniti moja na hivyo kulifanya shirika hilo kupoteza shilingi 99 kwa kila uniti inayotumika.

Dk. Rashidi aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco mwishoni mwa mwaka jana kuchukua nafasi ya menejimenti ya Net Group Solutions kutoka Afrika Kusini iliyohitimisha mkataba wake wa miaka minne Desemba 31 mwaka jana.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Rashidi alikuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rabobank Holland inayosimamia shughuli za benki ya National Microfinance (NMB) tangu Oktoba mwaka juzi.

Mbali ya kuwa Gavana wa BoT, Dk. Rashidi aliwahi pia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC kati ya mwaka 1992 hadi Juni mwaka 1993 na Mkurugenzi wa Benki ya Akiba Commercial (ACB) tangu mwaka 1999 hadi Machi 2000.

raiamwema.co.tz
 
Wewe babayangu, Kazaura, magari na ofisi vinakufanya mnashindwa kuelewana kweli? Kwanzaa nakupongeza kwa ukarimu wako juu ya Watanzania. Usikubali hata maramoja kisa ni mchumi. Huo uchumi akauendeleze Akiba Bank. Hapa anagusa maisha ya Watanzania, na kama Jakaya Kikwete umemwomba kisa kumkubalia matakwa yake kupandisha umeme, hakika damu za Watanzania utasikia harufu yake muda si mrefu. Ila kama swala ni kweli, magari mbona babayangu huyu jamani anamagari kama uchafu? Maana naomba wenye hints kidogo wadondoshe kabla sijashuka.

Mkuu ni mwenyekiti wa board, sijui zaidi ya ngapi, na kila sehemu an ofisi yake, chuo kikuu yeye na mkumbuke huyu ndie wetu pale chuo SISM. TANESCO yeye, nyingine nikiorodhesha nasikitika mliokuwepo Mlimani na hivyo vyuo vya nje, natumaini mtaamua kubaki uko mliko. Maana sasa hivi mwenye nacho ndio anaongezewa, karibuni Tanzania!

Mtu mmoja, mbunge, mwenyekiti wa bodi, mjumbe wa NEC, yeye huyohuyo anaongoza kamati mbili zilizoteuliwa na raisi. Unafikiri ijekukuta wewe nafasi hizo, si ushakufa. Loh! Baba Rashidi, usituue wanao, si ni Watanzania kama wengine. Tulitamani kwenda kusoma na kuishi maisha mazuri nje kama wanao. Tuoneeni huruma vizazi haba. Na Mungu akubadilishe kwa uamuzi wako, na wote tumshukuru Mungu kwa kusema AMEN.
 
Kwani lazima wawe marafiki? Wao wachape kazi tu kwa kufuata taratibu na sheria walizojiwekea katika shirika lao, sio lazima waelewane
 
Kwani lazima wawe marafiki? Wao wachape kazi tu kwa kufuata taratibu na sheria walizojiwekea katika shirika lao, sio lazima waelewane

Si lazima waive, wanaweza kukubaliana kutokukubaliana katika masuala binafsi na kupishana mawazo lakini kwa kuwa kuna kanuni za utendaji wachape kazi.

Tatizo la kupanda kwa bei ya umeme ni la kifisadi, utakuta shirika la umeme linahujumiwa kila kona, kuna RICHMOND, IPTL, KIWIRA wizi wa mafuta ya Transforma, Vishoka, kujiunganishia umeme kinyemela au kwa wizi. Kwa haya yote ni lazima TANESCO ijiendeshe kihasara na njia moja wapo ya kuikwepa hii hasara ni kwa kumbambikia mlalahoi bei kubwa ya umeme wakati watumishi wa TANESCO wakiwa na bei zao ndogo na Mafisadi yakiwa hayalipii kabisa matumizi ya umeme.

HII NCHI HAITAKAA IPIGE HATUA ZA KIMAENDELEO BILA KUUKATA KWANZA MZIZI WA UFISADI.
 
kwa nini lakini? hivi wao waingie mikataba mibovu kwa ajili yao na ufisadi wao waishie kulipa milions for nothing, halafu mzigo wote wabebe watanzaania maskini kama mimi kwa kupandishiwa bei ya umeme. Wake up watanzania, tuandamane hadi watupige risasi, this is too much jamani.
 
