Dk. Kitine: Mtandao wa JK umeivuruga nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Kitine: Mtandao wa JK umeivuruga nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 8, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,359
  Trophy Points: 280
  Dk. Kitine: Mtandao wa JK umeivuruga nchi
  [​IMG]
  Na Mwandishi wetu - Imechapwa 01 June 2011

  [​IMG][​IMG]Ndani ya Jamii

  [​IMG]


  DK. Hassy Kitine, kada wa muda mrefu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameibuka na kutema nyongo. Anasema kuzorota kwa chama chake kisiasa hadi kufanya vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita, kumesababishwa na viongozi wake kuacha misingi yake ya asili.

  Katika mahojiano yake na MwanaHALISI wiki iliyopita nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Kitine anasema kudhoofika kwa CCM kumeletwa na kushindwa kusimamia maadili.

  Amesema, "Kudhoofika kwa CCM kisiasa; kupotea kwa mwelekeo wake na kupotea kasi na umaarufu wa chama hiki, kwa kiwango kikubwa kumechangiwa na hatua ya baadhi ya viongozi kushindwa kusimamia miiko ya uongozi na maadili ya chama chetu."

  Anasema kama chama chake kinataka kurejesha heshima yake kiliyokuwanayo huko nyuma, sharti kijitazame upya na kijirerejeshe kwa wanachama wake. Viongozi wake ni lazima waachane na tabia ya kukumbatia wenye fedha, jambo linalokidhalilisha chama kwa kuonekana mbele ya umma kuwa ni chama cha wenye fedha.

  Anasema viongozi waliopewa dhamana waangalie sana uteuzi wa viongozi katika nafasi za ubunge na udiwani, ambako ndiko malalamiko yanaanzia.

  "Leo ndani ya CCM, uongozi unanunuliwa…Rushwa ndiyo msingi wa mtu kuchaguliwa. Tukitoe chama chetu huko," anaeleza kwa sauti ya unyonge.

  Kingine ambacho Dk. Kitine anasema kimechangia kuzorota kwa chama chake, ni kile alichoita, "Mbegu chafu ya wanamtandao."

  Kundi hilo lililoundwa mara baada ya kumalizika kinyang'anyoro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, lilifanya kazi kubwa ya kuchafua wanachama na viongozi wa chama hicho waliojitokeza kusaka urais.
  Anasema kundi la mtandao lililoundwa maalum kwa ajili ya kumuingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete, nalo lazima libebe lawama kwa kuchangia kukivuruga chama chake.

  Kwanza, kwa hatua yake ya kumchafua kila aliyeonekana tishio katika kinyanganyiro cha urais mwaka 2005. Lakini pili ni kutokuwapo mipango thabiti ya kutekeleza pindi mpango wa kuingia ikulu utakapofanikiwa.

  Dk. Kitine ambaye aliwahi kuwa waziri wa utawala bora wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, mkurugenzi wa usalama wa taifa, mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anasema viongozi wa mtandao waliaminisha kila mmoja kuwa Kikwete ndiyo mwisho wa matatizo ya wananchi, jambo ambalo lilisababisha wananchi wengi kumuamini.

  Anasema, "Mtandao uliofanya kazi ya kumuingiza Rais Kikwete madarakani hauwezi kuachwa katika hili la kudhoofika kwa chama chetu. Ni kwa kuwa mtandao ulifanya kazi ya kutafuta ikulu kwa udi na uvumba, lakini ukiwa haujui ukifika ikulu utafanyia nini wananchi."

  Dk. Kitine anataja waliochafuliwa kwa kutaka urais kuwa ni pamoja na mwanadiplomasia anayeheshimika duniani, Dk. Salim Ahmed Salim ambaye wanamtandao walimzushia kuhusika na mauaji ya rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume na ujio wa chama cha Hizbu.

  Anasema, "Haya yote yamejenga ufa mkubwa ndani ya chama na yamechangia kukidhoofisha chama chetu. Si jambo jema kumtungia mtu tuhuma za uwongo kwa sababu ya urais."
  Anasema hata tuhuma dhidi yake kuhusiana na matibabu ya mkewe nje ya nchi, zililenga mbio za urais mwaka 2005.

  "Hata mimi nilichafuliwa katika mazingira hayohayo. Nikiwa waziri wa kwanza wa utawala bora nchini baada ya kuundwa kwa wizara hiyo mwaka 1997, nilidhaniwa nitagombea urais au nitakuwa na ushawishi kwa mmoja wa wagombea. Wakaamua kunisakama hadi nikaondoka," anasema Dk. Kitine huku akishusha pumzi.

  Akiongea kwa kujiamini, Dk. Kitine anasema alipokuwa ikulu aliweka utaratibu wa watu wachafu kutomkaribia rais au ikulu kugeuzwa kijiwe cha soga, jambo ambalo liliwaudhi wengi.

