Dk. Mengi: Tanzania inapoteza Sh. trilioni moja kwa bidhaa feki

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi, amesema Tanzania inapoteza zaidi ya Sh. trilioni moja kila mwaka kutokana na bidhaa feki ambazo ni asilimia 35 hadi 45 ya mauzo halali nchini.

Alisema takwimu hizo ni kwa mujibu wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na kwamba moja ya tatizo kubwa ambalo TPSF wanapambana nalo ni uharamia wa bidhaa na bidhaa feki ikiwamo vinywaji, chakula na dawa zinazoweka maisha ya watumiaji mashakani.

Dk. Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa kikao cha wakurugenzi wa kampuni za wajasiriamali wadogo zaidi ya 20 na kampuni ya Microsoft.
Alisema biashara nyingi nchini zimeporomoka kutokana na ushindani usio sawa unaotokana na soko kuvamiwa na maharamia wa bidhaa feki.

Alisema zipo sababu mbalimbali zinazotajwa kuchangia matumizi ya bidhaa feki ikiwamo bidhaa halali kuwa ghali na wafanyabiashara wengi wanazikimbilia kwa lengo la kutengeneza faida kubwa kwa haraka.

Dk. Mengi alisema sababu nyingine hasa bidhaa za mifumo ya kompyuta ni upatikanaji wa bidhaa zenye ubora ambazo zinaambatana na maelezo marefu hadi kuweka kwenye kompyuta, huku feki zikipatikana kirahisi na zenye maelekezo ya haraka.

Alisema sababu nyingine ni kukosekana kwa elimu kwa wateja, ikiwamo kushindwa kutofautisha kati ya bidhaa halisi na feki na kwamba kwa Tanzania watu wengi hawana elimu ya kompyuta na bidhaa zake hivyo wanashindwa kuzitofautisha wanapozikuta sokoni.

“Ujumbe wangu kwenu, haijalishi bidhaa feki ni rahisi kiasi gani, usinunue, usitumie. Tufikiri bidhaa feki za mfumo wa ndani ‘software’ zilivyo rahisi sana kuua biashara yako. Epuka kununua, kuuza na kutumia ‘software’ feki,” alisema.

Nae Mratibu Mkazi Afrika Mashariki na Kati wa kampuni ya Microsoft, Robin Njiru, alisema ni mara ya pili wanakutana na wakurugenzi watendaji wa kampuni za wajasiriamali wadogo kwa lengo la kuwaelimisha.

Mkurugenzi wa kampuni ya Raha, Aashiq Shariff, alisema ipo haja ya kufundisha masomo ya mawasiliano ya habari (IT) kila shule kwa kuwa ni muhimu katika hatua mbalimbali za maisha.

Chanzo: NIPASHE
 
TFDA na mashirika mengine yanaacha bidhaa feki zinaingia nchini, halafu wanakuja kumkomoa mtu wa chini kwa kuteketezza bidhaa alizonunua wakati mwananchi hana macho ya kugundua bidhaa feki, haya mashirika mengine ni ya ajabu sana.
 
Chini ya Mh. Magufuli mambo yote yatanyooka.
Kula kitu Magufuli, atasimamia show ngapi? Kila mmoja wetu atimize wajibu wake na sio kula jambo Magu, basi hata mtoto akiumwa Magu aje ampeleke hospital.
 
Back
Top Bottom