Dk. Mwakyembe awapa polisi siku 14 kuwataja polisi wezi wa mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Mwakyembe awapa polisi siku 14 kuwataja polisi wezi wa mafuta

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 25, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Richard Kilumbo, Kyela na Elias Msuya | Mwananchi

  WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe, amewashukia polisi nchini kwa kuendelea kufubia macho vitendo vya uhalifu na kuahidi kuchukua mkondo mpya kukabiliana na vitendo hivyo.

  Akizungumza katika ibada maalumu ya shukrani iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Kanisa la Nduli lililopo Ikolo, Kijiji alichozaliwa, Dk Mwakyembe alimtaka Kamanda wa Kanda Maalumu Dar es salaam, kuyaweka wazi majina ya askari wote walioshiriki katika wizi wa mafuta bandarini vinginevyo atahakikisha sakata hilo linakwenda mbali zaidi.

  Dk Mwakyembe ambaye alitumia muda mwingi kuelezea matukio aliyokumbana nayo kuanzia mwaka 2009, alitoa muda wa wiki mbili kwa polisi kuwataja askari waliohusika na wizi huo vinginevyo alitishia kulifikisha katika ngazi za juu ili wahusika wake wachukuliwe hatua.

  “Kamanda Kova ana muda wa wiki mbili kushughulikia suala hilo, kabla ya mimi kulifikisha suala hilo ngazi nyingine ili askari hao waweze kuchukuliwa hatua za kisheria badala ya kuendelea kuwakumbatia askari wasio waadilifu na wanawachafua polisi wema”,alisema Dk Mwakyembe.

  Kuhusu misukosuko aliyokumbana nayo pamoja na ugonjwa wa ajabu uliopata hivi karibuni, Dk Mwakyembe alisimulia mlolongo wa matukio kadhaa likiwamo la ajali aliyoipata mkoani Iringa wakati akiwa safarini.

  “Mwaka 2009 nilipata ajali mbaya kati ya Makambako na Iringa mjini, kitu ambacho sitokisahau milele ni kwamba niligongwa na lori,” alisimulia.

  Alisema pamoja na tukio hilo na matukio mengi mengine yaliyomwandama na kuyaripoti polisi, lakini amekuwa akishangazwa na watendaji wa polisi kwa kuyasemea matukio hayo pasipo kuyafanyia uchunguzi jambo ambalo limekuwa likimkera na kupoteza imani.

  Alisimulia mikasa inayomwandama alikisema aliandaliwa mpango wa kuuawa kati ya Iringa na Mbeya na aliyepangwa kumuua ni mhalifu sugu, lakini Mungu alijiinua. Muuaji alimfuata akamwambia unaenda safari ya Kyela, usiende, ukienda nitakua,” alisimulia Dk Mwakyembe akiacha watu wamepigwa butwaa.

  Alisema ajali ilikuwa mbaya na ilipangwa na kwamba lakini cha ajabu hata polisi waliofika eneo la tukio walikata tama ya kunipeleka hospitali.

  Alisema aliokolewa na kwa mujiza ya Mungu kwani aliojitokeza Mkurugenzi wa shule za sekondari na vyuo katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Mboka Mwambusi, ndiye alilazimisha ampeleke hospitali.

  “Aliyenichukua pale alinieleza kwamba polisi aliyemkuta alisema Dk Mwakyembe alikuwa amefariki dunia lakini yeye alinisisitizia kuwa kunipeleka hospitali”alisema.

  Akifafanua kuhusu vitisho vya kuawa alisema muuaji huyo alimweleza mpango mzima wa mauaji ulivyopangwa na kumpa uhuru wa kumrekodi maelezo yake, ambayo ameyahifadhi hadi leo.

  Alisema katika matukio yote yaliyomsibu ndani ya miaka mitatu, Dk Mwakyembe alikuwa akiwaarifu polisi, lakini hawakuchukua hatua zozote zaidi ya kuendesha juhudi za kuficha ukweli.

  Kuhusu ugonjwa wake alisema nayo ni utata mtupu kwani katika mazingira ya kushangaza kumekuwapo na juhudi za kuupotosha umma.

  “Mwaka 2011 niliugua, cha kusikitisha niliugua wakati huohuo na kaka yangu, Profesa Mark Mwandosya, Mungu ni mwema, alitunyanyua vitandani, leo tunatembea, mimi na kaka yangu Mwandosya ni ushahidi juu ya utukufu wa Mungu,” alisema Dk Mwakyembe.

  “Daktari aliyenitibu aliniambia, amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 27, hakuwahi kuona ugonjwa wa aina ile,” alisema Dk Mwakyembe.