  Anasema, "Sasa kuona hivyo, wale waliokuwa wanataka kugeuza ikulu kijiwe cha soga wakaungana na wale waliokuwa wanatafuta urais na kuanza kunisakama; katika mambo yanayohusu nchi, hakuna anayemuogopa."

  Alipoulizwa kwa nini anadhani hatua yake ilimsababishia kusakamwa na wetu wengi, wakiwamo hasa wale aliodai kuwa walikuwa wanautafuta urais, Dk Kitine aliishia kujibu, "…Inatosha kusema yale yamepita na nimeshasamehe."

  Mwaka 1997 mara baada ya kushinda kiti cha ubunge katika jimbo la Makete, rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa alimteua Dk. Kitine kuwa waziri wa utawala bora, jambo ambalo lilizusha minong'ono mingi kuwa anaweza kuwa miongoni mwa watakagombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

  Wizara hii iliundwa mara baada ya rais Mkapa kupokea ripoti ya tume ya Jaji Joseph Warioba ambayo sehemu kubwa ya mapendekezo yake yalilenga udhibiti wa mianya ya rushwa serikalini.

  Uchaguzi mdogo wa Makete ulikuja kufuatia kifo cha Tumtemeke Sanga ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo. Wakati Dk. Kitine anagombea ubunge wa Makete alikuwa mkuu wa mkoa wa Tanga.

  Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, Dk. Kitine alijitosa katika kinyang'anyiro cha ubunge katika jimbo la Iringa Mjini. Ingawa alipenya katika kinyang'anyiro cha kura za maoni kwa kuwamwaga washindani wenzake zaidi ya 10, lakini alipoingia katika ushindani na wagombea wa vyama vingine vya siasa, Dk. Kitine alishindwa na mgombea wa chama cha NCCR-Mageuzi, Kibaasa.

  Hata hivyo, mwenyewe anasema kushindwa kwake katika kiti cha ubunge Iringa Mjini kulitokana na anachokiita "fitina za kisiasa." Anasema fitina hizo zilijikita katika ukabila na udini. Ziliibuliwa na washindani wake ndani ya chama chake.

  Kitine alizungumzia pia hatua ya CCM kutaka kuwachukulia hatua watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini – Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge.
  Anasema chama chake kitafute ushahidi wa kutosha na kisha kiwape nafasi wanaotuhumiwa kujitetea, kisha ikithibitika kuwa wametenda makosa wanayotuhumiwa waondolewe moja kwa moja kwenye chama.
  Hatua kama hizo zichukuliwe pia kwa wale wanaotuhimiwa kuanzisha Chama cha Jamii (CCJ) wakati wakiwa bado wanachama wa CCM.

  Wanaotuhumiwa kuanzisha chama ndani ya chama, ni pamoja na Samwel Sitta, Dk. Harrison Mwakyembe, Nape Nnauye na Victor Mwambalaswa.
  "Hili la hawa walioanzisha chama ndani ya chama na wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi, ni lazima chama chetu kitafute ushahidi wa kutosha na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika kufuatana na katiba na taratibu za chama," ameeleza.
  Anasema kuanzisha chama ukiwa bado ndani ya chama ni kosa ambalo haliwezi kuachwa bila kutolewa maelezo.

  "CCM kisifanye parapara. Pamoja na kwamba kumfukuza mtu ndani ya chama ni hatua kubwa, lakini utafutwe ushahidi; ikithibitika kwamba hawa watu walishiriki katika kuazishwa kwa chama wakiwa bado ndani ya CCM, basi wawajibishwe," ameeleza.

  Anasema, "Ushahidi huu lazima ueleze ushiriki wa kila mmoja. Ukipatikana wote wafukuzwe."
  Akizungumzia matatizo yaliyopo katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Dk. Kitine anasema wakati umefika wa mataifa hayo mawili kila mmoja kujiamulia mambo yake.

  "Baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliniambia muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda Uingereza, '…nadhani sasa wakati umefika kwa Zanzibar kuachwa kujiamulia mambo yake,'" anaeleza Dk. Kitine akimnukuu Nyerere.

  Anasema, "Mwalimu alifikia hatua hiyo baada ya kuona Zanzibar kila siku hawaishi malalamiko. Nami naona sasa wakati umefika wa Zanzibar kutengana na Bara. Tufungue mjadala, wananchi wajadili suala hili na wakiona kuwa Muungano uvunjike, basi tufanye hivyo kwa amani na utulivu."

  Anasema hilo ni muhimu kuliko kusubiri nchi kuingia katika machafuko. "Tujadili kwa uwazi jambo hili. Kama tutavunjika tuwe na utaratibu wa undugu kushirikiana. Kuogopa tatizo hili, kunaweza kutuingiza katika matatizo mengi makubwa huko mbele."

