Dk. Mwakyembe Huku Namna Gani?


K

K-Boko

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Messages
700
Likes
7
Points
35
K

K-Boko

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2013
700 7 35
Kumekuwa na juhudi kubwa za kuboresha miundombinu nchini. Majuzi JK ametangaza ujenzi wa reli mpya (standard gauge) katika reli ya kati (Dar-Tabora-Kigoma/Mwanza). Cha kushangaza ni kwamba reli ya Dar-Korogwe/Tanga/Moshi haizungumzwi kabisa. Hii ndio reli iliyokuwa ikiunganisha reli ya kuingia Kenya kupitia Taveta. Tunajua kuna suala la vipaumbele vya kiuchumi, lakini baadhi yetu tunajua ni jinsi gani reli hiyo ilivyokuwa mkombozi wa usafiri na kiuchumi kwa wananchi wa maeneo inakopita. Mbaya zaidi ni kwamba maeneo mengi inakopita reli hiyo hakuna barabara za maana. Dk Mwakyembe mbona mko kimya kuhusu ufufuaji wa reli hii? Endapo waziri yumo humu au wadau wengine wenye ufahamu (current) wa suala hili watujuze!
 

Forum statistics

Threads 1,272,651
Members 490,095
Posts 30,456,080