Dk. Mwele Ntuli Malecela ametoa somo kubwa kwenye vyombo vya usalama

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
4,301
2,000
Hili ni zaidi ya somo, kumbe ndani ya serikali mtu anaweza kuibuka nakusoma taarifa amabayo matokeo yake yanaweza kuwa ni janga la taifa. Kiuhalisia hakuna alie juwa Malecela alikuwa kienda kusoma taarifa nzito ambayo uwenda ingweza kwenda kusababisha madhara makubwa kwa taifa.
Hili nijambo la hatari sana na tusikatae vyombo vya usalama vimeona madhara ya watumishi wa seikali kufanya mambo pasipo kutoa taarifa kwa wizara husika.
Ikiwa serikali itaangalia hili jambo kwa jicho la saba unaweza kugunduwa upo udhaifu mkubwa sana ktk utowaji taarifa za serikali, mfano mzuri nikile kitendo cha mh fulani kumchongea mkurugenz mahali ambapo hapakuwa mahali pa kufanya hivyo, pia siku zakaribuni wakurugenz na wakuu wa mikoa wamekuwa na matamko ambayo yanaleta taharuki kwa taifa yote haya ni darasa kwa vyombo vyetu vya usalama.

Nilazima kuanzia sasa kuwe na utaratibu wakuangalia nini nani anasema upo uwezekano mkubwa Mh Ummi alialikwa na Mkurugenz na report alikwenda kuisikiliza protoco kama hizi ni hatari kwa usalama yani waziri anakaribishwa kusikiliza report amabyo hata yeye uwenda hajaiona au kujuwa nini kitasomwa.

Nimtu mjinga au asie na ufaham mzuri kwenye maswala yakiusalama anaweza kusimama nakumtetea huyu mama, kiukweli yapo maswali magumu na mazito wana usalama wanapaswa kujiuliza Huyu Mtafiti alikuwa na agenda gani? Na how smart she was to blind the all state. oR Mh Rais ndie alikuwa smart kuona agender ya siri nyuma ya hili tamko?
Nani walikuwa wakwanza kuona madhara ya msg ya huyu mama au Rais ndie alikuwa wakwanza kuona.
Ndugu zanguni sichelei kusema ikiwa yagizani yatawekwa kwenye nuru hili taifa wapo watu inapaswa kupigwa risasi hadharani, ifike mahali watumishi wa serikali na tahasisi zake wawe na hofu kusema kwa niaba ya serikali mambo yanahusu serikali.
Yapo majaribio mengi yamepangwa ila huko tuendapo Tiss lazima wafanye kitu kabla ya jambo halijatokea.
Nitajitaidi next mada kugusia mpango wa kumfanya Mh Magufuli kuwa Rais wa term moja mpango amabo wapangaji wanapanga kwa namna yakushangaza sana ila kama nilivyokwisha wahi kusema mipango yao kuelekea 2020 nikama mvuke sina uhakika wala sidhani kama watafanikiwa.

TUJIFUNZE KWA MATUKIO KAMWE WATU WACHACHE WASIJE KUTUHUJUMU. Mungu ibariki Tz na Rais wetu Magufuli.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,100
2,000
Hili ni zaidi ya somo, kumbe ndani ya serikali mtu anaweza kuibuka nakusoma taarifa amabayo matokeo yake yanaweza kuwa ni janga la taifa. Kiuhalisia hakuna alie juwa Malecela alikuwa kienda kusoma taarifa nzito ambayo uwenda ingweza kwenda kusababisha madhara makubwa kwa taifa.
Hili nijambo la hatari sana na tusikatae vyombo vya usalama vimeona madhara ya watumishi wa seikali kufanya mambo pasipo kutoa taarifa kwa wizara husika.
Ikiwa serikali itaangalia hili jambo kwa jicho la saba unaweza kugunduwa upo udhaifu mkubwa sana ktk utowaji taarifa za serikali, mfano mzuri nikile kitendo cha mh fulani kumchongea mkurugenz mahali ambapo hapakuwa mahali pa kufanya hivyo, pia siku zakaribuni wakurugenz na wakuu wa mikoa wamekuwa na matamko ambayo yanaleta taharuki kwa taifa yote haya ni darasa kwa vyombo vyetu vya usalama.

Nilazima kuanzia sasa kuwe na utaratibu wakuangalia nini nani anasema upo uwezekano mkubwa Mh Ummi alialikwa na Mkurugenz na report alikwenda kuisikiliza protoco kama hizi ni hatari kwa usalama yani waziri anakaribishwa kusikiliza report amabyo hata yeye uwenda hajaiona au kujuwa nini kitasomwa.

