Dk. Magufuli ajitosa Katiba Mpya, awabeza CHADEMA

Kwa Tanzania yetu hii,,,watu wameshasahau kama walichakachuliwa katiba yao mimi naona hakuna jipya
Ndo bongo hiii bwana! Wepesi wa kusahau unatisha!

Katiba ya kifisadi itakuwa imepita ili kutengeneza mafisadi wengine wapya!
 
Sita wamemaliza kisiasa kwa hiyo hiyo Katiba ya kulazimisha. Huyu naye si alikuwa mmoja wao. Leo hii tena
 
Mwanzoni wabunge hao hao walisema hawamtambui rais, lakini sasa wamekuwa wa kwanza kukimbilia Ikulu kuzungumza na rais wasiyemtambua…kuona hivyo rais kawapa chai, juisi na soda wakanywa, kesho yake akasaini muswada wa kupata tume ya Katiba mpya,” alisema Dk. Magufuli.

Unaweza usiamini, lakini ndo hivyo.

Wananchi wa leo wanaukataa mfumo mbovu uliopo ndani ya ccm kauli mbiu mwaka huu UKAWA kwanza Magufuli badaadaeee.
 
Wananchi wa leo wanaukataa mfumo mbovu uliopo ndani ya ccm kauli mbiu mwaka huu UKAWA kwanza Magufuli badaadaeee.

Endelea kuzoea taratibu,uchaguzi wa Rais ushaisha jumapili iliyopita.Magufuli anasubiri kuapishwa tu.
 
magufuli amewekewa msaidizi ambaye aliongoza uchakachuaji wa maoni ya wananchi kwenye suala la katiba mpya. magufuli hana jipya ni wanaccm walewale..
 
Watanzania tusitegemee Magufuri kufanya vitu tofauti ndani ya CCM kwani tatizo ni MFUMO na sio yeye.

Hivo Mafisadi wa Escrow wataendelea kulindwa,Nyumba alizoziuza kifisadi hazitarudishwa,Mikataba ya Siri ya Mafuta na Gesi haitawekwa wazi.

Tusijidanganye na mtu kwani tatizo ni CCM na ndio kinatakiwa tupiganie ili kitoke madarakani na si vongonevyo
 
Magufuli aje kutuambia je, zina million 156 daily capacity charge wataendelea kulipwa DOWANS/RICHMOND?

Je, wakulima na masikini wa Tanzania watandelea kunyonywa kupitia mafuta taa bei juu?

Je, Magufuli atuambie zile Million 700 ni za nini?

je mfupa alioushindwa mkapa, yeye atauweza?

Je, Pombe magufuli,,,, utalinda wazee waliofilisi nchi na maakiba yao USWISS?

Je Magufuli... Pesa za USWISS utarudisha..

Je waziri Wa ujenzi utamteua nani?

Waziri wa fedha ni Saada Mkuya tena

Je magufuli, shillingi yetu vipi
 
Habarini wakuu,

Naomba kujulishwa kuwa Mgombea urahisi wa CCM, bwana John Magufuli anasemaje kuhusu ile katiba inayotakiwa na Wananchi wa Tanzania?

Je ataibariki au ataiendeleza ile yenye maslahi ya Wachache na isiyotakiwa na Wananchi? Kwakuwa sikuwahi kumsikia akiiongelea.

Msaada wenu tafadhali.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom