Dk. Mwinyi ataka Waislamu kushikamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Mwinyi ataka Waislamu kushikamana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzito Kabwela, Jul 18, 2011.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi La kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, amewataka Waislamu nchini kushirikiana ili kujenga umoja thabiti kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu dini yao.


  Dk. Mwinyi amewataka pia wanazuoni wa Kiislamu kufanya utafiti zaidi kwa lengo la kuusaidia Uislamu kusimama katika misingi yake kama ilivyokusudiwa na Mwenyezi Mungu.


  Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Peacock Hotel, wakati akizindua kitabu chenye maudhui ya mwezi upi sahihi wa kitaifa au wa kimataifa kilichoandikwa na Profesa, Juma Mikidadi, ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislamu mkoani Morogoro (MUM).


  Katika uzinduzi huo ulioratibiwa na Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Dk. Mwinyi, alisema suala la muandamo wa mwezi limekuwa likiwagawa Waislamu pasipo sababu za msingi hali inayosababisha umoja baina yao kutokuwepo.


  “Hili la mwezi tumekuwa tukitofautiana kwa muda mrefu, na sasa kuna hiki kitabu tunashukuru kitatoa mwanga kwetu kwa kuwa nina hakika mwandishi amefanya tafiti za kutosha hata akaamua kuja na hoja hii,” alisema Waziri Mwinyi.


  Alisema kutofautiana kusiwe sababu ya kugombana hivyo watumie nafasi hiyo ya kutofautiana kufahamishana zaidi juu ya maagizo ya Mwenyezi Mungu.
  Huku akinukuu baadhi ya aya za Mwenyezi Mungu zinazohimiza kushirikiana Dk. Mwinyi alisema pamoja na mambo mengine kuna haja ya kuwakutanisha Waislamu na kuweka umoja wao.


  Awali akizungumzia kuhusu kitabu hicho, Profesa Juma Mikidadi, alisema ni aibu kwa Waislamu kuitana majina mabaya kwa sababu ya kuhitilafiana katika kufunga na kufungua jambo ambalo alisema linawezekana likaongelewa na kupata muafaka wa kitu cha kufanya kwa ajili ya Waislamu.
  Alisema ni jambo la kushangaza kuona Waislamu wakifikiria kutengana katika suala hilo wakati dunia inahimiza kuunganisha nguvu.

  Source:
  http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=32711
   
 2. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Washikamamne au waswali?
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Washikamane ili kuhakikisha wanamchagua yeye kuwa rais!!
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Thread hiyo HAPA SIO MAHALI PAKE,Msimsingizie kuwa Mazungumzo yake yalihusu SIASA.Ukitizama Mwaliko wake huko ulikaa zaidi kwenye IMANI YA DINI YAKE YA UISLAM.Hivyo sioni ni kwanini ikakubliwa kukaa kwenye POLITICS.

  Maudhuhi yote ya ujumbe huo uko ni kuhusu maswala ya UISLAM kwenye mfungo wao.Kwani nin mambo ya imani za watu zinaingizwa kwenye SIASA.Naomba thread hii ipelekwe kwenye Dini hapa sio mahala pake.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Dr Husein Mwinyi. Hakika wewe ni kiooo cha WaZanzibar ndani ya Watanzania. Huna kashfa yoyote ya ufisadi . Big up.
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Karibu MBAGALA na GONGO LA MBOTO sheikh tule pilau....
   
Loading...