Dk Mkumbo:Tuchukue hatua, taifa limo katika mtikisiko wa elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Mkumbo:Tuchukue hatua, taifa limo katika mtikisiko wa elimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Jun 27, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Dk Mkumbo:Tuchukue hatua, taifa limo katika mtikisiko wa elimu
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 20 June 2011 21:12
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Dk Kitila Mkumbo

  TAKWIMU zinaonyesha kutoka mwaka 2008 hadi 2010, zaidi ya nusu ya wahitimu wa kidato cha nne wamekuwa wakifanya vibaya kwa kupata madaraja ya nne na sifuri.

  Kama haitoshi, masomo ya sayansi na hesabu yameendelea kuwasumbua wanafunzi wengi, jambo linaloweka rehani jitihada za serikali na wadau kuongeza wataalamu wa fani hizo ambao ni muhimu katika maendeleo ya nchi.

  Dk Kitila Mkumbo, Mkuu wa Idara ya Saikolojia ya Elimu na Masomo ya Mitalaa ya Shule Kuu ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anazungumzia sababu zinazoitikisa sekta ya elimu nchini kama alivyohojiwa na mwandishi wetu Gedius Lwiza.

  Swali: Nini maoni yako kuhusu jitihada zinazoendelea kuhakisha elimu inayotolewa nchini inakuwa bora?
  Jibu: kwa hali ilivyo sasa, elimu bora ni ndoto na hali ni mbaya kadiri siku zinavyosonga mbele.Tutegemee miujiza gani katika harakati za kupata elimu bora ikiwa wahusika kila wanapoambiwa, wanalichukulia kama suala kawaida? Kwa hali hii ni dhahiri kuwa taifa linaelekea kubaya.

  Swali: Umesema hali ni mbaya, lakini hivi mnawashirikisha viongozi mnapofanya tafiti na kubaini changamoto katika shule hasa zile za umma?
  Jibu: Tunawafahamisha, lakini hali ya kusikitisha ni kwamba, wahusika wamejikita katika siasa zaidi na ndio maana wanashindwa kuzisaidia shule za umma.Hali ni mbaya katika shule za kata, ni kwa sababu hii, viongozi hawataki kuwapeleka watoto wao katika shule hizi. Wengine wanawapeleka watoto nje ya nchi.

  Swali: Kama hali iko hivi, nini mustakbali wa elimu yetu?
  Jibu: Ukweli ni kwamba kwa sasa nchi iko kwenye mtikisiko mkubwa wa elimu, kutokana na kitendo cha serikali kuamua kudharau mtihani wa kidato cha pili ambao ulikuwa muhimu.

  Ukitoa marufuku ya mtihani huo iliyowafanya wanafunzi kuwa wazembe, maendeleo ya elimu yanakwamishwa na kuwapo kwa mazingira mabovu shuleni ikiwa ni pamoja na uhaba wa walimu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

  Jambo jingine linaloonekana kuwa hatari katika siku zijazo, ni kitendo cha kuwatumia walimu ambao hawana sifa katika ufundishaji. Matokeo yake ni kuendelea kuwalaumu walimu wakati wanaotakiwa kulaumiwa ni wale wanaoruhusu kuwatumia walimu wasiokuwa na sifa.

  Swali: Wadau wengi wanataka kurejeshwa kwa mtihani wa kidato cha pili na ule wa darasa la nne, nini umuhimu wa mitihani hii katika mfumo wetu wa elimu?
  Jibu: Unajua mtihani ni kipimo muhimu kwa mwanafunzi kuweza kufahamu kama amefanikiwa kuelewa mambo aliyofundishwa au la.Mitihani huwapa wanafunzi ari katika kujisomea.

  Kitendo cha kuondoa mtihani huo ni sawa na utovu wa nidhamu shuleni, maana mtihani huo ulikuwa unamjenga mwanafunzi kuwa na utayari wa kufanya mtihani na kuacha uzembe akiwa shuleni. Hivi sasa wanafunzi wana hali mbaya kwani wameanza kuwa wavivu

  Swali:Uhaba wa walimu umekuwa changamoto kubwa nchini kwa miaka mingi. Kwa nini shule zikose walimu ilhali maelfu ya wanafunzi wa ualimu wanahitimu kila mwaka vyuoni?
  Jibu: Sikubaliani na kauli kuwa kuna ukosefu wa walimu. Walimu wapo wengi na kila mwaka vyuo vikuu vinatoa maelfu ya walimu, lakini sababu kubwa inayowakimbiza ni kuwapo kwa mazingira mabovu ya kufanyia kazi. Ni kwa sababu hii, wanaamua kufanya kazi tofauti na ualimu.

  Unajua hakuna mtu ambaye hataki kufanya kazi katika mazingira bora na maslahi bora. Ukitaka kuamini nenda katika shule binafsi, utaona miujiza kwani kila kitu kipo kuanzia maabara, maktaba na walimu.
  Kwa nini matatizo yapo katika shule za serikali peke yake? Ni wazi serikali ikiamua shule za kata nazo zinaweza kuwa kama hizi binafsi.

  Swali: Lakini ualimu ndio fani waliyoisomea tena baada ya kuichagua wao wenyewe?
  Jibu: Unajua kwa sasa, wengi wanaichukulia fani ya ualimu kama njia ya kupita hasa walimu wa sayansi. Walimu wa sayansi kwa mfano, wanapata asilimia 100 ya mkopo, kwa hiyo baada ya kumaliza masomo yao wanakwenda kufanya kazi katika shule binafsi au kazi zingine tofauti na ualimu.Pia ukumbuke watu waliosoma sayansi wana nafasi kubwa katika soko la ajira.

  Shule zinakosa walimu wa sayansi kwa sababu kila mtu anaposoma fani fulani, anahitaji fani hiyo aifanye kwa vitendo. Lakini, kitendo cha mwalimu aliyesoma sayansi kumpeleka katika shule ambayo haina maabara pamoja na vifaa vyake ni sawa na kumharibia utaalamu wake

  Swali: Kwa nini shule za vijijini zinafanya vibaya zaidi kuliko zile za mijini?
  Jibu: Shule kuwa kijijini sio sababu ya kuwafanya wanafunzi wafeli, bali shule za serikali zimetelekezwa na walimu wanaotegemewa, wametupwa huko bila kupewa vitendea kazi. Pia wanapewa maslahi duni.

  Kuna utafiti ambao umefanyika sehemu za vijijini kuhusu shule za watu binafsi na shule za serikali.Iligundulika kuwa shule za watu binafsi ambazo ziko vijijini na zina kila kitu kama vifaa vya kufundishia na kujifunzia, walimu wa kutosha na wenye sifa zinafanya vizuri.

  Swali: Kwa haya uliyoyasema na hata uzoefu wa mambo ulivyo, bila shaka elimu yetu inaporomoka, tufanyeje?
  Jibu: Kutokana na hali ya elimu kuendelea kuporomoka, hakuna haja ya kuendelea kutafakari, bali sasa tuchukue hatua. Haiwezekani kuendelea kulifumbia macho suala hili kwani kufanya hivyo ni kuendelea kujenga taifa lisilokuwa na watu wa kuliendeleza taifa lenyewe
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa ni kichwa..sijui kama ndio yule wa jf ama mwingine
  shule za kata bado ni janga jamani
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  tatizo la nchi yenu arifu mtu akitoa angalizo basi ataitwa mpinzani anajitafutia umaarufu......aliosema kitila sio lazima uwe daktari ujue.....ni wazi ilimu yenu imekaa kimitego tego
   
Loading...