Si lazima waive, wanaweza kukubaliana kutokukubaliana katika masuala binafsi na kupishana mawazo lakini kwa kuwa kuna kanuni za utendaji wachape kazi.

Tatizo la kupanda kwa bei ya umeme ni la kifisadi, utakuta shirika la umeme linahujumiwa kila kona, kuna RICHMOND, IPTL, KIWIRA wizi wa mafuta ya Transforma, Vishoka, kujiunganishia umeme kinyemela au kwa wizi. Kwa haya yote ni lazima TANESCO ijiendeshe kihasara na njia moja wapo ya kuikwepa hii hasara ni kwa kumbambikia mlalahoi bei kubwa ya umeme wakati watumishi wa TANESCO wakiwa na bei zao ndogo na Mafisadi yakiwa hayalipii kabisa matumizi ya umeme.

HII NCHI HAITAKAA IPIGE HATUA ZA KIMAENDELEO BILA KUUKATA KWANZA MZIZI WA UFISADI.

Wananchi inabidi tuanze kuwashikisha adabu wale wote wanahujumu shirika kuanzia wezi wa mafuta ya transfoma, nyaya, wanajiunganishia umeme kwa dili maana nao wanatuumiza wengine tunaolipa kihalali,wadaiwa sugu nao walazimishwe kuanza kulipia madeni yao na TANESCO iachiwe ijiendeshe yenyewe bila kuingiliwa na serikali kuu.
 
Kwani lazima wawe marafiki? Wao wachape kazi tu kwa kufuata taratibu na sheria walizojiwekea katika shirika lao, sio lazima waelewane

TANESCO ni shirika nyeti. Hawa jamaa hawatakiwi kuwa marafiki lakini ni lazima wawe on the same page when it comes to important decisions about TANESCO and its product, otherwise they are doomed to fail. Rais inabidi amuondoe mmoja haraka sana kabla hakujazuka mtafaruku mwingine.
 
I will tell you tommorow why Idrissa resigned.

We have long way to go comrades, this country needs liberation and we need to join forces who we are within the system and those who are outside the system too.

I sign out cause here in the office i m watched so much.
 
I will tell you tommorow why Idrissa resigned.

We have long way to go comrades, this country needs liberation and we need to join forces who we are within the system and those who are outside the system too.

I sign out cause here in the office i m watched so much.

Uhuuuu, isije ikawa Hurma mwingine!
 
I will tell you tommorow why Idrissa resigned.

We have long way to go comrades, this country needs liberation and we need to join forces who we are within the system and those who are outside the system too.

I sign out cause here in the office i m watched so much.

Naona Hasara amekuja na jina lingine style ile ile....hataonekana tena JF....mmmmhh kazi kweli kweli...
 
..Dr.Rashidi ameshakuwa hero tayari?

..huyu si ndiyo walikopa NSSF mil 50 yeye na Sumaye kwa ajili ya ujenzi wa nyumba?

..hivi Kamati ya Bunge ya Oyombe Ayila ilisema nini kuhusu Dr.Rashidi na OGL funds?
 
Mkurugenzi Tanesco: Kiwanda cha Saruji Tanga lazima kilipe deni

Na Andrew Msechu

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Dk Idris Rashidi amesema Kiwanda cha Saruji Tanga kinapaswa kulipa deni lake la umeme katika muda waliopewa.

Akizungumza ofisini kwake jana, Dk Rashidi alisema kiwanda hicho ambacho kilikatiwa umeme na hatimaye kurejeshewa kabla ya kulipa deni lake, hakina budi kulipa deni hilo ndani ya muda uliowekwa ambao mwisho wake ni Desemba 20, mwaka huu.

"Nilipomaliza masuala yangu na kurejea nilielezwa kuwa wameandikiwa barua wakitakiwa kulipa deni hilo mwisho wa mwezi, umeme bado wanaendelea kuutumia, lakini suala la kulipa si la mjadala, ni lazima walipe," alisema.

