Dk. Mwakyembe mambo mazito: Ripoti ya ugonjwa wake yaivuruga Serikali: Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Mwakyembe mambo mazito: Ripoti ya ugonjwa wake yaivuruga Serikali: Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Jan 11, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  RIPOTI ya ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, imeendelea kuivuruga serikali, safari hii Wizara ya Mambo ya Ndani ikisisitiza kuwa Wizara ya Afya ndiyo inayopaswa kuzungumzia suala hilo.

  Kauli hii mpya toka Wizara ya Mambo ya Ndani imekuja ikiwa ni takriban wiki moja tangu gazeti hili lilipomuuliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, kuhusiana na ripoti hiyo na kusema kuwa suala hilo haliwahusu. Uamuzi wa Tanzania Daima Jumatano kutaka kupata kauli toka Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo kimantiki inashughulikia madai ya jinai ulikuja baada ya kile kinachodaiwa kuwa ripoti ya ugonjwa wa waziri huyo kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya Apollo nchini India ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri, inadaiwa kueleza chanzo cha ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kuwa umetokana na sumu kali aliyowekewa hapa nchini.

  Gazeti hili jana lilimtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, kutaka kupata kauli yake juu ya ripoti hiyo na tuhuma zinazotajwa ambapo alisema mwenye uwezo wa kuzungumzia juu ya ripoti hiyo ni Mkemia Mkuu wa Serikali toka Wizara ya Afya. Alipoulizwa na gazeti hili anazungumziaje juu ya kile kinachodaiwa Dk. Mwakyembe kuwekewa sumu hapa nchini, Waziri Nahodha alijibu kwa sauti kali kidogo: "Aa..ah, sikiliza; wenye uwezo huo nimekwambia ni Wizara ya Afya, mimi kama Waziri wa Mambo ya Ndani kuzungumzia suala hilo ni mpaka niletewe taarifa kama mtu anatuhumiwa kwa sababu wizara yangu inashughulika na kesi za jinai.

  "Sasa sijaletewa taarifa, mimi ripoti siijui, ripoti za afya za watu ziko Wizara ya Afya... hao si ndiyo wanawapeleka watu India?...Sijaletewa ripoti sijaiona na sidhani kama nitalewa," alisema. Alipoulizwa kwa nini anasema hadhani kama ataletewa ripoti hiyo je hakuna taarifa zinazodai kuwa ugonjwa unaomsumbua Dk. Mwakyembe unatokana na sumu? Bado aliendelea kusisitiza kuwa hajapokea taarifa zozote za mtu kutuhumiwa kumuwekea sumu Dk. Mwakyembe na kusisitiza kuwa kama gazeti hili linamfahamu mtuhumiwa huyo basi limtajie. Hata hivyo ingawa taarifa rasmi ya serikali haijatolewa, ripoti ya ugonjwa wa waziri huyo kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya Apollo nchini India ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri inadaiwa kupelekwa serikalini kupitia Wizara ya Afya.

  Taarifa za Dk. Mwakyembe kuwekewa sumu, mara ya kwanza ziliibuliwa rasmi nchini na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni rafiki mkubwa na mshirika wa karibu wa Dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ITV katika kipindi chake cha dakika 45 kilichorushwa mwaka jana. Sitta alisikika akisema kuwa wasiwasi huo wa Dk. Mwakyembe kuwekewa sumu unatokana na mabadiliko ya ngozi na nywele alivyoondoka navyo nchini kwenda India.

  Kwa Mujibu wa Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema alipokwenda kumwona Dk. Mwakyembe nyumbani kwake, alipata mshtuko mkubwa kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza katika umri alionao kushuhudia ngozi ya mtu ikitoa unga. Sitta alikaririwa akisema, "Kuna kitu kama mba kwenye nywele na kwenye ngozi ya Dk. Mwakyembe. Akishika hivi, baadhi ya nywele zinadondoka. Mkono umevimba, sehemu mbalimbali. Mke wake alichukua video. Alikuwa anatuonyesha kwenye laptop (kompyuta ndogo). Kwa kweli inatisha." Hata hivyo, Sitta alihojiwa na polisi kuhusiana na taarifa hiyo kwa madai kuwa ingeweza kuhatarisha amani, lakini alipotakiwa kutoa ushahidi anadaiwa kutoa ushahidi wa habari za kwenye mitandao ya kijamii.