TUJIFUNZE KWA MATUKIO KAMWE WATU WACHACHE WASIJE KUTUHUJUMU.
Watu wa aina ya Malecela wanaitwa PROFESSIONAL ECONOMIC HITMAN.Hawa hutumia taaluma zao kuubamiza uchumi chini KWA SIRI na kustukiza.Anatoa news alert ya dakika inauulilia mbali uchumi kwa dakika.Matamko yote mazito inabidi yapitiwe na wizara husika na wizara ya ulinzi.

Nashauri hata kesi kubwa kubwa za uhujumu uchumi si vibaya hukumu zikapitiwa na wizara ya sheria na wizara ya ulinzi kabla ya kusomwa
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,947
2,000
Kwangu Dr Mwele atabakia kuwa SHUJAA siku zote.

Report ya utafiti hutolewa na aliefanya utafiti..

Na siku zote tafiti zinazofanywa kuhusisha jamii ni Mali ya Jamii husika.

Report hii Dr Mwele angewapa serikali mpaka sasa ungekuta serikali ipo kimya na haijawaeleza lolote jamii ya Watanzania.

Hata kama taratibu/protocol inasema alipaswa kuwapa wizara utafiti then waziri ndio atangaze hizi ni protocol za KIJINGA na ambazo haziwezi kutusaidia chochote.

Tusiangalie tu maslahi sijui uchumi utashuka.. Sijui watalii hawatakuja..
Those are cheap arguments..

Uhai ni muhimu kuliko watalii waje waambukizwe ZIKA hapa.

Big up Dr Mwele...
Mungu anakwenda kukufungulia mlango mwingine mzuri zaidi na watawala hawa hawa watakukumbuka.
 
tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,195
2,000
Watu wa aina ya Malecela wanaitwa PROFESSIONAL ECONOMIC HITMAN.Hawa hutumia taaluma zao kuubamiza uchumi chini KWA SIRI na kustukiza.Anatoa news alert ya dakika inauulilia mbali uchumi kwa dakika.Matamko yote mazito inabidi yapitiwe na wizara husika na wizara ya ulinzi.

Nashauri hata kesi kubwa kubwa za uhujumu uchumi si vibaya hukumu zikapitiwa na wizara ya sheria na wizara ya ulinzi kabla ya kusomwa
Watalii wa US na Ulaya tangu mwanzoni mwa 2010s wakitaka kujua taarifa za magonjwa yaliyopo Afrika mashariki including Tanzania, Zika ilikuwemo na walikuwa wanakuja hivyohivyo so nakataa kwamba taarifa hii ya juzi itaathiri utalii unless mtu aje na orodha ya watalii (ikibidi na majina yao) walio-cancel safari zao kwa sababu ya issue hii.
 
WAR

Member
Dec 16, 2016
41
95
Maoni ya kipuuzi hayo.nani anauhakika kuwa wizarani walikuwa hawajui? mleta janga ni yule anayeficha au anayeeleza ukweli? kuficha uovu kwenye.kivuli cha usalama wa taifa vepe? pelekeni ushabiki wa vyama huko Lumumba.
Kwa akili yako unafikili ZIKA ni malaria kwamba kila mtu atatangaza tu, huyo mama alikosea nakulikuwa na umuhimu wakujiridhisha na kushirikisha wizara husika ,angalia impact ya ZIKA wakati Brazil ilipokuwa inaandaa michuano ya Olyimpic najitihada walizotumia katika kuzima vyombo vya habari, maana ilitishia hata kunyang'anywa nafasi ya kuaandaa hiyo michuano
 
Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,555
2,000
Shida
Hili ni zaidi ya somo, kumbe ndani ya serikali mtu anaweza kuibuka nakusoma taarifa amabayo matokeo yake yanaweza kuwa ni janga la taifa. Kiuhalisia hakuna alie juwa Malecela alikuwa kienda kusoma taarifa nzito ambayo uwenda ingweza kwenda kusababisha madhara makubwa kwa taifa.
Hili nijambo la hatari sana na tusikatae vyombo vya usalama vimeona madhara ya watumishi wa seikali kufanya mambo pasipo kutoa taarifa kwa wizara husika.
Ikiwa serikali itaangalia hili jambo kwa jicho la saba unaweza kugunduwa upo udhaifu mkubwa sana ktk utowaji taarifa za serikali, mfano mzuri nikile kitendo cha mh fulani kumchongea mkurugenz mahali ambapo hapakuwa mahali pa kufanya hivyo, pia siku zakaribuni wakurugenz na wakuu wa mikoa wamekuwa na matamko ambayo yanaleta taharuki kwa taifa yote haya ni darasa kwa vyombo vyetu vya usalama.

