Dk. Mwakyembe: Katiba inampa mamlaka Rais Kuteua na Kutengua Atakavyo

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,659
2,822
Waziri wa Katiba na Sheria, Dokta HARRISON MWAKYEMBE, ametoa ufafanuzi kuhusu uteuzi wa Rais JOHN MAGUFULI wa Wabunge Wawili, pamoja na Naibu Waziri kuteuliwa kuwa Balozi, huku akisisitza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano haijakiukwa.

Akizungumza na Uhuru Fm, Waziri MWAKYEMBE, ameshangazwa na baadhi ya watu kushutumu teuzi hizo za Wabunge wa kuteuliwa alizofanya Rais, huku akisema Katiba ya Nchi inampa nafasi Rais kuteua na kutengua nafasi ya mtu yoyote aliyemteua.

Amesema ni vema watanzania wakamuacha Rais afanyekazi zake ikiwemo kufanya teuzi kwa kuwa yeye ndiye anaona mtu gani anafaa wapi na nani amteue kwa wakati gani.

Jana jioni, Rais JOHN MAGUFULI, amemteua Dokta ABDALLAH POSSI kuwa Balozi, ambaye Kituo chake cha kazi na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadae.

Kabla ya uteuzi huo Dokta POSSI alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu aliyekuwa akishughulikia Ulemavu.

Kwa mujibu wa Waziri MWAKYEMBE, Ubunge wa Kuteuliwa wa Dokta POSSI unakoma kufuatia uteuzi huo wa kuwa Balozi.
 
=====
Hivi kama iko hivyo asemavyo Mwakyembe, kwa nini tuwe na katiba? Kwamba Rais ana uhuru wa kufanya atakavyo; ndiye anayejua nani anafaa, nani hafai, n.k. Katiba ya nini? Hivi wanasheria kama Mwakyembe wakisema hivyo, sisi wana sharia wa vichakani tuseme nini? Na tangu lini tumekubali kupalilia huu umungu mtu? Mimi sidhani kama hata rais mwenyewe anapenda atukuzwe hivi. I doubt.
 
katiba inampa mamlka hayo kuu ,ndio maana katika katuba ya warioba mamlaka ya rais yalipunguzwa
 
=====
Hivi kama iko hivyo asemavyo Mwakyembe, kwa nini tuwe na katiba? Kwamba Rais ana uhuru wa kufanya atakavyo; ndiye anayejua nani anafaa, nani hafai, n.k. Katiba ya nini? Hivi wanasheria kama Mwakyembe wakisema hivyo, sisi wana sharia wa vichakani tuseme nini? Na tangu lini tumekubali kupalilia huu umungu mtu? Mimi sidhani kama hata rais mwenyewe anapenda atukuzwe hivi. I doubt.
Si amesema KATIBA ya nchi inampa mamlaka hayo...?!
 
Back
Top Bottom