Dkt. Mpango: Mkandarasi wa Bwawa la Nyerere Hana Uzoefu, pia mradi upo nyuma ya muda

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Wakati akitoa maelekezo alipotembelea mradi wa kufua wa umeme wa stiglers gorge , Mh. Mpango alipongeza kwa kazi nzuri unayoendelea na kuongea mengi yakiwemo

1. Mkandarasi Hana Uzoefu wa kutosha katika ufanyaji wa kazi zake huku akisema kwasababu anatumia subcontractor kwa karibu kazi zote kila sehemu. Serikali labda ilitaka mkandarasi mkuu afanye kazi zote peke yake, lakini sehemu nyingi ameweka wachina

2. Mkandarasi yupo nyuma ya mpango kazi, na kwamba amechelewa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mafuriko na uvico19. Kauli ambayo Kalemani amekuwa akitudanganya kuwa tupo mbele ya muda na maji yataanza kujazwa Mwezi wa 11 tarehe 15, na kuwasha mitambo June 2022( KAULI AMBAYO NI DHAHIRI ALITUDANGANYA NA ILIKUWA YA KISIASA) Laini Makamu wa Rais ameongea ukweli.

Kutokana na Kauli ya Mh. Makamu wa Rais ni DHAHIRI kuwa Mradi huu hautaweza kukamilika 2022 Wala 2023 Wala 2024 labda 2025.
 
Tanzania ni zaidi ya uijuavyo...

Kwahiyo, kwa lugha inayoeleweka, Mkandarasi HANA SIFA za kupewa hiyo kazi lakini serikali ya Rais Mtukufu bado ikatoa kazi kwa Mkandarasi asiye na sifa!

Yaani, kwa maana nyingine tulimpa kazi Middle Man...

Na pesa anapewa Middle Man

Middle Man anachukua chake, na kinachobaki anawapa subcontractors wanaofanya kazi yenyewe!!

Yaani ni sawa na mtu unampa kazi Civil Contractor akujengee mjengo halafu nae ana-subcontract kila idara including civil works!
 
😁😁😁
Q0f.jpg
 
Kwahiyo ndio Mpango wa kufifisha ujenzi wa bwawa hilo umeanza? Kisha watasema kasma hamna, kisha Mwezi wa kwanza na genge lake lote la msoga watasema tununue umeme wa dharula, paaap wamerudi, kazi inaendelea!

Eti mkandarasi hana uzoefu, kabla ya hii ziara, kuna ziara ya viongozi wastaafu ilitangulia eeenhe?
 
Hapa ndipo nategemea waziri ajiuzulu kwa kutudanganya kila kukicha juu ya maendeleo ya bwawa, tatizo utaona wala hawajibiki kwa namna yeyote, tabia hii ipo hadi kwa waziri wa afya pia alipaswa ajiuzulu kuipa nguvu kampeni ya Covid-19, uwepo wake baadhi ya watu hawamwamini kwani alipinga chanjo kipindi cha nyuma, sasa anageuka eti inafaa,!
 
Wakati akitoa maelekezo alipotembelea mradi wa kufua wa umeme wa stiglers gorge , Mh. Mpango alipongeza kwa kazi nzuri unayoendelea na kuongea mengi yakiwemo
1. Mkandarasi Hana Uzoefu wa kutosha katika ufanyaji wa kazi zake huku akisema kwasababu anatumia subcontractor kwa karibu kazi zote kila sehemu. Serikali labda ilitaka mkandarasi mkuu afanye kazi zote peke yake, lakini sehemu nyingi ameweka wachina
2. Mkandarasi yupo nyuma ya mpango kazi, na kwamba amechelewa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mafuriko na uvico19. Kauli ambayo Kalemani amekuwa akitudanganya kuwa tupo mbele ya muda na maji yataanza kujazwa Mwezi wa 11 tarehe 15, na kuwasha mitambo June 2022( KAULI AMBAYO NI DHAHIRI ALITUDANGANYA NA ILIKUWA YA KISIASA) Laini Makamu wa Rais ameongea ukweli.

Kutokana na Kauli ya Mh. Makamu wa Rais ni DHAHIRI kuwa Mradi huu hautaweza kukamilika 2022 Wala 2023 Wala 2024 labda 2025.
Ohooo ,niliwaambia hii miradi ya mfukoni ,, mkandarasi aliletwa na Sukuma gang Ili wapige pesa ndio maana akina Kalemani walikuwa wanajitahidi kuficha taarifa nk..

Eti na yule Kadogosa alitaka yule mkandarasi wao wa yep Markez apewe tenda bila ushindani.

Mama fukuza hiyo miradi ina upigaji wa kutisha na fukuza watu wa Mwendazake wote.
 
Mmmhhh..!! Mh. Mpango anasema mkandarasi hana uzoefu wa kutosha? Sasa alipewaje kazi? Kama ni sub-contractor na hana uzoefu wa kutosha, atajenga ktk viwango vya kimataifa kweli Bwawa letu la umeme? Au ndio mwanzo wa figisu?
Mpango si alikuwa waziri wa Fedha na alikuwa mstari wa mbele ktk ujenzi wa bwawa hili na bungeni alitetea sana, kama mkandarasi hana uzoefu kwa nafasi yake akiwa waziri wa fedha alishindwa nini kusema haya leo anayosema mapema?
 
Yap wa sgr na huyu Arab contractor ni wakandarasi wa ten percent wa kundi la mwendazake
 
Mkandarasi wa miradi mikubwa kama hiyo anashinda tender kutokana na design yake ya mradi wote kuanzia physical project, ulinzi wa mazingira kama ecosystem, namna ya kuvuta maji and so forth with hydro power project scope.

Anakupa na costs zake za kujenga mradi, work break down structure ya wewe kuweza kufuatilia progress ya mradi kwa makubaliano ya muda wa kazi, etc.

Kazi yenyewe inafanywa na sub-contractors anachosimamia mkandarasi na ku coordinate hatua za kazi, kuangalia quality ya kazi, time, anapanga critical path ya mradi na other supervision roles.

Mtu kama makamu wa raisi awezi kwenda kwenye mradi kama huo bila ya mshauri wa maswala ya project management; hivi mbona tunaviongozi waropokaji halafu wepesi sana vichwani ukiwasikiliza.

Au anadhani huu sawa na miradi wa kujenga barabara. Yaani nchi inaviongozi wa ovyo kweli.
 
Back
Top Bottom