  Anasema, "Tufike mahali tuamue kama tunataka Muungano, basi uwepo. Kama hatuutaki, basi tuachane nao kwa salama na kisha tutafute njia ya kuishi kwa umoja na amani kama ndugu," anaeleza.

  Anasema katika kufikia suluhu ya malalamiko ya Muungano, serikali iruhusu kuitishwa kwa kura ya maoni na kila upande wa Muungano uruhusiwe kupiga kura yake.
   
 2. FREEHERMAN

  FREEHERMAN Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Mheshimiwa ameshindwa kusafisha chama chake sababu yeye mwenyewe mzigo uliowekwa kama ngao ya kuwalinda mafisadi nyuma yake kwa kutumia cheo chake
   
 3. Kinyasi

  Kinyasi Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Kudos Kitine. Wape wana Magamba maneno yao bila kumung'unya. Siku chama cha Magamba kikienda na maji yatokanayo na Nguvu ya umma au sanduku la kura, basi Historia itaandikwa kuwa ulikuwa ni mmoja wanaMagamba wachache waliotoa taadhari iliyopuuzwa kwa maslahi ya kuwalinda mafisadi wakiongozwa na Juma Kilaza.
   
 4. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kumbe siasa zao za uzushi walianzia kwa Salim Ahmed Salim kisa tu madaraka. Kweli huyu mtu hatari sana. Naona hii dhambi ya uzushi inamtafuna taratibu. Kweli what goes around comes around.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  asante mwenyekiti wangu wa bodi pale FAIDIKA....asante sana.
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Huyu Kitine mwenyewe alivuliwa 'GAMBA' kwa ufisadi, sijui ameoga sabuni kiasi gani hadi akawa msafi?
  Hatujasahau jinsi alivyoshiriki fitna dhidi ya Jenerali Ulimwengu hadi akanyang'anywa uraia.
   
 7. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Walianza kwake Kitine, wakaja kwa Frederick Sumaye, wakaja Salim A Salim. Wakiwatumia waandishi tambala la deki kama Salva Rweye, P Bagenda, the goes on.
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Na wanaendelea kwa Lowasa(wameshatamka wazi kuwa anataka urais baada ya JK), wakamuunganisha na Chenge+Rostam ati kwa kuwa ni financial partner wao. Lakini hawajamuacha nyuma Mr pombe(wameshamzushia kashfa ya kumuzia nyumba mdogo wake). All in all yafurahisha kuwa chama kisiombe huruma ya wananchi kuwasurubu watuhumiwa(hii ni hatari kwa jamii) bali kitafute ushahidi na kichukue hatua kwa kufuata miongozo. Bravo hans.
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Kama ali-facilitate kumchukulia hatua jenerali ul namuunga mkono kwani JU mwenyewe hakulalamika bali alifanya kile kinachotakiwa kwa kuwa aliona kuwa amechukuliwa hatua sahihi: sijui wewe unahoja gani vs this unless wewe ni "type" ya wale wanao hudumia mataifa na/au empire mbili.
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Utaratibu walioutumia au wanaoutumia kuingia madareakan ndio unaowahukumu kwa sasa,unawagarimu na unatugarimu raia
   
 11. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Na sasa amewageukia watumishi wa Mungu kuwa wanajihusisha na madawa ya kulevya badala ya kuwataja wahusika
   
 12. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nadhani akina EL hawajajua kama JK anawazunguka. Nadhani kuna haja ya kuthubutu wakatoka mbele ya watu wakasema yote peupe pe ili watu wajuwe tatizo halisi ni nini kuliko kunung'unika wakiwa ndani!

  Wasipofanya hivyo basi umma utajua ni kweli na watampa point JK. Kwa hali ya nchi ilivyo sidhani kama kuna sababu ya kucompromise maana hakuna atakaye pona. Jk anajidanganya kuwa anaweza kutuchagulia Rais wake 2015 naye EL anadhani anaweza kuwa Rais 2015. Hizi zote ni ndoto maana daraja la kuwavusha kuingia huko ni CCM ambayo haipo tena!

  Nadhani wanatakiwa kufanya "WOTE TUKOSE" maana hakuna atakayepata anyway.

  EL aingie mkataba na CDM wa kutomshitaki kwa ufisadi wakiingia Ikulu ili atoboe siri kuu iliyojificha katika serikali hii ya magamba kwa faida ya nchi.
   
 13. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Jk kweli kazi anayo. Anapambana na akina lowasa, Chadema na sasa ameongeza listi- anawatuhumu viongozi wa dini kuuza unga. wananchi wanalalamika maisha magumu. Huyu asipojiuzulu kabla ya 2015 ana bahati sana.
   
 14. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Yaani jk sasa ivi kila kukicha anatamani aachie kiti akimbie lakini wapi!!!kazi ipo mwaka huu!!!
   
 15. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  mungu ni mkubwa..watasema yoooteeee.....bora huyu lakini sijui Nape umemsikia?
   
Loading...