Tanesco ilikata umeme katika kiwanda hicho kwa kuwa ilikuwa ikidai zaidi ya Sh49milioni, uamuzi ambao ulipingwa na kiwanda, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Balozi Fulgence Kazaura. Baada ya hatua hii ya kuingilia kwa wakubwa hao, Dk Rashidi aliandika barua ya kutaka kujiuzulu.

Katika hatua nyingine, Dk Rashidi alisema kuwa hajawahi kuingiliwa katika kazi zake na viongozi wa juu wa serikali akiwemo Waziri Mkuu Edward Lowassa, kama ilivyodaiwa mara baada ya kutangaza kwake kujiuzulu wiki iliyopita.

Wiki iliyopita, Mkurugenzi huyo aliripotiwa kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo, kukiwa na maelezo ya sababu mbali mbali zilizopelekea kuamua kujiuzulu, lakini baadaye kuamua kutengua uamuzi wake huo na kurejea kwenye wadhifa wake wa awali.

Dk Rashid alisema pamoja na kuelezea kwake kukerwa na kuingiliwa na baadhi ya viongozi, hakuwahi kuingiliwa na Waziri Mkuu kama ilivyodaiwa.

Alisema mzozo huo uliopelekea kuandika barua ya kujiuzulu na hatimaye kutengua uamuzi wake, si sahihi kuwahusisha viongozi wakuu wa nchi kwa kuwa hawajawahi kuwasiliana naye, wala kutoa agizo lolote kwa menejimenti na Bodi ya Tanesco katika utendaji wake.

"Wapo waliokuwa wakiingilia maamuzi ambao walishatajwa, wakiwemo walioingilia suala la kiwanda cha saruji Tanga, lakini mimi sijawahi kuwasiliana, kuzungumza wala kupokea amri kutoka kwa Waziri Mkuu kipindi cha matatizo haya, ninaomba suala hili lisifanywe kuwa malumbano hadi kuingia kusikohusika," alisema Dk Rashid.

Dk Rashid aliongeza kuwa kwa sasa, vuguvugu lililokuwepo kuhusu nia yake ya kujiuzulu limeshamalizika hivyo suala lililopo ni kuangalia hatua za kiutendaji zinazoweza kulipeleka mbele shirika hilo.

Dk Rashid alifahamisha kuwa Tanesco ina mpango wa kufanya ukarabati wa kubadili mfumo wa mitambo ya kutengeneza umeme ya IPTL kutoka kwenye matumizi ya mafuta kwenda kwenye matumizi ya gesi ili kupunguza gharama za uzalishaji umeme.

Alisema tayari Benki ya Dunia imesharidhia kutoa kiasi cha fedha kinachohitajika hivyo ukarabati huo unatarajiwa kuanza mwaka 2009, baada ya kukamilika kwa mpango wa kuongeza uwezo wa mitambo ya gesi ya Songosongo kusukuma gesi nyingi zaidi.

Source: Mwananchi
 
..Dr.Rashidi ameshakuwa hero tayari?

..huyu si ndiyo walikopa NSSF mil 50 yeye na Sumaye kwa ajili ya ujenzi wa nyumba?

..hivi Kamati ya Bunge ya Oyombe Ayila ilisema nini kuhusu Dr.Rashidi na OGL funds?

jokaKuu ukikumbusha hayo ya OGL na Chavda unaweza kusababisha jamaa apate Pressure! sometimes huwa tunawasifia watu pasipokujua nini walifanya huko walikotokea. ni ukweli kwamba alipokuwa BoT naye alitafuna mihela, lakini sasa hivi anasifiwa kwamba hero, may be amebadilika siku hizi baada ya kulamba bingo ya fedha za OGL! nimekubali JF watu wanatunza kumbukumbu!
 
Jokakuu tumwagie hizo data kuhusu OGL na kamati ya Ayilla... maana kuna dots that need to be connected..
 
..Dr.Rashidi ameshakuwa hero tayari?

..huyu si ndiyo walikopa NSSF mil 50 yeye na Sumaye kwa ajili ya ujenzi wa nyumba?