Nilazima kuanzia sasa kuwe na utaratibu wakuangalia nini nani anasema upo uwezekano mkubwa Mh Ummi alialikwa na Mkurugenz na report alikwenda kuisikiliza protoco kama hizi ni hatari kwa usalama yani waziri anakaribishwa kusikiliza report amabyo hata yeye uwenda hajaiona au kujuwa nini kitasomwa.

TUJIFUNZE KWA MATUKIO KAMWE WATU WACHACHE WASIJE KUTUHUJUMU.
Shida ni kuwa kila mtu ni mteuzi wa raisi
 
Gaspare Mbile

JF-Expert Member
Aug 30, 2016
1,496
2,000
Watu wa aina ya Malecela wanaitwa PROFESSIONAL ECONOMIC HITMAN.Hawa hutumia taaluma zao kuubamiza uchumi chini KWA SIRI na kustukiza.Anatoa news alert ya dakika inauulilia mbali uchumi kwa dakika.Matamko yote mazito inabidi yapitiwe na wizara husika na wizara ya ulinzi.

Nashauri hata kesi kubwa kubwa za uhujumu uchumi si vibaya hukumu zikapitiwa na wizara ya sheria na wizara ya ulinzi kabla ya kusomwa
Mmeshimdwa kujenga viwanda na kutoa ajira sasa mmeanza kumuandama mama wa watu kwa kusema ukweli,kwahiyo kabla ya kauli ya Dkt Mwele uchumi ulikuwa vizuri? Mbona watalii high seasonal wamekuwa wachache nayo imesababishwa na kauli ya huyo mama? Acheni ushabiki usiokuwa na msingi bwana.
 
senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,509
2,000
Hapa nadhani tunapiga chenga tu.Dr.Mwele alikuwa anatafuta uhalali wa kuanzisha mradi wa ZIKA ambapo kitengo hicho kingekuwa chini yake na kingepata ufadhali wa fedha nyingi.Na ninadhani alishasuka mipango na wakubwa juu yake ili kujenga mazingira.Bahati mbaya sana mkuu wa nchi amewazidi mbali sana katika kufikiria.Hali imekuwa ngumu ,wakubwa wanatafuta namna yoyote ile angalau pesa ipatikane.Ninamlaumu saba Dr. Mwele kwani hakufikiria upande muhimu wa usalama wa nchi na uchumi wake.
 
afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Huyo Mwele katika watu wapumbavu hakuna zaidi yake.

Nnashangaa sana alikuwa anafanyaje kazi zake hapo NIMR?

Nnahisi alikuwa ni boya tu hapo na kila kitu kukubali tu ili kuficha u.pumbavu wake.
Naamini unaandika out of your ignorance. Dr. Mwele alikuwa ni Director General wa taasisi ya utafiti wa afya zetu. Ndiye msemaji mkuu wa mambo yote ya taasisi. Alilolifanya lipo katika majukumu yake ya kisheria. Muhimu na kama kweli tunatumia akili, tujiulize kanuni ya kumzuia mtafiti kutangaza matokeo ya utafiti alioufanya mpaka matokeo hayo yafanyiwe sensorship na mwanasiasa ambae si mtaalamu wa kile kilichofanyika. Unatukana matusi badala ya kushirikisha akili yako na vidole unavyotumia kuandikia.
 
Gaspare Mbile

JF-Expert Member
Aug 30, 2016
1,496
2,000
Watalii wa US na Ulaya tangu mwanzoni mwa 2010s wakitaka kujua taarifa za magonjwa yaliyopo Afrika mashariki including Tanzania, Zika ilikuwemo na walikuwa wanakuja hivyohivyo so nakataa kwamba taarifa hii ya juzi itaathiri utalii unless mtu aje na orodha ya watalii (ikibidi na majina yao) walio-cancel safari zao kwa sababu ya issue hii.
Hao watalii safari hii 'high seasonal' wamekuwa wachache kutokana na hizo VAT walizoongeza kwenye huduma mbalimbali za kitalii kwenye bajeti ya 2016/2017 halafu wanaanza kumuadaa mama eti kahujumu uchumi,waliohujumu uchumi ni hao walionunua kivuko kibovu kutoka Denmark kwa mabilioni ya walipa kodi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom