WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema lazima Katiba mpya izingatie matakwa ya wananchi ili kuliweka taifa katika hali ya utulivu.
Amewataka Watanzania kutoiga vurugu zilizotokea kwenye nchi za Libya, Sirya, Tunisia na Misri badala yake waendelee kuwa wavumilivu huku akiwaomba kutotumia maandamano kama suluhu za matatizo ya kiuchumi yanayolikumba taifa na watu wake kwa sasa.
Dk. Magufuli alisema hayo juzi alipohutubia maelfu ya wananchi wakati wa uzinduzi wa Kivuko cha mv Kome II, uliofanyika kwenye Kata ya Nyakarilo, Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema, Mwanza.
Kivuko hicho kimejengwa na kampuni kutoka Uholanzi na kimegharimu zaidi ya sh bilioni 1.6 katika matengenezo yake ili kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa visiwa vya Ntama, Kome, Lugata na Nyakarilo.
Waziri huyo aliitaka tume maalumu ya kukusanya maoni ya upatikanaji wa Katiba mpya itakayoundwa na Rais Jakaya Kikwete itekeleze jukumu hilo bila kuchakachua maoni ya wananchi.
"Hili la Katiba mpya ni jambo mhimu na nyeti, tunataka Katiba ijayo ikidhi matakwa ya Watanzania. Tume itakayoundwa na rais kukusanya maoni ifanye hivyo bila konakona fulani fulani," alisema Dk. Magufuli.
Waziri huyo pia aliwabeza viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Kikwete kuhusu Katiba mpya na kusema taratibu zote zilifuatwa na muswada ulipelekwa na kupitishwa bungeni licha ya wengine kutoka nje.
"Mwanzoni wabunge hao hao walisema hawamtambui rais, lakini sasa wamekuwa wa kwanza kukimbilia Ikulu kuzungumza na rais wasiyemtambua, kuona hivyo rais kawapa chai, juisi na soda wakanywa, kesho yake akasaini muswada wa kupata tume ya Katiba mpya," alisema Dk. Magufuli.
Kuhusu kivuko hicho, alimwagiza Wakala wa Serikali wa Ufundi na Umeme (TAMESA) kuhakikisha wanawafukuza kazi watumishi wazembe na wasiojali kazi zao na kwamba vivuko vyote lazima vifanyiwe matengenezo ya mara kwa mara.
Katika hatua nyingine alimwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, Leonard Kadashi, kuhakikisha mkandarasi anayejenga barabara ya kutoka Sengerema kwenda Nyakarilo anakamilisha mradi huo ndani ya muda vinginevyo afukuzwe kazi.
"Wakati nakuja huku nimekuta mkandarasi ndiyo anatengeneza barabara hii. Na nimeambiwa walianza usiku baada ya kusikia nakuja. Nataka mchezo huu ufe mara moja na barabara hii ikamilike ndani ya muda unaotakiwa.
"Nakuagiza wewe wakala wa barabara mkoa ukimuona huyu mkandarasi analeta uzembe mfukuze kazi maana hadi sasa tulishafukuza makandarasi kama hawa 2,800, sitaki lelemama katika kazi," alisisitiza Dk. Magufuli.