  Kabla ya Dk. Mwakyembe kwenda India kutibiwa, kulikuwa na uvumi kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa kiongozi huyo kulishwa sumu, ingawa yeye binafsi hajakanusha wala kuthibitisha habari hizo. Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aliporejea nchini, Dk. Mwakyembe alisema ripoti ya ugonjwa wake iko serikalini. Hata hivyo, serikali hadi sasa imekataa kuitoa hadharani ripoti hiyo ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Apollo, India, waliomtibu Dk. Mwakyembe. Habari zaidi zinasema kuwa mwanasiasa huyo amepania kuianika ripoti hiyo hadharani kama serikali itaendelea kuifanya kuwa siri.

  Dk. Mwakyembe alipelekwa India Oktoba 9 mwaka jana na kurejea nchini Desemba 11 mwaka jana hata hivyo licha ya kupata matibabu nchini India na kuendelea na tiba hiyo hapa nchini, hali yake bado siyo ya kuridhisha kwani amenyonyoka nywele, kope, nyuzi na hata vinyweleo vyote mwilini.


  Source: Tanzania Daima 11/01/2012

  KITENDO CHA MAAFISA WA SERIKALI KUPISHANA KAULI KINAZIDI KUONGEZEKA KASI SIKU BAADA YA SIKU. WAPEMBUZI WA MAMBO YA KIJAMII WANAJUA MAANA HALISI YA WATU KUPISHANA KAULI NA SABABU YA HIZO SINTOFAHAMU. KAMA ASILI YA UGONJWA WA DK NI SUMU??NINI KIFANYIKE ILI KUBAINI MAHARAMIA WALIOMDHURU DK MWAKYEMBE?

  JE NI WATETEZI WANGAPI WA RASILIMALI YA TAIFA HILI WATADHURIKA KWA UTARATIBU HUU??WAPO WAPI WALE WANAINTELLEJENSIA WETU MAHIRI WA KUZUIA MAANDAMANO YA CHADEMA, WAPO WAPI WALE MAJEMEDARI WA KUSAFIRISHA KWA NDEGE ZA KIVITA VIONGOZI WA CHADEMA KUWAPELEKA MAHAKAMANI KUHUDHURIA KESI??

  MBONA HATUWAONI KAZINI, MMEGOMA KUFANYA KAZI AU BADO MNASUBIRI MAELEKEZO KAMA KAWAIDA YENU?? HIVI NI KWELI MPO KWA AJILI YA USALAMA WA RAIA WEMA AU MNATUMIA HUO KAMA MSEMO KUJUSTIFY MALIPO YA MISHAHARA YENU KUPITIA KODI ZA WANANCHI MASIKINI????INAUMA SAAAANA.

  I STRONGLY BELIEVE KWAMBA IPO SIKU MATESO HAYA YATAKUWA HISTORIA!!!! SUALA LA SIKU HIYO NI LINI NAOMBA NAWAACHIE WANANCHI WAAMUE WAO SIKU WATAYOONA INAFAA KUACHANA NA HAYA MATESO YA KUJITAKIA!

  HIVI KWELI TANZANIA IMAFIKA MAHALI HAPA??? NINI CHANZO!!!

  Mungu akupe nguvu Dk. Mwakyembe, wananchi wengi sana wapo nyuma yako wakikuombea upone maradhi yanayokusumbua. Kwa kuwa repoti ya tatizo lililokupata ni haki yako, wananchi wengi sana wangeshukuru kama ungewajulisha kilichojiri ili tuweze kuchukua tahadhari stahiki na kuweka kumbukumbu vizuri.
   