  “Sitta alipofika kuniona, nilisikitika sana kwa nini alikuja, ndio maana aliporudi alikuja na kilio kwa polisi akiwataka wachunguze, wakamgeuzia kibao, walisau kuwa Sitta ni Mwanasheria aliyebobe.”

  Katika ushuhuda wake, Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, alihitimisha kwa kuhoji “Mungu hapendi uongo, na ukweli hauna tabia ya kujificha, ipo siku utadhihirika, ikiwa polisi walikuwa wanachunguza ugonjwa uliomsibu Dk Mwakyembe, kwa nini hawakwenda kwenye hospitali aliyokuwa akitibiwa?” alihoji.
   
 2. n

  nndondo JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe mwakyembe unataka kumchezea nani hapa, unafikiri matanzania wa leo ni mabwege wale mliokua mnawachezea kwenye kazi zenu za usalama? hivi inakuingia kichwani mtu aliyetaka kuuawa kwa kipindi cha miaka mitatu katika misa yake ya shukurani, tena kijijini kwao, anatoa wito wa kuwatafuta polisi wa mafuta? shenzi kabisa, yaani sio wauaji wako, kama kweli na kama wapo? see, peleke ukonyofu wako huko, hao wauaji uliotangaza kuwataja ukiwa India? magonjwa yenu mnajua mlikoyatoa mlikolalalio ndio wenzenu tulikoamkia myeka
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe acha unafiki..ushapewa uwaziri endelea kupiga kimya tu mshenzi mkubwa wewe..ulituambia hukusema yote juu ya richmond ili kuilinda serikali ya ccm je mungu anapenda unafiki huo, je unajua leo watanzania tunatakiwa kuwalipa kiasi gani hao richmond..wewe,mark, sitta ni wanafiki tu wachumia matumbo..
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,421
  Likes Received: 19,731
  Trophy Points: 280
  mwakyembe again? Kuhusu suala la ugonjwa sichangii kitu ila kuhusu hao polisi waonyeshe jinsi ya kufanya kazi kwani wamezoea sana kukumbatiwa
   
 5. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Dr. Mwakyembe pia awadhibiti na hao wanasimamisha mabasi njiani na kudai rushwa bila kuangalia usalama wa wasafiri.
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  ni aibu kwa serikali kuwa na double standard
   
 7. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Hapo kwenye nyekundu ndo tatizo kubwa lililopo katika Jeshi la Polisi. IGP Mwema amekuwa mzuri mno katika kulinda makamanda wake wazembe. RPC akifanya vizuri haraka haraka ana muhamishia makao makuu, wanaoboronga na kutoa mgao wanapelekwa mikoa mingine. Mfano Kamuhanda aliua Songea akasogezwa Iringa.

  Kasababisha mauaji ya Mwangosi bado anamkumbatia tu. Afande Sillo aliokoa maisha na mali za wana Mwanza aka hamishwa kupelekwa Makao Makuu, OCD Nyamagana aliweza kudhibiti ujambazi na kuepusha mauaji ya kisiasa hasa kutoka amri za magamba , Mabina na wenzake akaambulia uhamisho wa kwenda Bahi...

  Ukiuliza utaambiwa ni uhamisho wa kawida tu katika jeshi. Mwema kwa kuwa aliua mahabusu Mbeya na kuwa IGP haoni soni pale maisha ya mtanzania yanapo potea isipokuwa pale magamba wanapo guswa...He should leave the post
   
 8. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Unajuaeeeh? Mimi nafurahi kwamba polisi hao hawana ubaguzi katika kutenda dhuluma zao. Labda kwa uchochoro huo wanaotuongoza watajua kwamba hatuishi mbingu tofauti na wao, hata wao wakilengwa na mapolisi watakamuliwa kamasi kama sie tu. Sina urafiki wa kweli na mapolisi.
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  Duh mtu aliyewahi kuchungulia "MAUTI" huwa si mwoga wa mauti............safi sana mwakyembe........
   
 10. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Hivi Mwakyembe ni CDM? Baada ya JK kung'atuka madarakani, mengi yatafichuka.
   
 11. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,075
  Likes Received: 4,658
  Trophy Points: 280
  TATIZO KUBWA NI MWAKYEMBE MWENYEWE......

  --- Tz nchi ya waoga sana duniani -----

  ... Mwakyembe kuhusu la Bandari uko right...

