Mbojoz
JF-Expert Member
- Jul 7, 2016
- 578
- 562
Ni kweli tafiti husomwa na mtafititi, lkn kwa ugonjwa kama ZIKA ilikuwa lazima uwasiliane kwanza na uongozi wa juu yako(wizara). Iko hivi, kwa wataalam wa Maabara kama anampima mtu HIV huwezi ukatoa majibu kirahisi kama ya mgonjwa wa malaria, lazima ujiridhishe kwanza(utapima kwa vipimo zaidi ya kimoja kama unavyo),pia kama mko wawili utamshirikisha na mtaalam mwenzio naye ajaribu kupima kama majibu yatalingana, majibu yakiwapa matokeo Sawa sasa process ya kumpatia mgonjwa majibu hufuata kwa utaratibu. Sasa huyu mama kweli watalamu wake walifanya utafiti wakagundua kuna virus vya ZIKA ilitakiwa kwanza awasiliane na wizara ikiwezekana sample walizotumia zipelekwe hata kwenye Maabara zingne hata nje ya nchi kwa utambuzi zaidi, baada ya hapo ndio majibu yakilingana na ya kwake sasa watatangaza, sasa yeye kapita shortcut. ZIKA ni ugonjwa mkubwa sana kuuchukulia kama vile ni malaria utaleta tahaaruki.