Dk Mwinyi, Mwamunyange wakwama kwenye lifti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Mwinyi, Mwamunyange wakwama kwenye lifti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EMT, Feb 19, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  MSAFARA wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Mwinyi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, wameonja adha ya mgawo wa umeme baada ya kukwama kwenye lifti kwa muda wa zaidi ya dakika nne, kufuatia kukatika umeme. Adha hiyo iliwakuta wakati walipokwenda kuwajulia hali watoto wawil,i ambao wamelazwa wodi zilizopo ghorofa ya tatu jengo la wodi ya watoto.

  Dk Mwinyi baada ya kupokelewa, aliongozwa hadi kwenye jengo hilo na kufunguliwa lifti ambayo walipanda na msafara wake, baada ya milango kujifunga na kabla safari haijaanza umeme ulikatika. Hali hiyo ilizua kizazaa cha muda na askari na maofisa wengine waliokuwa nje, walianza kuwasiliana na wenzao waliotangulia na Dk Mwinyi na Mwamunyange.

  Maelekezo yaliyotoka kwa baadhi ya wauguzi ni kuwataka wasome namba ambazo zipo ndani ya lifti, hivyo askari hao waliwapigia simu wenzao waliokuwa na waziri na kuwapa maelekezo. Waliwapigia simu mafundi ili kwenda kuwasaidia.
  "Someni namba hizo zilizopo hapo pembeni karibu na hivyo vitufe tuwapigie simu," alisema muuguzi mmojawapo jirani na mlango.

  Wakati hekaheka za kuwasaka mafundi zikiendelea, ghafla mlango ukafunguka na haikujulikana ni njia iliyotumiwa na waziri aliyekuwa amevaa koti alitoka nje akiwa amelishika mkononi huku akijifuta jasho.

  Kutokana na kadhia hiyo, ilibidi Waziri Mwinyi na Jenerali Mwamunyange kutumia ngazi kwenda kuona majeruhi hao, walimkuta mtoto moja na mwingine tayari alikuwa ameruhusiwa.

  Waziri na msafara wake waliendelea na ziara yao wodi zingine, ikiwamo Mwaisela na Kibasila na kuzungumza na waathirika wa mabomu na baadhi ya madaktari wamelalamikia kuhusu mgawo wa umemu hospitalini hapo.

  "Kipindi hiki cha janga kama hili sioni logic (msingi) ya kuendelea kwa mgawo hata kwa hospitali ya Taifa, pengine kutokana na kilichompata waziri kuna kitu watajifunza," alisema daktari mmojawapo ambaye hakutaka kutajwa.

  Daktari mwingine hospitalini hapo, alilalamikia hali hiyo kuwa inachangia vifo vya majeruhi na wagonjwa wengine, kwani madaktari wapo na wanataka kufanyakazi lakini wanatatizwa na ukosefu wa umeme.

  Dk Mwinyi, Mwamunyange Waonja adha ya umeme
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hivi hata hospitali kubwa kama muhimbili wanapewa umeme kwa mgao? tena hata katika kiindi kama hiki cha janga la GLM? jamani kweli nchi yetu hii ngumu kuishi!
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kikwete aliahidi kuibadilisha iwe Dubai ya Afrika, na TUME ikaridhia! Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, tutafika tu.
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kama hata hosipitali kubwa kama Muhimbili inapata mgao wa umeme basi kwisha kazi.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  tena tutafika mapema 2kiwa salama
   
 6. v

  vassil Senior Member

  #6
  Feb 19, 2011
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kwa nini waliwafungulia wangewaacha kwa siku mbili pumbavu nani amewaambia tunataka kuona sura zao muhimbili
   
 7. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuna viongozi wenye mgao wa akili, tegemea madudu tu.
   
 8. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ingependeza sana kama mlango ungejifunga kwa angalau nusu saa. Ningefurahi sana.
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nini kukwama, wapolomoke kabisa.
   
 10. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2011
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ...Ameahidi mangapi?
   
 11. Double X

  Double X Senior Member

  #11
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kukwama wao haitoshi walitakiwa wamalizikie humo ndani ya lifti kabisa, hawana faida yoyote kwa watz.
   
 12. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #12
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :A S 112:kama hadi muhimbili kuna mgao,serikali yastahili kuwajibishwa:rain:
   
 13. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #13
  Feb 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Hata Muhimbili napo kuna mgawo??????
  Kweli Serikali yetu imeshakufa kibudu...
   
 14. c

  chetuntu R I P

  #14
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani muhimbili mgao wa nini tena na hawa majeruhi? Daah. Y mijitu haithink of that. Aaaaaagh .
   
 15. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Siamini wakuu kama mlikuwa hamjui kama hata Muhimbili napo kuna mgao! kha!?? mbona ulianza kuda mrefu tu! tangu 2005! sem sio mara kwa mara kama Mbagara au Gongo la Mboto!
   
 16. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  binamu unachangaa nn wakati kwnye ghala kuu la silaha wanakatiwa umeme pia
   
 17. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mgao upo nchi nzima save kwa wakubwa
   
Loading...