Dk. Magufuli ajitosa Katiba Mpya, awabeza CHADEMA

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema lazima Katiba mpya izingatie matakwa ya wananchi ili kuliweka taifa katika hali ya utulivu.

Amewataka Watanzania kutoiga vurugu zilizotokea kwenye nchi za Libya, Sirya, Tunisia na Misri badala yake waendelee kuwa wavumilivu huku akiwaomba kutotumia maandamano kama suluhu za matatizo ya kiuchumi yanayolikumba taifa na watu wake kwa sasa.

Dk. Magufuli alisema hayo juzi alipohutubia maelfu ya wananchi wakati wa uzinduzi wa Kivuko cha mv Kome II, uliofanyika kwenye Kata ya Nyakarilo, Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema, Mwanza.

Kivuko hicho kimejengwa na kampuni kutoka Uholanzi na kimegharimu zaidi ya sh bilioni 1.6 katika matengenezo yake ili kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa visiwa vya Ntama, Kome, Lugata na Nyakarilo.

Waziri huyo aliitaka tume maalumu ya kukusanya maoni ya upatikanaji wa Katiba mpya itakayoundwa na Rais Jakaya Kikwete itekeleze jukumu hilo bila kuchakachua maoni ya wananchi.

"Hili la Katiba mpya ni jambo mhimu na nyeti, tunataka Katiba ijayo ikidhi matakwa ya Watanzania. Tume itakayoundwa na rais kukusanya maoni ifanye hivyo bila konakona fulani fulani," alisema Dk. Magufuli.

Waziri huyo pia aliwabeza viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Kikwete kuhusu Katiba mpya na kusema taratibu zote zilifuatwa na muswada ulipelekwa na kupitishwa bungeni licha ya wengine kutoka nje.

"Mwanzoni wabunge hao hao walisema hawamtambui rais, lakini sasa wamekuwa wa kwanza kukimbilia Ikulu kuzungumza na rais wasiyemtambua, kuona hivyo rais kawapa chai, juisi na soda wakanywa, kesho yake akasaini muswada wa kupata tume ya Katiba mpya," alisema Dk. Magufuli.

Kuhusu kivuko hicho, alimwagiza Wakala wa Serikali wa Ufundi na Umeme (TAMESA) kuhakikisha wanawafukuza kazi watumishi wazembe na wasiojali kazi zao na kwamba vivuko vyote lazima vifanyiwe matengenezo ya mara kwa mara.

Katika hatua nyingine alimwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, Leonard Kadashi, kuhakikisha mkandarasi anayejenga barabara ya kutoka Sengerema kwenda Nyakarilo anakamilisha mradi huo ndani ya muda vinginevyo afukuzwe kazi.

"Wakati nakuja huku nimekuta mkandarasi ndiyo anatengeneza barabara hii. Na nimeambiwa walianza usiku baada ya kusikia nakuja. Nataka mchezo huu ufe mara moja na barabara hii ikamilike ndani ya muda unaotakiwa.

"Nakuagiza wewe wakala wa barabara mkoa ukimuona huyu mkandarasi analeta uzembe mfukuze kazi maana hadi sasa tulishafukuza makandarasi kama hawa 2,800, sitaki lelemama katika kazi," alisisitiza Dk. Magufuli.
 
Dkt. Magufuli kitu kinaweza kufuata taratibu zote but is sub-standard. Be careful with what you say. Watanzania sasa wajua mambo kulivyo unavyoweza kufikiria
 
Dr. Magufuli, achana na hizo longolongo za kisiasa za chama chako. Tunakujua na kukuaminia kuwa wewe ni mchapa kazi, hizo ngonjera za ubabaishaji waachie kina Kikwete ndo zao.

Btw, nakupongeza kwa hilo la kutaka mkandarasi mzembe apigwe chini. Waangalie kwa macho mawili hao kina Kadashi, wanakula na wakandalasi hao, watakuangusha.
 
Unafanya research:
population mikoa 26..... sample mikoa 3..... time to collect data siku mbili tu...... haya ni maajabu ya kuunda katiba BORA zaidi Tanzania
 
Magufuli ni fisadi, nani asiemjua! Aende huko, anasema sababu yupo chama cha magamba, cdm wangekuwa na dola angewasifia pia.
 
Dr. Magufuli, achana na hizo longolongo za kisiasa za chama chako. Tunakujua na kukuaminia kuwa wewe ni mchapa kazi, hizo ngonjera za ubabaishaji waachie kina Kikwete ndo zao.
Btw, nakupongeza kwa hilo la kutaka mkandarasi mzembe apigwe chini. Waangalie kwa macho mawili hao kina Kadashi, wanakula na wakandalasi hao, watakuangusha.

Mnamjua wewe na nani??
 
Magufuli licha ya uchapa kazi wake, bado ana mawazo ya kizamani sana, hajui kuwa maandamano ni moja ya njia ya kudai haki.

Wafanye kazi, watoe haki sawa, then hakutakuwa na maandamano
 
Mwanzoni wabunge hao hao walisema hawamtambui rais, lakini sasa wamekuwa wa kwanza kukimbilia Ikulu kuzungumza na rais wasiyemtambua…kuona hivyo rais kawapa chai, juisi na soda wakanywa, kesho yake akasaini muswada wa kupata tume ya Katiba mpya," alisema Dk. Magufuli.

Unaweza usiamini, lakini ndo hivyo.
 
Nafikiri magufuli apewe uenezi sababu Siku tangu aitwe dr.sio yule mchapaka kazi aliyejulikana ndani ya harass la mawaziri!mh.unakera sana na siasa za Maji taka zenu na zaidi Siku bidi hufanyi kazi unajipendekeza kwa maboss .
 
Nimeota leo kwamba KATIBA MPYA IJAYO ITAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YANAYOFANYWA NA VYAMA VYA SIASA ili kulinda amani na uvunjifu wa amani nchini Tanganyika.
 
Nashangaa wengi wetu tunasahau kuwa UKAWA walijiunga kwa dhumuni la kupata katiba mpya ya wananchi.

Sasa naskia kelele nyingi kuhusu Magufuli na uchapakazi, je ataifanyia kazi katiba mpya ili tuipate katiba ya wananchi kama yalivyo malengo ya UKAWA?

kwasababu nimeona wengi wanampambanisha Magufuli na UKAWA, nikakumbuka madhumuni halisi ya UKAWA, nikaona kwamba kumbe ni Magufuli vs katiba ya wananchi!

Kama wananchi si wasahaulifu, basi kwenye kupiga kura hapo October, misimamo wa wagombea na vyama vyao kuhusiana na katiba mpya, utakuwa one of the main deciding factors!
 
Makufuli vipi sheria ya gesi anaikubali sasa kama anaikubali vipi anawambia watanzania anaweza kuleta maendeleo?
 
Back
Top Bottom