Dk. Mpango akunjua makucha aivaa Wizara ya Nishati kusuasua kwa mradi wa umeme

juma30

Senior Member
Jun 25, 2022
149
421
Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdori Mpango amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Gridi ya Taifa katika Mkoa wa Katavi na kuiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha ifikapo 2023 mradi uwe umekamilika na hataki kusikia kiswahili wala kisingizio anataka Mkoa wa Katavi uwe umeunganishwa na umeme.

“Oktoba 2023 sitaki Kiswahili, sitaki kisingizio Mkoa wa Katavi uwe umeunganishwa na Gridi ya Taifa nafikiri tumeelewana, napenda niseme kwa uwazi kabisa sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa huu mradi wananchi wa wa Katavi wamesubiri umeme muda mrefu” amesema Dk. Mpango

SOURCE: ITV

Huyu aliyepewa hii Wizara sijui ana nia Gani na hii Nchi.

Anagawa mitungi ya Gesi badala ya Kuimarisha Umeme ili apunguze Bei na uwe mbadala wa gesi.

Tunakomaa kujenga SGR wakati Umeme siyo wa Uhakika.

NB:
January ni kama ana hisa pale Taifa Gesi. Anawapa Watu Bure ili ikiisha waanze Kununua hiyo Gesi. Hii ni Marketing Strategy ya Kukuza kipato Cha Taifa Gesi.
 
“Oktoba 2023 sitaki Kiswahili, sitaki kisingizio Mkoa wa Katavi uwe umeunganishwa na Gridi ya Taifa nafikiri tumeelewana, napenda niseme kwa uwazi kabisa sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa huu mradi wananchi wa wa Katavi wamesubiri umeme muda mrefu” amesema Dk. Mpango
Tulizoea kusikia "...ndugu zangu wapinzani wametuchelewesha sana"
 
Dk Mpango endelea kukunjua makucha kweli kweli fuatilia mambo yote yanayolalamikiwa kwenye Wizara ya Nishati usiishie huo mradi wa Katavi
Nadhani akijikita huko, na siyo maswala ya umeme pekee, bali katika mirandi mingine yote atakuwa anajenga bila kuonekana kukanyaga siasa zilikolalia.

Ninamsihi sana aliwekee msisitizo sana hili. Hii ni kazi inayoeleweka, na matokeo yake yatakuwa rahisi kuonekana kwa watu wote.
 
Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdori Mpango amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Gridi ya Taifa katika Mkoa wa Katavi na kuiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha ifikapo 2023 mradi uwe umekamilika na hataki kusikia kiswahili wala kisingizio anataka Mkoa wa Katavi uwe umeunganishwa na umeme.

“Oktoba 2023 sitaki Kiswahili, sitaki kisingizio Mkoa wa Katavi uwe umeunganishwa na Gridi ya Taifa nafikiri tumeelewana, napenda niseme kwa uwazi kabisa sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa huu mradi wananchi wa wa Katavi wamesubiri umeme muda mrefu” amesema Dk. Mpango

SOURCE: ITV

Muulize na hiyo mitungi ya Rostam Aziz anayogawa huko Kanda ya Ziwa vipi geni ikiisha watajaziwa na nani?
 
Nilishafurahi kuwa Bwawa la Nyerere kumbe sivyo!!

Siku bwawa la Nyerere likikamilika nitafurahi sana!!
 
Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdori Mpango amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Gridi ya Taifa katika Mkoa wa Katavi na kuiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha ifikapo 2023 mradi uwe umekamilika na hataki kusikia kiswahili wala kisingizio anataka Mkoa wa Katavi uwe umeunganishwa na umeme.

“Oktoba 2023 sitaki Kiswahili, sitaki kisingizio Mkoa wa Katavi uwe umeunganishwa na Gridi ya Taifa nafikiri tumeelewana, napenda niseme kwa uwazi kabisa sijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa huu mradi wananchi wa wa Katavi wamesubiri umeme muda mrefu” amesema Dk. Mpango

SOURCE: ITV

Umeingia huko ndugu Philip, utajibiwa una "NONGWA"
 
Dk Mpango endelea kukunjua makucha kweli kweli fuatilia mambo yote yanayolalamikiwa kwenye Wizara ya Nishati usiishie huo mradi wa Katavi

Hicho cheo ni ceremonial zaidi, hana power yoyote ya kuagiza jambo na likatekelezwa. Labda aagize polisi kukamata wapinzani.
 
Nilishafurahi kuwa Bwawa la Nyerere kumbe sivyo!!

Siku bwawa la Nyerere likikamilika nitafurahi sana!!

Kama wanasisitiza hayo mabwawa madogo, ujue hilo la Nyerere itakuwa si leo wala kesho.
 
Back
Top Bottom