  Mwakyembe anasahau sana,

  1: Case 1: Richmond >>
  ULISEMA UTASEMA MENGI ULIYOYAACHA KUOKOA SERIKALI, meaning kuna makubwa machafu uliyaacha
  kusema na wakikutibua UTASEMA, ukakaa kimya UNATISHIA, utasema,utasema
  ukakoswa ajalini, Mungu akakuokoa

  2: Case 2: Ajali >>
  LEO UMESEMA MUUAJI/ Killer alikuambia atakuua, NA
  UNAMJUA, meaning hata aliyemtuma unamjua, unasema umemrekodi, meaning una ushahidi, tena ww ni mwanasheria mwalimu, you have all in all Mwayembe, ila umekaa na KUTISHIA UTASEMA UTASEMA, huku husemi

  3: UGONJWA wako >>

  UKASEMA ni siri ya mgonjwa na Daktari, na uvumi mkubwa ukazagaa umepewa SUMU, umekaa kimya...
  Ulivyotoka India UKASEMA MJADALA WA AFYA YAKO
  UMEFUNGWA RASMI, hutaki kusikia mtu akiongelea, ni lako, sasa mbona unajichanganya, leo mbona unaliongelea publicly, are u ok, sir..??? Nakuheshimu & i luv u Mwakyembe, ila huna msimamo, muoga & huku ww ni msomi mzuri... I doubt ur memory status by the time being....!!! Ni vipi Mwakyembe...!!

  ACHA KUTISHIA, watakuumiza, SEMA KILA KITU, ukweli uwe wazi, itakuwa funzo,
  Dr. Ulimboka naye kimyaaaa, the same story.....
  Hivi mtu ULISHAKUFA 90%, ukapona, unaogopa nn
  kusema yote, we are tired....

  HUU NI UOGA, COWARDNESS ya hali ya juu......

  Habari ya Mwakyembe sitaki kusikiliza tena.....

  --- We are tired with these CHINESE MOVIES LIKE ----
   
 12. G

  Gene Senior Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naomba na wewe yakukute siku moja......
   
 13. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hakuna double Standard hapa Mkuu, kama wao walikuwa wametumwa tu, ni nani wa kuwachukulia hatua.
   
 14. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alishatulizwa kwa kupewa uwaziri, hatawataja tena
   
 15. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Yeye mwenyewe mbona hakuwataja walimuwekea sumu? kama kiongozi aonyeshe mfano yeye kwanza au ndio aliuza utu wake kwa Uwaziri
   
 16. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Polisi wa tanzania wawa wezi wa mafuta, haohao ndio wauwaji wa wananchi haohao ndio wala rushwa kupindukia ....unategemea ipo siku watakaa ofisini kufanya kazi walizoajiriwa?
   
 17. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Mr. President Mijitu mingine ni minafiki ya kupindukia...ameshidwa kufikisha malalamiko yake ya kutaka kuuwawa ngazi za juu anashupalia hili la bandari...hivi wewe mzee akili yako iko sawa kweli!?,afya yako na hilo la bandari lipi limetangulia!?...anyway hilo la bandari sawa likomalie lakini kumbuka kuwa watanzania bado tunataka kujua ukweli kuhusu afya yako,1.nani huyo alitaka kukuuwa?,2.nani alikuwekea sumu...kuhusu Richmond,labda uwe ameshakufa lakini kama utakuwa hai pindi serikai makini itakapoingia madarakani utasema tu ukweli utake usitake...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. a

  artorius JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tukisema serikali ya ccm imefika mwisho tunajibiwa tutakufa sisi tuiache,sasa let's all stay focused and watch this delicious thrill as it unfolds
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,442
  Likes Received: 5,695
  Trophy Points: 280
  Mh mwakyembe amesema kama mh igp mwema na kova amtowataja hadharani wahusika wa wizi wa mafuta bandarini na kuwashugulikia basi kazi hiyo nitaifanya baada ya wiki mbili na kuweka hadharani
  siwezi kuona wezi wahalifu na ni polisi wa kulinda raia leo wanakumbatiwa kama watoto wa changa alilalama mh mwakyembe...


  Ndugu zanguni nawambia sipepesi macho wala kumumunya mdomo nimewapa igp wiki mbilia ama awataje hadharani na kusema wamechukua hatua gani kama wataendelea kuwakumbatia kama wauwaji wengine wa mikoani basi mimi nitakuwa wa kwanza kuwataja na siogopi kufa walitaka kuniua siku nyingi mungu akanipitisha kwenye moto wa daniiel..sasa basi naawaambieni ujing mliokuwa mkifanya zamani sasa basi tunataka kazi kama mmeiba amjafanikiwa sahauni kuiba tena ...nitapiga kazi nitakaa na wale wanaotaka kufanya kazi tu alisema hon mwakyembe
   
 20. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Hii ni kujitafutia tu political mileage, hamna lolote. Tumeshazoea hizi kauli.
   
Loading...