..hivi Kamati ya Bunge ya Oyombe Ayila ilisema nini kuhusu Dr.Rashidi na OGL funds?


Joka mwaga upupu wao.
 
Kwani lazima wawe marafiki? Wao wachape kazi tu kwa kufuata taratibu na sheria walizojiwekea katika shirika lao, sio lazima waelewane

Kitila,

Umesema kweli kabisa, ili kusimamia vizuri corporate governance sio lazima hawa wawe marafiki, tena wasipokuwa marafiki ni nzuri zaidi.

Kinachonishangaza kama Mwenyekiti aliachwa bila ofisi wala watendaji wakumsaidia, angewezaji kufanya kazi za kulinda maslahi ya stakeholders? Unles kama alikuwa anataka jengo zima lakini kuwa na ofisi ni kitu muhimu kwa Mwenyekiti wa board ya shirika kubwa kama Tanesco.

Kama hawakumpa ofisi basi ilitakiwa wawe tayari kulipia ofisi ambayo angepanga.

Tatizo la Tanzania hakuna corporate governance na Mwenyekiti wa board anaonekana kama yupo yupo tu.
 
Kitila,

Umesema kweli kabisa, ili kusimamia vizuri corporate governance sio lazima hawa wawe marafiki, tena wasipokuwa marafiki ni nzuri zaidi.

Kinachonishangaza kama Mwenyekiti aliachwa bila ofisi wala watendaji wakumsaidia, angewezaji kufanya kazi za kulinda maslahi ya stakeholders? Unles kama alikuwa anataka jengo zima lakini kuwa na ofisi ni kitu muhimu kwa Mwenyekiti wa board ya shirika kubwa kama Tanesco.

Kama hawakumpa ofisi basi ilitakiwa wawe tayari kulipia ofisi ambayo angepanga.

Tatizo la Tanzania hakuna corporate governance na Mwenyekiti wa board anaonekana kama yupo yupo tu.

Mtanzania,
Mwenyekiti wa Bodi si mtendaji kwa hivyo HAHITAJI ofisi. Nadhani hata wenyeviti wa bodi za makampuni mengine ni hivyo hivyo ... na hata huku Marekani ni hivyo hivyo. Kwanza unaweza kukuta sana sana bodi inakutana kwa wastani wa mara 1 kwa mwezi; sasa hiyo ofisi ni ya nini??!!
 
Mtanzania,
Mwenyekiti wa Bodi si mtendaji kwa hivyo HAHITAJI ofisi. Nadhani hata wenyeviti wa bodi za makampuni mengine ni hivyo hivyo ... na hata huku Marekani ni hivyo hivyo. Kwanza unaweza kukuta sana sana bodi inakutana kwa wastani wa mara 1 kwa mwezi; sasa hiyo ofisi ni ya nini??!!

Watu wewe,

Nafikiri unaelewa maana ya corporate governance, hakuna sehemu niliyosema Mwenyekiti wa board ni mtendaji. Nilichosema ni kwamba wajibu wa hao non-executive members wa board ni kulinda maslahi ya stakeholders wa Tanesco, ingelikuwa kwenye private companies basi ni kulinda maslahi ya shareholders. Matumizi yao pamoja na vitendea kazi vyao hutolewa na kampuni husika.

Wanaweza wakawa wanakutana mara kumi au hata chini ya hapo kwa mwaka, lakini pia wanatumia sehemu ya muda wao kwenye shughuli mbalimbali za kampuni, kwa mfano uteuzi wa mkurugenzi wa board, mishahara ya wakurugenzi nk.

Sio lazima wawe na ofisi kwenye eneo la kampuni husika lakini kama wanahitaji ofisi kwa matumizi yao kwa ajili ya kampuni husika basi hayo matumizi yanalipwa na kampuni.

Kama huyo Mwenyekiti alikuwa na ofisi Tanesco, sioni ubaya wake maana vinginevyo si ajabu Tanesco wangelazimika kumlipia ofisi sehemu nyingine. Mwenyekiti anatumia sehemu kubwa ya muda kufanya kazi za kampuni tofauti na hao wajumbe wengine.
 
Back
Top Bottom