mimi kwa mawazo yangu huyu mama ataungwa mkono na watu wote kwani ana upeo na kipaji cha kuzaliwa, hayupo kwenye siasa za sana na vilevile atakuwepo kwa muda wote wa kamati kwani bado sio mzee na hii kamati inaweza kuchukua muda sana. Cha maana zaidi ni mwanasheria ambaye amesomea katiba na anajua katiba za nchi nyingine kwasababu ametoka un.
ebu kuwa mkweli na hakika na unachoandika. Kwamba ana kipaji cha kuzaliwa kwenye nini? Kwenye siasa si alipewa upendeleo kupitia viti maalumu vya vyuo vikuu? Toka lini amewahi kufanya siasa na kuonekana anaweza? Kuwa mwalimu chuo kikuu siyo kigezo bwana, kwani dr. Bana si senior lecturer udsm? Au prof. Mukandara si ni profesor? Je nini kinaendelea sasa pale udsm na serikali yetu wanayoishauri kupitia nafasi zao redet na kama washauri wa rais? Wewe hauoni kama nchi inamwelemea rais wetu kwa ushauri anaoupata toka kwa watu hao?
Kama ana uwezo na kipaji kikubwa, ni nini kimemshinda un? Je kasi ilikuwa kubwa sana? Kiasi kwamba kwake imekuwa vigumu kuendana nayo? Usilete hoja kwamba un kaacha yeye, hizo ni dhana za kuleta kupoteza hasa kilichotokea un kwa huyo mama. Mama aliomba lkn imeonekana hakuwepo kwenye lon-term plan ya utendaji wa katibu mkuu wa un. Isitoshe hiyo nafasi alipewa kama zawadi tu.
Kama hoja ni kufundisha sheria chuo kikuu hiyo isiwe dhana kwani walimu wako wengi sana na haimaanishi kwamba wote wana vipaji vya hali ya juu ndugu yangu. Wengine ni msuli sana tu ndiyo waweze kuperform, kwani iq zao si kubwa kiivyo. Na wote wakishabaki pale, inakuwa ni vigumu kutambua yupi ni mkali zaidi kuliko mwingine.
Sasa narudi kwenye point; kwenye kamati ya katiba hatuhitaji mtu anayekuja kujifunza siasa na utendaji kwenye public ambaye hana kasi itakayotusaidia sisi watanzania. Kumbuka, watanzania tunahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kasi ya ajabu kuliko hata ya un, kwani kwasasa tz ina hali mbaya sana kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hivyo, kama ameshindwa kasi ya un, then hata tz hatuhitaji mtu kama huyo.