 2. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  hizi ngonjera zitaisha lini?
   
 3. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Siku pale haki itakapochukua mkondo wake.
   
 4. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ni Tanzania hii hii?Haya wacha tusubiri kama tunavyomsubiri yesu ashuke kwa mara ya pili
   
 5. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Dhulma inapozidi sana huwapata hata wale wasiotarajiwa, Kama waziri mwenye dhamana analishwa sumu Je ni raia wangapi wanaopatwa na visa kama hivi?

  Katika kampeni za Igunga wananchi watano waliuwawa kisa walishabikia chama pinzani, Imran Kombe na wengine wengi wameuwawa sababu hasa ni kukipinga Chama tawala.

  Raia wengi wapo magerezani sababu hasa ni misimamo yao juu ya chama tawala.

  Hali hii mpaka lini sasa? Nani atakaye mtetea mnyonge wa nchi hii kama hata waziri nae anatendwa hivi?

  Tuamueni moja, Huu uonevu na dhulma sasa basi, wahusika wawajibishwe!!
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Watu wanamhurumia Mwakyembe lakini yeye hajihurumii.
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kuna mwanasayansi mmoja hapa JF aliichambua hali ya Dk. Mwakyembe aliyokuwa nayo kabla ya kwenda India.......nafikiri ule uchambuz haijawa disputed hadi leo...........
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Tukumbushe mkuu
   
 9. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Siku tutakapomsindikiza jimboni kwake.
   
 10. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  viongozi watatupiana mpira mwisho wa siku itatupiliwa mbali kilichopo Dr Mwakiembe mwenyewe aisome hadharani wananchi wapate ukweli ilikuwa simu au ugonjwa ya kawaida
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  ...B, Serikali hii taahira haiwezi kumruhusu Mwakyembe azungumzie mwenyewe ripoti hiyo na hao Serikali wanajaribu kila namna ili waizike ripoti hiyo kimya kimya. Ngoja tuangalie hii kasheshe litakuwaje lakini naamini hakutakuwa na chochote cha maana kwa hiyo huyu mlambisha sumu anaweza akamlambisha mwingine tena. Sitta inabidi awe muangalifu sana vinginevyo naye atalambishwa visivyostahili.
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida hili sakata la sumu liliibuliwa humu na kupewa uzito na JB lakini kama kawaida ya magazeti yetu kwa makusudi wanasema eti Sitta ndio aliibua kwa mara ya kwanza! Wakati hata huyo Sitta alipeleka polisi ushahidi wa maelezo ya JB! Kwanini magazeti yanakataa kuipja credit JF? Au ndio lile bifu la magazeti kudoda maana wasoma magazeti wakubwa wameacha kununua sababu kila kitu kinapatikana hapa!
   
 13. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  unachosema ni kweli serikali haiwezi kukubali Dr kuitoa hadharani kama kweli inamkono wa mtu
  viongozi wa nchi hii ni zaidi ya tunavyowajua.
   
 14. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,312
  Trophy Points: 280
  Namkumbuka Jason Bourne na ile issue yake ya LTK
   
 15. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  wenye nayo waiweke hapa.
   
 16. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hakunaga siri humu duniani hiyo ripoti ipo siku 2 itatoka kwa wananchi whether akiwa hai au hayupo,shame on the government,
   
 17. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama Mwakyembe mwenyewe anayo basi watu wataipata tu.
   
 18. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  hebu iweke tuisome (kama haitaondolewa!!)
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwanini aliisoma nusu report ya Richmond bungeni?
   
 20. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mwakyembe keshajifia, kosa kubwa atakalofanya ni kutotoa ripoti hadharani kama alivyoficha baadhi ya mambo ya Richmond ambayo hata leo akiyatoa hakuna atakayeyaamini kwa asilimia mia. Aseme kitu gani kinamsumbua, anahusika, na kwanini kafanyiwa hivyo. La sivyo tutaishia kuwa na story za akina Balali tu.
   
Loading...